JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: MAHUSIANO KATI YA MAAFISA WA POLISI KUPIGWA MARUFUKU

- Serikali inaandaa Kanuni zitakazozuia Polisi kuoana au kuwa na mahusiano na Polisi wenzao

- Hatua hiyo inalenga kupambana na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na mauaji

Soma > https://jamii.app/NdoaPolisiKE
JAMIIFORUMS INAKUTAKIA 'WEEKEND' NJEMA

> Tunawatakia Watembeleaji wa JamiiForums.com na wafuatiliaji wa kurasa zetu kwenye Mitandao ya Kijamii mwisho mwema wa Juma

> Tembelea JamiiForums.com na ujisajili kwa kubofya 'Register' na kisha fuata maelekezo

#JamiiForums #TGIF
KUPAMBANA NA #COVID19: MITAMBO YA OKSIJENI YASIMIKWA KUBORESHA HUDUMA

Serikali imesema uwekezaji huo utaweza kujibu changamoto kipindi cha mlipuko wa #COVID19

Imesimikwa Hospitali 7 za Rufaa na inalenga kuzalisha mitungi 200 ya Oxygen kwa saa 24

Soma - https://jamii.app/MitamboHewa
TANGA: WATU WAWILI WAUAWA NA TEMBO NDANI YA WIKI 1

> Tembo waliovamia makazi ya Watu ktk mtaa wa Malezi wapelekea Wananchi kuishi kwa hofu

> Aprili 30, 2021 asubuhi, Mtu wa pili aliuawa alipokuwa na wajukuu zake wakichimba mihogo ya futari

Soma - https://jamii.app/TemboHandeni
TUCTA: WAFANYAKAZI KUTOONGEZEWA MISHAHARA KUMEPUNGUZA ARI YA KAZI

- Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA asema Mishahara haijaongezwa kwa miaka 8 kwa Sekta isiyo rasmi na miaka 6 kwa Sekta ya Umma

- Asema "Gharama zimezidi kupanda, stahiki zimeendelea kuwa duni"

Soma https://jamii.app/MishaharaWafanyakazi
RAIS MWINYI: CORONA ILISABABISHA SHIDA HATA KWENYE ULIPAJI MISHAHARA

- Asema Wataalamu wakiwemo Walimu na Watumishi wa Afya wanastahili kufikishwa sehemu nzuri ya mishahara

- Amesema Uchumi ukiimarika Serikali ya Awamu ya 8 itaanza na kada ya kati

Soma https://jamii.app/MwinyiMishahara
SERIKALI YAPUNGUZA PAYE KWA 1%

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu ametangaza punguzo ya Kodi ya 'Lipa kadiri unavyovuna' (PAYE) kutoka 9% hadi 8% ili kuwapa unafuu watumishi

> Hii imetokana na ombi la Katibu Mkuu wa TUCTA kuomba kupunguziwa kodi hiyo kwenye mishahara

Soma > https://jamii.app/RaisMeiMosi
MAKATO YA HELSB KUBAKI 15%, β€˜VALUE RETENTION FEE’ YAONDOLEWA

- Rais Samia Suluhu ametangaza kuwa Makato ya Mikopo ya Elimu ya Juu yatabaki kuwa 15% huku akiondoa tozo ya kutunza thamani ya Fedha za Mkopo (6%) inayotozwa kwa mwaka katika deni lililosalia (Outstanding Loan Balance)

#JamiiForums
RAIS SAMIA ATAJA COVID19 KUWA MOJA YA SABABU MISHAHARA KUTOPANDISHWA

> Rais Samia Suluhu amewapa pole Watumishi wa Umma kwa kuwa hawezi kuongeza mishahara kwa mwaka huu, labda mwaka ujao wa fedha

> Ametaja Corona kuwa kati ya sababu za kushindwa kuongeza mishahara

Soma https://jamii.app/RaisMeiMosi
TUCTA YAPENDEKEZA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA KIWE TSH. 970,000

> Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA amesema wamefanya tafiti kubaini kiwango cha mshahara ambacho kinaweza kumtosha mtumishi kuendesha maisha yake ni 970,000

Soma https://jamii.app/MinimumWage
#JamiiForums
AUSTRALIA YAPIGA MARUFUKU RAIA WANAOTOKEA INDIA KUREJEA NCHINI HUMO

- Ni sehemu ya Kanuni zinazolenga kuzuia wasafiri wakati India inapambana na #COVID19

- Ni mara ya kwanza kwa Australia kufanya kitendo cha Raia kurejea nyumbani kuwa kosa la jinai

Soma https://jamii.app/AusBanIndia
KOMBE LA SHIRIKISHO: SIMBA KUKABILIANA NA KAGERA SUGAR

- Klabu ya Simba ambayo ni bingwa mtetezi wa kombe itakutana na Kagera Sugar majira ya saa 1:00 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mchezo mwingine unaoendelea ni kati ya Dodoma Jiji dhidi ya KMC Fc

- Washindi wa #Michezo ya leo wataungana na Yanga na Mwadui ambazo zimetinga robo fainali ya michuano baada ya Yanga kuifunga Tz Prisons 1-0 na Mwadui kuiadhibu Coastal union goli 2-0

#JamiiForums #Sports
HUAWEI YAJIPANGA KUWA NA KASI YA 6G JULAI 2021

> Wakati Afrika inapambana na teknolojia ya 3G. Kampuni ya Teknolojia ya Huawei inajaribu kwa mara ya pili teknolojia ya 6G

> 6G inatarajiwa kuwa na kasi mara 100 ya kasi ya 5G

Soma https://jamii.app/Huawei6G
#JFTeknolojia
JE, FILAMU ZAKO PENDWA ZA KIVITA NI ZIPI?

> Ziko filamu nyingi za kivita zilizokonga nyoyo za watazamaji kiasi cha Watu kujivisha uhusika wa filamu. Mfano kufunga usongo kama Rambo ili kupigana

> Je, unazikumbuka filamu gani za kivita zilizokukosha?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/FilamuZaKivita
KOMBE LA SHIRIKISHO: SIMBA NA DODOMA JIJI ZATINGA ROBO FAINALI

- Michezo ya hatua 16 bora imemaliza kwa timu za Simba SC na Dodoma Jiji kusonga mbele katika hatua ya robo fainali

- Simba imeibuka kidedea kwa kuifunga Kagera Sugar goli 2-1 huku Dodoma Jiji ikiifunga KMC FC goli 2-0

- Simba na Dodoma Jiji zinaungana na Yanga SC na Mwadui FC katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo

#JamiiForums #JFSports
SOMALIA: BUNGE LAPIGA KURA KUMFUTIA RAIS NYONGEZA YA MUDA

- Ni baada ya hatua hiyo iliyoidhinishwa mwezi Aprili kuibua mvutano mkubwa

- Kuna wasiwasi waasi wa Al Shabaab wanaweza kutumia nafasi hiyo kuhatarisha hali ya usalama Nchini humo

Soma > https://jamii.app/BungeSomalia
WADAU WALALAMIKIA HALI YA STENDI YA KAGERA

> Mdau wa JamiiForums ameandika kuwa Stendi Kuu ya Mkoa wa Kagera haiko ktk hali nzuri mbali na kutumiwa na wageni wa nchi jirani

> Mdau amedai bajeti ya Wizara ya OR-TAMISEMI haijaongelea Stendi hiyo

Soma https://jamii.app/StendiKagera
SAMSUNG YAIPIKU APPLE KWENYE MAUZO YA SIMU ROBO YA KWANZA YA MWAKA

- Kampuni hiyo imeteka soko kwa 22%, ikiuza takriban simu Milioni 76.5 ikilinganishwa na Apple iliyouza simu Milioni 52.4 na kuambulia 15% tu ya soko kuanzia Januari hadi Machi 2021

Soma https://jamii.app/SamsungVsApple
MNYIKA: TULIJUA NYALANDU NA SELEMAN WANGEHAMA

> Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema walifahamu Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew wangeondoka kutokana na mienendo waliyokuwa wakiionesha kwa hivi karibuni

Soma https://jamii.app/MnyikaWasaliti
#JFLeo #JamiiForums