JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI KENYA

> Rais wa #Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku mbili nchini #Kenya

> Anatarajia kufanya ziara hiyo kuanzia Mei 4, 2021 ambapo atapokelewa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Soma https://jamii.app/ZiaraKenya
INTER MILAN YAWA BINGWA WA β€˜SERIE A’

- Inter chini ya Kocha Antonio Conte imekuwa Bingwa baada ya Sassuolo kutoka sare ya goli 1-1 na Atalanta iliyo nafasi ya 2

- Ushindi huu tangu ishinde taji hilo 2009/10 umemaliza utawala wa miaka 9 wa Juventus kushinda taji hilo

#JFSports
MECHI YA MANCHESTER UNITED DHIDI YA LIVERPOOL YAAHIRISHWA

- Ni baada ya mashabiki takriban 200 wa Man. Utd kuvamia Old Trafford kupinga Umiliki wa familia ya Glazer katika Klabu hiyo

- Man. Utd imesema EPL itapanga upya tarehe ya mchuano huo muhimu kwa Ligi Kuu

#JFSports
TUANZE WIKI KWA ARI YA KAZI

> Habari yako Mdau wa JamiiForums. Tunakutakia kila la kheri kwenye kazi zote njema utakazozifanya wiki hii

> Tunashukuru kwa kuwa nasi na kukusihi kuendelea kutufuatilia ili kupata taarifa na maarifa mbalimbali

#JFLeo
JUKUMU LA KULINDA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI SIO LA SERIKALI PEKEE

> Mei 3 ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari na Maadhimisho yanafanyika Jijini Arusha

> Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, asisitiza kuweka maslahi ya Taifa mbele

Soma - https://jamii.app/FreePress
#MediaRights
NIGERIA YAPIGA MARUFUKU WASAFIRI KUTOKA INDIA, BRAZIL NA UTURUKI

- Watu wenye Hati za Kusafiria zisizo za Nigeria na waliozuru Mataifa yaliotajwa siku 14 kabla ya kwenda #Nigeria, watanyimwa ruhusa ya kuingia kuanzia Mei 4 kutokana na #COVID19

Soma - https://jamii.app/NigeriaBanIndia
WAZIRI UMMY: NI MARUFUKU SHULE KUWADAI CHETI WANAOANZA DARASA LA KWANZA

- Amesema "Bado hatujafanya vizuri ktk kuongeza 'access' ya Watoto kuanza Elimu ya Awali. Haileti mantiki kusema kila Mtoto aanze Darasa la 1 akiwa na Certificate ya Awali"

Soma > https://jamii.app/ShuleCheti1
LSF: KUPATA TAARIFA NI HAKI YA MSINGI YA KILA MTU

- Mkurugenzi wa Shirika la Legal Services Facility (LSF) Lulu Ng’wanakilala amesema ili kuwa na Jamii yenye maendeleo nyanja zote ni muhimu kuwa na taarifa sahihi zitakazowawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi

- Amesema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari ambayo kilele chake kinafanyika Arusha

- Ameeleza, "Tunapoadhimisha Siku hii ya #UhuruWaHabari napenda kusisitiza kuwa kupata taarifa ni Haki ya msingi ya kila mtu"

Soma > https://jamii.app/PressFreedomDay

#WPFD #WorldPressFreedomDay #AccessToInformation
TEF: MWAKABIBI AMEKUWA AKIKAMATA WAANDISHI, TUNAPONGEZA HATUA ZILIZOCHUKULIWA

- Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile amesema aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri Temeke, Lusabilo Mwakabibi amekuwa akikamata waandishi na kuwaweka ndani na wanaipongeza Serikali kwa kuchukua hatua ya kumsimamisha kupisha uchunguzi

- Amesema Kumekuwa na wimbi la Watendaji wa Serikali na baadhi ya Askari kuwanyang’anya Wanahabari vitendea kazi na kuwashikilia bila sababu za msingi na wanakemea matukio hayo kama Wanahabari

Soma > https://jamii.app/PressFreedomDay

#WPFD #WorldPressFreedomDay #AccessToInformation
- Wabunge hao wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA, Halima Mdee, walifukuzwa uanachama Novemba 27, 2020 baada kwenda Bungeni kuapishwa kuchukua nafasi za viti maalum

- Akizungumza leo Bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu, Ndugai amewataka Wabunge hao wachape Kazi kwa kuwa wako mikono salama, huku akionya Vyama viache kuwanyanyasa Wanawake
NYALANDU: KABLA YA UCHAGUZI, NILIPIGIWA SIMU KUAMBIWA MGOMBEA URAIS WANGU HANITAKI

- Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kupitia CHADEMA, Lazaro Nyalandu, amesema β€œKuna mitihani ilitokea kwenye Uchaguzi. Kulikuwa na chaguzi za aina mbili, moja ni kupigiwa kura kwenye Kamati kisha Baraza Kuu. Kwenye Kamati Kuu nilipata 100%, kilichotokea Viongozi wakasema Nyalandu asije akawa kama Lowassa”

Soma - https://jamii.app/NyalanduChadema
#Siasa
UHURU WA HABARI: TANZANIA IMESHUKA NAFASI 53 NDANI YA MIAKA 4

- Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodatus Balile amesema Tanzania imeshuka nafasi 53 ndani ya miaka 4 katika orodha ya dunia ya #UhuruWaHabari na jambo hilo linapaswa kuangaliwa kwa kina

- Balile amesema wanampongeza wazi Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alifungulia Vyombo vya Habari katika hotuba yake Aprili 6, 2021

- Hata hivyo amesema, "Tunasikitika kuwa baada ya muda mfupi agizo hili pana lilitolewa tafsiri finyu na baadhi ya Watendaji wa Serikali"

Soma > https://jamii.app/PressFreedomDay

#WPFD #WorldPressFreedomDay #AccessToInformation
UNESCO: UHURU WA HABARI NI MSINGI WA DEMOKRASIA

- Kiongozi na Mwakilishi wa UNESCO Tanzania, Tirso Dos Santos amesema #UhuruWaHabari ndio msingi wa Demokrasia ya kweli na kufikia jamii yenye Amani na Haki

- Amesema wamechagua maeneo 5 muhimu ya mjadala kwa manufaa ya Tanzania ambayo ni Uhuru na Kujitegemea kwa Vyombo vya Habari, Maendeleo ya Rasilimali Watu na Uwezeshaji wa Wanawake kwenye Vyombo vya Habari

- Mengine ni Mazingira ya Kisheria na hali ya utendaji kazi, Ulinzi na Usalama wa Wanahabari na Uelewa wa Vyombo vya Habari na Taarifa pamoja na teknolojia ya kidijitali

Soma > https://jamii.app/PressFreedomDay

#WPFD #WorldPressFreedomDay
TEF: UTAYARI WA KUFANYIA MABADILIKO SHERIA ZA HABARI ISIWE AHADI HEWA

- Jukwaa la Wahariri (TEF) limeomba utayari wa Serikali kufanya mabadiliko ya Sheria za Habari isiwe ahadi hewa na utekelezaji wake ufanyike haraka

- Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile ameomba Sheria za Media Services Act, Cybercrimes Act, Statistics Act, Access to Information Act na Online Content Regulations zifanyiwe mabadiliko katika sehemu zinazominya #UhuruWaHabari

Soma > https://jamii.app/PressFreedomDay
BASHUNGWA: MITANDAO ITUMIKE VYEMA, KUNA WATU WAMEJIKITA KWENYE UPOTOSHAJI

- Waziri wa Habari, Innocent Bashungwa, amesema Serikali inatoa jukwaa kwa watu kupata Haki ya kupata na kutoa taarifa lakini wapo wachache wanaotumia kichaka hicho kwenda tofauti na maadili ya Uandishi

- Amesema, "Kuna watu wamejikita kufanya upotoshaji kwenye mitandao na wana vikosi vyao wanavyovitumia. Tujitahidi kutumia majukwaa haya vyema ili tusiwaathiri wengi wanaotumia mitandao kwa manufaa mema"

- Ameongeza kuwa Habari ni mhimili muhimu katika kujenga Nchi na ndio daraja la kushirikisha wananchi katika shughuli za Maendeleo

#WPFD #UhuruWaHabari
COLOMBIA: MAANDAMANO YAPELEKEA SERIKALI KUFUTA MUSWADA WA KUONGEZA KODI

- Awali, Rais alisema ongezeko la Kodi lilihitajika kukabiliana na mdororo wa kiuchumi uliosababishwa na Corona

- Muswada ulikasirisha wananchi na kupelekea maelfu kuandamana

Soma https://jamii.app/ColombiaTaxBill