JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ISRAEL: WATU 44 WAFARIKI DUNIA KWA KUKANYAGANA

- Vifo hivyo vimetokea katika tamasha la kidini ambapo wengine wamejeruhiwa

- Imeripotiwa maelfu walihudhuria tamasha hilo ambalo limetajwa kuwa kubwa zaidi Israel tangu kuanza kwa #COVID19

Soma https://jamii.app/44DieIsrael
SHINYANGA: WATUMISHI KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MATUMIZI MABAYA YA MAMLAKA

- TAKUKURU itawafikisha Mahakamani Watumishi wa Halmashauri, Godfrey Mwagairo na Edward Maduhu

- Mwagairo atashtakiwa kwa Uhujumu Uchumi na Maduhu kwa kosa la jinai

Soma > https://jamii.app/WatumishiMahakamani
AINA MPYA YA KIRUSI CHA CORONA KUTOKA INDIA CHARIPOTIWA UGANDA

- Mbali na Kirusi hicho cha B.1.617, aina nyingine 4 zimethibitishwa Nchini humo

- Mamlaka zimesema Virusi vinavyosambaa zaidi #Uganda ni kutoka UK, Afrika Kusini na #India

Soma > https://jamii.app/IndianVariantUG
ZIMBABWE YALAUMIWA KWA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU TANGU KUWEPO KWA #COVID19

> #Zimbabwe imelaumiwa kukiuka haki za kimsingi za Binadamu ikiwemo kuwakamata Wanaharakati kwa kuandamana dhidi ya Serikali kushindwa kuwasaidia walioathiriwa

Soma - https://jamii.app/HakiZaBinadamuZimbabwe
CCM YAMCHAGUA SAMIA SULUHU KUWA MWENYEKITI WA CHAMA

- Ktk Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika Aprili 30 Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa Mgombea pekee wa nafasi hiyo ambapo amepata 100% ya kura

- Amechukua nafasi hiyo baada ya Hayati Dkt. John Magufuli

Soma https://jamii.app/SamiaMwenyekiti
LAZARO NYALANDU AREJEA CCM

> Lazaro Nyalandu amerejea CCM akitokea CHADEMA. Amerejea Aprili 30 katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika Dodoma

> Nyalandu aliwahi kuwa mtia nia wa kugombea Urais kupitia CHADEMA ktk Uchaguzi Mkuu

Soma https://jamii.app/NyalanduCCM
DKT. KIONGO: NI KOSA KURUSHIANA NYIMBO YA MSANII BILA IDHINI YAKE

- Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni amesema, "#Sheria ya Mtandao (Cyber Law) inakataza na inasema Mtu anaweza kulipa faini ya Milioni 5 au kifungo"

Soma > https://jamii.app/IdhiniKurushaNyimbo

#JFLeo #Sanaa
WADAU WALALAMIKIA UCHAFU WA SOKO LA MACHINJIO MWANZA

> Soko la Machinjio lililoko Kirejeshi Igoma - Nyamagana limelalamikiwa kuwa hatarishi kwa Afya ya watumiaji kutokana na uchafu

> Inadaiwa Wananchi wanalipa kodi za vibanda Tsh. 15,000 na vizimba Tsh. 6,000 kwa mwezi lakini eneo halijafanyiwa maboresho

Soma - https://jamii.app/SokoLaNdizi
DANIEL CHONGOLO APENDEKEZWA KUWA KATIBU MKUU CCM

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Ndg. Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho

> Kwa sasa, Chongolo ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar

Soma > https://jamii.app/ChongoloKatibuCCM
WAIRAN 7 WANAODAIWA KUSAFIRISHA HEROIN WAFIKISHWA MAHAKAMANI

- Wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha Heroin (Kilo 504.36) na Methamphetamine (Kilo 355)

- Wanakabiliwa na Kesi ya Uhujumu Uchumi

Soma > https://jamii.app/Wairan7Mahakama
#COVID19: VIFO BRAZIL VYAFIKIA 400,000. UUNGWAJI MKONO WA RAIS BOLSONARO WAPOROMOKA

- Bunge laanza uchunguzi kuhusu namna Serikali inavyoshughulikia mlipuko

- Mara nyingi Rais Jair Bolsonaro amekuwa akipinga Lockdown na ameendelea kukosolewa vikali

Soma https://jamii.app/BrazilVifo
KENYA: MAHUSIANO KATI YA MAAFISA WA POLISI KUPIGWA MARUFUKU

- Serikali inaandaa Kanuni zitakazozuia Polisi kuoana au kuwa na mahusiano na Polisi wenzao

- Hatua hiyo inalenga kupambana na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na mauaji

Soma > https://jamii.app/NdoaPolisiKE
JAMIIFORUMS INAKUTAKIA 'WEEKEND' NJEMA

> Tunawatakia Watembeleaji wa JamiiForums.com na wafuatiliaji wa kurasa zetu kwenye Mitandao ya Kijamii mwisho mwema wa Juma

> Tembelea JamiiForums.com na ujisajili kwa kubofya 'Register' na kisha fuata maelekezo

#JamiiForums #TGIF
KUPAMBANA NA #COVID19: MITAMBO YA OKSIJENI YASIMIKWA KUBORESHA HUDUMA

Serikali imesema uwekezaji huo utaweza kujibu changamoto kipindi cha mlipuko wa #COVID19

Imesimikwa Hospitali 7 za Rufaa na inalenga kuzalisha mitungi 200 ya Oxygen kwa saa 24

Soma - https://jamii.app/MitamboHewa
TANGA: WATU WAWILI WAUAWA NA TEMBO NDANI YA WIKI 1

> Tembo waliovamia makazi ya Watu ktk mtaa wa Malezi wapelekea Wananchi kuishi kwa hofu

> Aprili 30, 2021 asubuhi, Mtu wa pili aliuawa alipokuwa na wajukuu zake wakichimba mihogo ya futari

Soma - https://jamii.app/TemboHandeni
TUCTA: WAFANYAKAZI KUTOONGEZEWA MISHAHARA KUMEPUNGUZA ARI YA KAZI

- Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA asema Mishahara haijaongezwa kwa miaka 8 kwa Sekta isiyo rasmi na miaka 6 kwa Sekta ya Umma

- Asema "Gharama zimezidi kupanda, stahiki zimeendelea kuwa duni"

Soma https://jamii.app/MishaharaWafanyakazi
RAIS MWINYI: CORONA ILISABABISHA SHIDA HATA KWENYE ULIPAJI MISHAHARA

- Asema Wataalamu wakiwemo Walimu na Watumishi wa Afya wanastahili kufikishwa sehemu nzuri ya mishahara

- Amesema Uchumi ukiimarika Serikali ya Awamu ya 8 itaanza na kada ya kati

Soma https://jamii.app/MwinyiMishahara
SERIKALI YAPUNGUZA PAYE KWA 1%

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu ametangaza punguzo ya Kodi ya 'Lipa kadiri unavyovuna' (PAYE) kutoka 9% hadi 8% ili kuwapa unafuu watumishi

> Hii imetokana na ombi la Katibu Mkuu wa TUCTA kuomba kupunguziwa kodi hiyo kwenye mishahara

Soma > https://jamii.app/RaisMeiMosi
MAKATO YA HELSB KUBAKI 15%, β€˜VALUE RETENTION FEE’ YAONDOLEWA

- Rais Samia Suluhu ametangaza kuwa Makato ya Mikopo ya Elimu ya Juu yatabaki kuwa 15% huku akiondoa tozo ya kutunza thamani ya Fedha za Mkopo (6%) inayotozwa kwa mwaka katika deni lililosalia (Outstanding Loan Balance)

#JamiiForums