JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS SAMIA ATAJA COVID19 KUWA MOJA YA SABABU MISHAHARA KUTOPANDISHWA

> Rais Samia Suluhu amewapa pole Watumishi wa Umma kwa kuwa hawezi kuongeza mishahara kwa mwaka huu, labda mwaka ujao wa fedha

> Ametaja Corona kuwa kati ya sababu za kushindwa kuongeza mishahara

Soma https://jamii.app/RaisMeiMosi
TUCTA YAPENDEKEZA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA KIWE TSH. 970,000

> Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA amesema wamefanya tafiti kubaini kiwango cha mshahara ambacho kinaweza kumtosha mtumishi kuendesha maisha yake ni 970,000

Soma https://jamii.app/MinimumWage
#JamiiForums
AUSTRALIA YAPIGA MARUFUKU RAIA WANAOTOKEA INDIA KUREJEA NCHINI HUMO

- Ni sehemu ya Kanuni zinazolenga kuzuia wasafiri wakati India inapambana na #COVID19

- Ni mara ya kwanza kwa Australia kufanya kitendo cha Raia kurejea nyumbani kuwa kosa la jinai

Soma https://jamii.app/AusBanIndia
KOMBE LA SHIRIKISHO: SIMBA KUKABILIANA NA KAGERA SUGAR

- Klabu ya Simba ambayo ni bingwa mtetezi wa kombe itakutana na Kagera Sugar majira ya saa 1:00 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mchezo mwingine unaoendelea ni kati ya Dodoma Jiji dhidi ya KMC Fc

- Washindi wa #Michezo ya leo wataungana na Yanga na Mwadui ambazo zimetinga robo fainali ya michuano baada ya Yanga kuifunga Tz Prisons 1-0 na Mwadui kuiadhibu Coastal union goli 2-0

#JamiiForums #Sports
HUAWEI YAJIPANGA KUWA NA KASI YA 6G JULAI 2021

> Wakati Afrika inapambana na teknolojia ya 3G. Kampuni ya Teknolojia ya Huawei inajaribu kwa mara ya pili teknolojia ya 6G

> 6G inatarajiwa kuwa na kasi mara 100 ya kasi ya 5G

Soma https://jamii.app/Huawei6G
#JFTeknolojia
JE, FILAMU ZAKO PENDWA ZA KIVITA NI ZIPI?

> Ziko filamu nyingi za kivita zilizokonga nyoyo za watazamaji kiasi cha Watu kujivisha uhusika wa filamu. Mfano kufunga usongo kama Rambo ili kupigana

> Je, unazikumbuka filamu gani za kivita zilizokukosha?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/FilamuZaKivita
KOMBE LA SHIRIKISHO: SIMBA NA DODOMA JIJI ZATINGA ROBO FAINALI

- Michezo ya hatua 16 bora imemaliza kwa timu za Simba SC na Dodoma Jiji kusonga mbele katika hatua ya robo fainali

- Simba imeibuka kidedea kwa kuifunga Kagera Sugar goli 2-1 huku Dodoma Jiji ikiifunga KMC FC goli 2-0

- Simba na Dodoma Jiji zinaungana na Yanga SC na Mwadui FC katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo

#JamiiForums #JFSports
SOMALIA: BUNGE LAPIGA KURA KUMFUTIA RAIS NYONGEZA YA MUDA

- Ni baada ya hatua hiyo iliyoidhinishwa mwezi Aprili kuibua mvutano mkubwa

- Kuna wasiwasi waasi wa Al Shabaab wanaweza kutumia nafasi hiyo kuhatarisha hali ya usalama Nchini humo

Soma > https://jamii.app/BungeSomalia
WADAU WALALAMIKIA HALI YA STENDI YA KAGERA

> Mdau wa JamiiForums ameandika kuwa Stendi Kuu ya Mkoa wa Kagera haiko ktk hali nzuri mbali na kutumiwa na wageni wa nchi jirani

> Mdau amedai bajeti ya Wizara ya OR-TAMISEMI haijaongelea Stendi hiyo

Soma https://jamii.app/StendiKagera
SAMSUNG YAIPIKU APPLE KWENYE MAUZO YA SIMU ROBO YA KWANZA YA MWAKA

- Kampuni hiyo imeteka soko kwa 22%, ikiuza takriban simu Milioni 76.5 ikilinganishwa na Apple iliyouza simu Milioni 52.4 na kuambulia 15% tu ya soko kuanzia Januari hadi Machi 2021

Soma https://jamii.app/SamsungVsApple
MNYIKA: TULIJUA NYALANDU NA SELEMAN WANGEHAMA

> Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema walifahamu Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew wangeondoka kutokana na mienendo waliyokuwa wakiionesha kwa hivi karibuni

Soma https://jamii.app/MnyikaWasaliti
#JFLeo #JamiiForums
RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI KENYA

> Rais wa #Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku mbili nchini #Kenya

> Anatarajia kufanya ziara hiyo kuanzia Mei 4, 2021 ambapo atapokelewa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Soma https://jamii.app/ZiaraKenya
INTER MILAN YAWA BINGWA WA β€˜SERIE A’

- Inter chini ya Kocha Antonio Conte imekuwa Bingwa baada ya Sassuolo kutoka sare ya goli 1-1 na Atalanta iliyo nafasi ya 2

- Ushindi huu tangu ishinde taji hilo 2009/10 umemaliza utawala wa miaka 9 wa Juventus kushinda taji hilo

#JFSports
MECHI YA MANCHESTER UNITED DHIDI YA LIVERPOOL YAAHIRISHWA

- Ni baada ya mashabiki takriban 200 wa Man. Utd kuvamia Old Trafford kupinga Umiliki wa familia ya Glazer katika Klabu hiyo

- Man. Utd imesema EPL itapanga upya tarehe ya mchuano huo muhimu kwa Ligi Kuu

#JFSports
TUANZE WIKI KWA ARI YA KAZI

> Habari yako Mdau wa JamiiForums. Tunakutakia kila la kheri kwenye kazi zote njema utakazozifanya wiki hii

> Tunashukuru kwa kuwa nasi na kukusihi kuendelea kutufuatilia ili kupata taarifa na maarifa mbalimbali

#JFLeo
JUKUMU LA KULINDA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI SIO LA SERIKALI PEKEE

> Mei 3 ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari na Maadhimisho yanafanyika Jijini Arusha

> Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, asisitiza kuweka maslahi ya Taifa mbele

Soma - https://jamii.app/FreePress
#MediaRights
NIGERIA YAPIGA MARUFUKU WASAFIRI KUTOKA INDIA, BRAZIL NA UTURUKI

- Watu wenye Hati za Kusafiria zisizo za Nigeria na waliozuru Mataifa yaliotajwa siku 14 kabla ya kwenda #Nigeria, watanyimwa ruhusa ya kuingia kuanzia Mei 4 kutokana na #COVID19

Soma - https://jamii.app/NigeriaBanIndia
WAZIRI UMMY: NI MARUFUKU SHULE KUWADAI CHETI WANAOANZA DARASA LA KWANZA

- Amesema "Bado hatujafanya vizuri ktk kuongeza 'access' ya Watoto kuanza Elimu ya Awali. Haileti mantiki kusema kila Mtoto aanze Darasa la 1 akiwa na Certificate ya Awali"

Soma > https://jamii.app/ShuleCheti1
LSF: KUPATA TAARIFA NI HAKI YA MSINGI YA KILA MTU

- Mkurugenzi wa Shirika la Legal Services Facility (LSF) Lulu Ng’wanakilala amesema ili kuwa na Jamii yenye maendeleo nyanja zote ni muhimu kuwa na taarifa sahihi zitakazowawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi

- Amesema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari ambayo kilele chake kinafanyika Arusha

- Ameeleza, "Tunapoadhimisha Siku hii ya #UhuruWaHabari napenda kusisitiza kuwa kupata taarifa ni Haki ya msingi ya kila mtu"

Soma > https://jamii.app/PressFreedomDay

#WPFD #WorldPressFreedomDay #AccessToInformation