JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBUNGE: KUNA MRUNDIKANO MAGEREZANI KWASABABU YA KESI ZA KUBAMBIKIWA

- Agnesta Kaiza amesema "Kila leo unasikia fulani ana kesi ya Uhujumu Uchumi"

- Asema uwepo wa masharti magumu ya dhamana ni sababu nyingine ya mrundikano ktk Magereza na Mahabusu

Soma - https://jamii.app/MbungeMagereza
AUSTRALIA: JELA MIEZI 10 KWA KUWAPIGA PICHA POLISI WALIOKUWA WANAKATA ROHO

- Richard Pusey (42) amekutwa na hatia kwa kuwadhihaki na kuwapiga picha Maafisa wa Polisi waliofariki ajalini

- Familia za Marehemu hazijaridhishwa na kifungo kilichotolewa

Soma https://jamii.app/PolisiWakikataRoho
MORRIS NYUNYUSA MLEMAVU WA MACHO ALIYEKUWA NA KIPAJI CHA KUPIGA NGOMA

- Yeye ndiye aliyepiga ngoma zinazosikika kupitia TBC Taifa kama kiashiria cha kuanza kwa taarifa ya habari

- Inaelezwa kuwa Mzee Nyunyusa hakunufaika na kazi zake hata nyumba yake iliponea chupuchupu kuuzwa kwa deni la mkopo wa benki

- Ingawa Morris Nyunyusa ameshafariki lakini kazi zake ni tunu ya Taifa kwenye sanaa

Soma https://jamii.app/HistoriaNyunyusa

#JamiiForums #JamiiTalks #Historia
UGANDA YASITISHA MATUMIZI YA VITAMIN C KATIKA KUTIBU COVID19

- Vidonge vya Vitamin C vinapatikana kirahisi hivyo Watu hutumia kiholela na kuleta madhara ikiwemo Figo kutofanya kazi

- Vitamin C husaidia chembe hai nyeupe kupambana na virusi

Soma - https://jamii.app/UgandaVitaminC
DRC: UMOJA WA MATAIFA WACHUKUA DOZI MILIONI 1.3 ZA COVID19 ILI ZISIISHE MUDA WA MATUMIZI

> Chanjo ya #Astrazeneca iliyopokelewa DRC itaisha muda wa matumizi Juni 24

> UNICEF imechukua dozi hiyo ili kuzipeleka #Senegal, Comoros, #Ghana na Angola

Soma - https://jamii.app/DRCChanjoUN
MOROGORO: MBARONI KWA KUUZA MISHKAKI YA NYAMA YA MBWA

> Hamza Rajabu (20), Omary Mohamed (12) na Mussa Juma (30) wanashikiliwa na Polisi kwa kuuza mishkaki ya Mbwa maeneo ya Msamvu

> Walikutwa wakimchuna ngozi Mbwa Darajani ktk barabara ya Iringa

Soma - https://jamii.app/MbwaMoro
WALIOSTAAFU 1996 OFISI YA MAKAMU WA RAIS HAWATALIPWA PENSHENI

> Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imesema waliostaafishwa walishalipwa stahiki zao

> Hawatalipwa pensheni kwani waliajiriwa kwa β€œOperational Services”

Soma - https://jamii.app/SerikaliPensheni
MBUNGE ASEMA SHERIA YA BIMA INA MATATIZO NA WANANCHI HAWATENDEWI HAKI

- Dkt. Oscar Kikoyo amesema mhanga wa ajali za barabarani anapokwenda kudai fidia, Sheria ya Bima ipo kimya

- Ameeleza, kiasi anachoenda kulipwa ni maamuzi ya Kampuni ya Bima

Soma > https://jamii.app/BungeSheriaBima
#COVID19: KENYA YAZUIA NDEGE KUTOKA INDIA

- Zuio hilo la siku 14 ni kufuatia ongezeko la maambukizi Nchini India

- Wataowasili #Kenya kutoka India katika saa 72 zijazo watafanyiwa vipimo na watakaokutwa na maambukizi watalazimika kujitenga siku 14

Soma https://jamii.app/KenyaNdegeIndia
KENYA: KITUO CHA RUNINGA CHAFUNGIWA KWA KUONESHA VIBONZO VYA NGONO

> Mt. Kenya TV kimefungiwa kwa wiki nne na kutakiwa kulipa faini ya takriban Tsh. Milioni 11.5

> Mamlaka ya Mawasiliano zimesema kituo hicho kilirusha picha zisizofaa mchana

Soma https://jamii.app/KituoChaRuninga
TSH. BILIONI 35.7 ZIMEKUSANYWA BAADA YA WASHTAKIWA KUKIRI MAKOSA

> Waziri Kabudi amesema Washtakiwa 243 ktk kesi 192 za Uhujumu Uchumi, wamekiri makosa na kulipa fidia/faini ya Tsh. Bilioni 35.7 ktk kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021

Soma https://jamii.app/KukiriUhujumu
WIZARA: TUPO TAYARI KUBADILI SERA NA SHERIA IKIWA WADAU WATAPENDEKEZA

> Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbas amesema Wadau wakupendekeza mambo yenye tija ktk Tasnia, Serikali itabadili Sheria ya Habari

Soma https://jamii.app/MabadilikoHabari
BIDEN: MAREKANI HAINA LENGO LA KUVUTANA NA URUSI

- Rais huyo amesema alimweleza wazi Rais Vladimir Putin kuwa hawalengi kuchochea mvutano lakini vitendo vinavyofanywa na Urusi vina athari

- Asema Marekani haitoacha kujitolea kwenye Haki za Binadamu

Soma https://jamii.app/BidenUSRussia
UNITAID: BEI YA VIFAA VYA KUJIPIMA VVU YASHUKA KWA 50%

- Vifaa hivyo sasa vitauzwa kwa Dola 2 (Takriban Tsh. 4,500) ktk Nchi zinazokidhi vigezo

- Kifaa hicho ni muhimu kwa Nchi za kipato cha chini na kati, ambako kuna changamoto za huduma za afya

Soma - https://jamii.app/VifaaVVU
RUVUMA: TEMBO 30 WAVAMIA MASHAMBA NA KUHARIBU EKARI 20

> DC wa Namtumbo amesema Tembo huvamia kutokana na Wafugaji na Wakulima kuharibu Ikolojia ya Hifadhi

> Mbali na kuharibiwa mazao, Wananchi wanaokota kinyesi cha Tembo wakidai ni dawa

Soma - https://jamii.app/TemboNamtumbo
NAIBU WAZIRI: KIPANDE CHA JANGWANI KINAFANYIWA USAFI KUPUNGUZA ATHARI ZA MAFURIKO

- Asema Serikali imepanga kubadili eneo la Bonde la Mto Msimbazi kuwa la Uwekezaji na usanifu wa mradi umekamilika

- Utekelezaji utaanza baada ya kupata idhini

Soma https://jamii.app/ChandeBungeni