JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DKT. MPANGO: SITAKUWA MPOLE KWA WANAOCHEZEA MUUNGANO

- Amesema katika kipindi chake kama Makamu wa Rais hatokubali Muungano kuchezewa

- Asema, "Kuna baadhi ya mambo huwa watu wanasema mimi mpole. Watakaojaribu kuchezea Muungano hapo sitakuwa mpole"

Soma https://jamii.app/MpangoMuungano
HALI YA USALAMA YAPELEKEA TOTAL KUSITISHA SHUGHULI MSUMBIJI

- Kampuni hiyo imesitisha shughuli za kuchunguza eneo kubwa la gesi Kaskazini mwa Msumbiji wiki kadhaa tangu Mji jirani kushambuliwa

- Total imesema itaondoa Wafanyakazi wake wote

Soma > https://jamii.app/MsumbijiTotal
EPUKA MAVAZI YAFUATAYO UNAPOENDA KWENYE USAHILI (JOB NTERVIEW)

- Nguo zenye rangi ya kung'aa na urembo mwingi. Mapambo mengi kama, hereni, bangili, pete n.k

Soma> https://jamii.app/MavaziYasiyofaa

#JFAjira #lifestyle #JamiiTalks
MAVAZI YANAYOFAA KUVAA WAKATI WA USAHILI 'INTERVIEW'

Vaa aina ya mavazi yanayokuonesha kuwa ni nadhifu na uko makini 'professional'

Soma> https://jamii.app/MavaziYanayofaa

#JFajira #lifestyle #JamiiTalks
MALAYSIA: #ASTRAZENECA KUTOLEWA KWA WENYE MIAKA 60 NA ZAIDI

- Mamlaka zasema Chanjo hiyo ni salama kutumika. Maafisa wanapitia taarifa kabla haijaidhinisha kwa Vijana

- Nchi kadhaa zimesitisha au kudhibiti utoaji kutokana na ripoti za ugandaji damu

Soma https://jamii.app/AstraZMalaysia
RAIS SAMIA ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 5,001

> Wafungwa 1,516 wameachiwa huru, 3,495 wanatumikia sehemu iliyobaki baada ya kusamehewa robo ya vifungo vyao

> Awataka walioachiwa huru kutumia mafunzo waliyoyapata wakiwa gerezani na wazingatie Sheria

Soma https://jamii.app/RaisSamiaMsamaha
WAZIRI AWESO: WASOMA MITA WASIPEWE MALENGO AMBAYO HAYATEKELEZEKI

- Serikali imetaka wasoma mita za Maji kutopewa malengo makubwa ya makusanyo yasiyo na uhalisia, ambayo yanaumiza Wananchi na kusababisha malalamiko

Soma > https://jamii.app/WaziriMitaMaji
IVORY COAST: WAKAGUZI WOTE WA MAJARIBIO YA UDEREVA WASIMAMISHWA KAZI

- Serikali imewasimamisha Wakaguzi ikisema inasafisha sekta. Zoezi litasimamiwa na Polisi

- Udanganyifu, ufisadi na ongezeko la ajali barabarani ni sababu za uamuzi huo

Soma > https://jamii.app/DrivingTestStaff
JINA TANZANIA LILIPATIKANA KUPITIA SHINDANO LA MAJINA

> Baada ya Muungano wa Tanganyika na #Zanzibar, lilitangazwa shindano la kubuni jina la pamoja

- Watu 80 walishiriki na Mohammed Iqbal Dar, Mwanafunzi wa Mzumbe alibuni jina #Tanzania

Soma - https://jamii.app/TanzaniaJina
#MYANMAR: WANAHARAKATI WAITISHA MGOMO KWENYE HUDUMA ZA JAMII

> Wanaharakati wanaopinga Utawala wa Kijeshi wamewataka watu kuacha kulipa Bili za Umeme na Mikopo ya Kilimo, na kutowapeleka watoto shuleni ili kuuwekea mgomo Utawala huo

Soma https://jamii.app/MgomoMyanmar
MAREKANI KUGAWA DOZI MILIONI 60 ZA ASTRAZENECA NA NCHI NYINGINE

- Taifa hilo limekuwa na akiba ya Chanjo hiyo japo Mamlaka hazijatoa idhini ya kutumika

- Wakosoaji wamekuwa wakiishutumu Marekani kuhodhi Chanjo wakati Nchi nyingine zina uhitaji

Soma > https://jamii.app/AstraZenecaUS
ARUSHA: BAADHI YA MALI ZA NGURDOTO MOUNTAIN LODGE ZAUZWA KULIPA MADAI YA MISHAHARA

> Watu 93 waliokuwa Wafanyakazi walifungua kesi wakidai Tsh. Milioni 129 za malimbikizo ya mishahara

> Mahakama itatoa amri Mei 4, 2021 kuhusu mali hizo

Soma https://jamii.app/HoteliArusha
INDIA YAREKODI MAAMBUKIZI MAPYA 300,000 KWA SIKU 6 MFULULIZO

- Ndani ya saa 24 zilizopita, visa 323,144 vya #COVID19 vimerekodiwa na maambukizi yamefikia Milioni 17.64

- Vifo 2771 vimerekodiwa lakini Wataalamu wanaamini idadi halisi ni kubwa zaidi

Soma https://jamii.app/VisaCOVIDIndia
KIKWETE: SITARAJII KOFIA YA UENYEKITI WA CHAMA KUTOFAUTISHWA NA URAIS

> Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, amesema Rais wa #Tanzania huwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ili kuepuka migongano ambayo inaweza kujitokeza ikiwa Mwenyekiti na Rais watatofautiana

Soma - https://jamii.app/UenyekitiCCM
#NIGERIA: WANAMGAMBO WAVAMIA KAMBI NA KUUA WANAJESHI 33

> Wanajeshi wa kambi ya #Mainok ktk Jimbo la Borno wameuawa na wapiganaji wa Dola ya Kiislamu (IS)

> Wapiganaji walifika kambini hapo na nguo za Jeshi na Magari 16 na kuiteka kambi

Soma - https://jamii.app/NigeriaIS
LIGI KUU KUENDELEA KUTIMUA VUMBI LEO

- Baada ya kushinda michezo 4 mfululizo, Simba leo inashuka dimbani kukipiga dhidi ya Dodoma Jiji majira ya saa 1:00 usiku

- Mchezo mwingine utakaopigwa leo ni kati ya Gwambina dhidi ya Mwadui majira ya saa 10:00 jioni

#JamiiForums #Sports
CCM-DODOMA: KATIBA ILIYOPO INAFAA, HAKUNA ULAZIMA WA KUICHOKONOA

- Halmashauri Kuu ya CCM Dodoma imesema #Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 bado inafaa

- Imesema Katiba imewezesha kufanyika mabadiliko ya Uongozi wa juu bila mgogoro

Soma https://jamii.app/CCMKatibaMpya
JULIAN NAGELSMANN KUWA KOCHA WA BAYERN MUNICH

- Bayern imemtangaza Nagelsmann (33) kuwa Kocha wao kuanzia Julai 1, 2021 baada ya kuilipa Leipzig £ milioni 21.7

- Kocha huyo wa Leipzig ana uwiano wa ushindi wa 58% akiwa na timu hiyo kwa miaka 2, ameshinda mechi 53/90

#JFLeo
MAENEO YA KAMBI KUREJESHWA SERIKALINI BAADA YA WAKIMBIZI KUONDOKA

- Naibu Waziri Mambo ya Ndani amesema maeneo yote ya kambi yatarejeshwa Serikalini ili yapangiwe matumizi

- Pia hakuna mgogoro wa Ardhi baina ya Kambi ya Nyarugusu na Kata ya Makere

Soma https://jamii.app/KambiWakimbizi