JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KIMBUNGA JOBO KIMERUDI KWENYE KASI YA AWALI

> Kimbunga JOBO kimekadiriwa kuwa umbali wa kilometa 76 kutoka Kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani huku kikisafiri kwa kasi ya 20Km/h

> TMA imesema kasi ya 20km/h ni kasi kubwa

Soma https://jamii.app/KimbungaJoboDhaifu
KILWA: ZAIDI YA TANI MOJA YA HEROIN YAKAMATWA

> Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na #DawaZaKulevya imekamata zaidi ya tani moja ya dawa za kulevya aina ya Heroin eneo la Kilwa Masoko zikisafirishwa kwa kutumia Jahazi

Soma https://jamii.app/DawaHeroinKilwa
TMA: KIMBUNGA JOBO HAKIPO

> Kimbunga JOBO kimepungua nguvu kadiri kilivyokuwa kinakaribia nchi kavu na hakutakuwa na madhara ya moja kwa moja yaliyotarajiwa

> Wananchi wameshauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka TMA

Soma https://jamii.app/KimbungaJoboDhaifu
KENYA: WENYE VVU WALALAMIKIA UHABA WA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI

- Uhaba wa Dawa umesababishwa na mzozo kati ya Serikali na USAID kutokana na kuongeza ushuru wa misaada

- Pia, USAID inatilia shaka madai ya rushwa dhidi ya Mamlaka ya Vifaa Tiba

Soma https://jamii.app/ARVsLackKE
MKURUGENZI WA TEMEKE ASIMAMISHWA KAZI KWA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA

> Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Ummy Mwalimu amemsimamisha Lusubilo J. Mwakibibi baada ya malalamiko

> Pia, DED wa Sumbawanga amesimamishwa kwa usimamizi mbovu wa Miradi

Soma https://jamii.app/MkurugenziTMK
ATHARI ZA MAAMBUKIZI YA MALARIA

- Matatizo ya kupumua
- Matatizo ya Ini
- Mshtuko wa Moyo
- Figo kushindwa kufanya kazi
- Kuvimba na kupasuka kwa bandama
- Kupungukiwa na maji mwilini

#InternationalMalariaDay #Malaria #JamiiAfya #JFLeo #WorldMalariaDay
WAKILI WA SERIKALI MWANDAMIZI MBARONI KWA RUSHWA YA TSH. MILIONI 5

> TAKUKURU Mkoa wa Manyara inamshikilia Mwendesha Mashtaka wa Serikali mkoani humo, Mutalemwa Kishenyi kwa kupokea rushwa ya Tsh. Milioni 5 kutoka kwa watuhumiwa

Soma zaidi - https://jamii.app/KishenyiArrested
VPL: JE, YANGA KUREJEA KILELENI LEO?

> Baada ya kushushwa katika nafasi ya kwanza na Simba SC kuchukua nafasi hiyo, Yanga leo inashuka dimbani kumenyana na Azam FC majira ya saa 2:15 usiku

> Yanga ikishinda mchezo huo itafikisha alama 60 na itafanikiwa kupanda katika nafasi ya kwanza kwa mara nyingine huku ikiwa mbele kwa michezo 3 dhidi ya Simba yenye alama 58

#JamiiForums #JFSports
#IRAQ: 82 WAFARIKI BAADA YA MITUNGI YA OKSIJENI KULIPUKA KATIKA HOSPITALI INAYOHUDUMIA WAGONJWA WA COVID19

> Aidha, watu wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa Aprili 24 ktk Hospitali ya IBN Khatib

> Waziri wa Afya amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Soma https://jamii.app/Iraq82Wafariki
CHANJO YA MALARIA YENYE UWEZO MKUBWA ZAIDI YAGUNDULIKA

- Timu ya Chuo Kikuu cha Oxford iliyohusika kutengeneza chanjo ya Oxford-AstraZeneca Covid-19 imetengeneza chanjo dhidi ya malaria inayofikia kiwango cha juu cha ufanisi kwa 75% ya Shirika la Afya Ulimwenguni. Chanjo hiyo imepewa jina la R21

- Chanjo ya kwanza kugundulika ni RTS mwaka 2015 ambayo Ufanisi wake ilikuwa 29.9% kwa kipindi cha kwanza cha majaribio ya kliniki na 57.7% kwa malaria kali.

- Kulingana na matokeo ya awali kutoka kwa jaribio la kliniki lililochapishwa Aprili 22, 2021 imeonesha R21 ni mafanikio makubwa dhidi ya vita ya malaria, ambayo ni chanzo kikubwa cha vifo duniani.

#ChanjoMalaria #InternationalMalariaDay #JamiiTalks
VPL: YANGA YASHINDWA KURUDI NAFASI YA KWANZA

Mchezo kati ya Yanga SC dhidi ya Azam FC umemaliza kwa ushindi wa Azam wa goli 1-0, lililofungwa na P. Dube 86'

> Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kusalia katika nafasi ya 2 ikiwa na alama 57

#JamiiForums #JFSports
TUNAWATAKIA MAADHIMISHO MEMA YA SIKU YA MUUNGANO

> Uongozi na Watendaji wa Jamii Forums unawatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya Siku ya Muungano

> Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kutengeneza Tanzania tarehe 26/4/1964

#Jamiiforums
CHAD: JESHI LAKATAA MAZUNGUMZO NA WAASI

- Msemaji wa Baraza la Jeshi linaloongoza Nchi hiyo kufuatia kifo cha Rais Deby asema sio muda wa upatanishi

- Jeshi linashinikizwa kukabidhi madaraka kwa Serikali ya Mpito ya raia haraka iwezekanavyo

Soma https://jamii.app/ChadArmyRebels
👍1
ARUSHA: POLISI ADAIWA KUMPIGA RISASI MUME WA MCHEPUKO

> Yohana Nasieli alipigana na Mkewe akimtuhumu kutoka nje ya Ndoa na Polisi ambapo Mke aliamua kumshtaki

> Askari walikwenda kwa Yohana ambapo alipomuona mbaya wake alichukua panga kuwakabili

Soma - https://jamii.app/PolisiAuaArusha
FEDHA ZA SHEREHE ZA MUUNGANO KUGAWANYWA BARA NA ZANZIBAR

- Rais Samia ameelekeza fedha kugawanywa na kila upande kuamua namna ya kuzitumia kwa shughuli za maendeleo

- Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais Dodoma ktk Kongamano la Miaka 57 ya Muungano

Soma https://jamii.app/FedhaShereheMuungano
INDIA KUPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUPAMBANA NA COVID19 KUTOKA MATAIFA YA ULAYA

> Idadi ya maambukizi na vifo vinavyotokana na #COVID19 nchini #India imeongezeka kwa kasi

> Wamesaidiwa vifaa 600 ikiwemo Oksijeni na Ventilators

Soma https://jamii.app/MsaadaIndia
DKT. MPANGO: CHANGAMOTO HAZIMAANISHI MUUNGANO SIO IMARA

- Asema Serikali zimekuwa zikibaini changamoto na kufanya jitihada kuzipatia ufumbuzi

- Ameeleza, "Serikali kwa pamoja zimefanikiwa kutatua changamoto 15 zilizokuwa zinaukabili Muungano wetu"

Soma https://jamii.app/VPMpangoDodoma