JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI KUWASILISHA MUSWADA WA KUREKEBISHA KIKOKOTOO CHA MAFAO

- Serikali itawasilisha Bungeni Muswada wa marekebisho ya #Sheria ya mafao ya Wafanyakazi kuhusu kikokotoo kipya ili kuondoa vikwazo kwa Wafanyakazi kuchukua fedha wanapostaafu

Soma - https://jamii.app/MuswadaMafao
ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TPA AACHIWA KWA DHAMANA

- TAKUKURU imesema Deusdedit Kakoko ameachiwa kwa dhamana na Taasisi hiyo imekamilisha uchunguzi kwa 98%

- Alishikiliwa kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Bilioni 3 ndani ya Mamlaka ya Bandari

Soma https://jamii.app/KakokoDhamana
SHINYANGA: BABU ATUHUMIWA KUBAKA MJUKUU WA MIAKA 7

- Jeshi la Polisi linamshikilia Juma Emmanuel (53) kwa kumbaka Mjukuu wake wakati Bibi wa Mtoto akiwa amelazwa Hospitalini

- Wananchi watakiwa kutoa taarifa kuhusu Ukatili dhidi ya Watoto

Soma - https://jamii.app/KubakaMjukuuSHY
TAKWIMU: KUNA ONGEZEKO LA WATOTO KUACHA SHULE. WAVULANA WAONGOZA

- Wavulana 96,683 waliacha Shule mwaka 2020 na Wasichana 71,151. Mwaka 2017 ilikuwa Wavulana 36,434 na Wasichana 29,708

- Wanafunzi 167,834 waliacha Shule kutokana na utoro

Soma - https://jamii.app/WanaoachaShule
MAREKANI YAAMURU WANADIPLOMASIA WAKE KUONDOKA CHAD

- Ni kutokana na hofu ya kutokea mashambulio katika Mji Mkuu wa N’Djamena

- Marekani imetoa kauli hiyo wakati vikundi vyenye silaha vikionekana kujiimarisha kuingia katika Mji huo

Soma > https://jamii.app/USDiplomatsChad
PERU: KASHFA YA CHANJO YAPELEKEA RAIS WA ZAMANI KUPIGWA MARUFUKU KWA MIAKA 10

- MartΓ­n Vizcarra amepigwa marufuku kushika wadhifa kwenye Ofisi ya Umma kwa muda wa miaka 10 kufuatia madai kuwa aliruka foleni kupokea Chanjo ya #COVID19

Soma > https://jamii.app/VizcarraPeru
MIKATABA YA VIJANA 854 WA JKT WALIOGOMA NA KUANDAMANA YASITISHWA

- Vijana hao wa kujitolea walifanya hivyo kushinikiza kuandikishwa Jeshini

- Jenerali Venance Mabeyo amesema, "Kitendo hiki hakikubaliki, kugoma au kuandamana Jeshini ni kosa la uasi"

Soma > https://jamii.app/VijanaMikatabaJKT
RAIS SAMIA ASHIRIKI KONGAMANO LA KUMUENZI MAGUFULI

- Rais Samia Suluhu na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, leo wameshiriki Kongamano lililoandaliwa na Viongozi wa dini Chimwaga, kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa maisha ya Hayati Magufuli

Angalia - https://youtu.be/e4bSqKFNb3M
ASKOFU KONKI: KUMSIFIA RAIS SAMIA NA KUMKASHIFU DKT. MAGUFULI NI KUJIPENDEKEZA

- Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania, Peter Konki, amesema, "Watu hawa wanafanya hivyo kwa kutugawa Watanzania, tunaanza kushambuliana. Hayati Magufuli ni kipenzi cha Watanzania wengi kwahivyo wanasiasa msitugawanye"

Msikilize https://youtu.be/e4bSqKFNb3M
RAIS SAMIA: KUNA MIJADALA BUNGENI HAINA AFYA KWA TAIFA

- Amesema kipindi hiki wabunge wanapaswa kupitisha bajeti kwa maendeleo

- Asema "Jikiteni huko mengine tutayazungumza siku zinavyokwenda. Tufanye kazi kama Bunge linavyotakiwa kufanya kazi"

Tazama > https://youtu.be/FB7b1J8Dcuw
Rais Samia: Kamati ya kuchunguza #CoronaVirus imeshaundwa na hivi karibuni nitakaa nayo kujua namna tunavyokwenda

> Niwaombe viongozi wa dini, muwaombe waumini wenu wafuate hatua zote za kujikinga na #COVID19 kama kunawa mikono n.k
MAREKANI: WANAOJITOKEZA KUPATA CHANJO YA CORONA WAPUNGUA

> Mamlaka za #Marekani zimesema wanaojitokeza kupata Chanjo ya #COVID19 wamepungua sababu ikitajwa kuwa wengi wanasubiri kuona madhara ya chanjo hizo kwa ambao wameshapata

Soma https://jamii.app/ChanjoMarekani
TABORA: JELA MIAKA 21 KWA KUVUNJA NYUMBA NA KUIBA

> Hamisi Jilala Kwabi na Mohamedi Kassim wamehukumiwa kutumikia kifungo baada ya kukiri makosa 3 ya kuvunja na kuiba

> Ktk tukio mojawapo waliiba televisheni yenye thamani ya Tsh 1,100,000

Soma - https://jamii.app/JelaWizi
JE, NI SAHIHI KUFURAHIA MAHUSIANO YA VIJANA WADOGO?

> Mdau ameandika wazazi wengi hufurahia watoto wa kiume wakijihusisha na mapenzi wakiwa hata Shule ya Msingi na huonekana ni kawaida wakati huo huo wakichukizwa hali hiyo inapokuwa kwa watoto wao wa kike

> Je, ni kweli wazazi wako hivyo. Je unadhani ni sahihi?

Soma https://jamii.app/MaleziMahusiao
MSONGO WA MAWAZO (STRESS) NA DALILI ZAKE

- Dalili zinaweza kuanza kwa kujihisi mgonjwa, maumivu ya misuli, kuumwa kichwa na kushindwa kutuliza akili. Iwapo upo kwenye Ndoa, unaweza kukosa kabisa hamu na mwenzako

- Kuwa na hasira bila sababu ya msingi, huzuni kila wakati, kuchoka bila hata kufanya kazi, hamu ya kula kuongezeka kwa kiasi kikubwa ama kutoweka kabisa

Soma - https://jamii.app/MawazoHuzuni
#StressAwarenessMonth
#UJERUMANI: MAKUBALIANO YA MRITHI WA KANSELA MERKEL YAKWAMA

- Vyama vya CDU na CSU vimeshindwa kufikia makubaliano ya atakayechukua nafasi ya Kansela Angela Merkel

- Wajumbe wenye nguvu wanawashinikiza Wagombea wakuu kumaliza tofauti zao

Soma - https://jamii.app/MkwamoMrithiMarkel
UFUGAJI: SABABU ZA KUKU KUPUNGUZA UTAGAJI WA MAYAI (1)

- Kupungua kwa saa za mwanga: Mwanga husisimua β€œpituitary gland” kwa Kuku ili kuchochea uzalishaji wa Mayai. Mtiririko mzuri wa utagaji wa Mayai huhitaji saa 14 mpaka 16 za mwanga (Jua)

- Msongo wa Mawazo (Stress) na mabadiliko mbalimbali: Ni rahisi kwa Kuku kuathirika na #Stress kwasababu hapendi mabadiliko ikiwemo chakula, mpangilio wa vyombo vya chakula na maji na kuwahamisha hamisha kila mara

Soma - https://jamii.app/MayaiKukuChini
#JFUfugaji
RAIS SAMIA KULIHUTUBIA BUNGE APRILI 22, 2021

- Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kulihutubia Bunge la #Tanzania kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi jioni

- Spika Job Ndugai awataka Wabunge wote kuhakikisha wanakuwepo Bungeni wakati huo

Soma - https://jamii.app/SamiaBungeni
MICHEZO: JOSE MOURINHO ATIMULIWA TOTTENHAM HOTSPURS

- Imeripotiwa kuwa Chriss Powell na Ryan Mason wanajiandaa kuifundisha timu hiyo hadi mwisho wa mwezi Juni

- Bodi ya Timu hiyo imeanza mpango wa kupata kocha mpya

Soma > https://jamii.app/MourinhoOut

#Spurs #JamiiForums
JE, NINI KIFANYIKE KUWA NA MIPANGO MIJI MIZURI?

> Mdau wa #JamiiForums anasema hata maeneo mapya katika Miji hujengwa kiholela na kuwa changamoto

> Mbali na kazi nzuri inayofanywa na Wizara, Mdau anahoji njia nzuri za kuwa na Miji iliyopangika

Soma - https://jamii.app/MipangoMiji