JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WAFAMASIA WAKUMBUSHWA KUHUISHA LESENI ZAO KABLA YA DESEMBA 31

> Baraza la Famasi linawakumbusha Wafamasia, Fundi Dawa sanifu kuhuisha leseni kwa mujibu wa #Sheria ya Famasi

> Pia, kuhakikisha Dawa zinatolewa kwa kuzingatia miongozo iliyopo

Tazama https://youtu.be/nIo6vtAENgw
#JFLeo
#ZANZIBAR: RAIS MWINYI AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA ZSSF

- Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Sabra Issa Machano na Watendaji wengine wanatuhumiwa kuhusika na makosa mbalimbali katika utekelezaji wa miradi ya Serikali

Soma - https://jamii.app/MwinyiZSSF
#JFLeo
SHINYANGA: ABIRIA WALIOMPIGA DEREVA WA LORI WAKAMATWA

> Mwita C. Chaguche, Dereva wa Basi la Frester na abiria 3 wamekamatwa na Polisi kwa kumpiga Emmanuel Msuya wakimtuhumu kutaka kusababisha ajali eneo la Samuye barabara ya Shinyanga – Mwanza

Tazama - https://youtu.be/4d_aIDxXyzU
ZAIDI YA WATU 100 WAUAWA KWENYE SHAMBULIO #ETHIOPIA

- Shambulio hilo limetokea Mkoa wa Benishangul-Gumuz, siku moja baada ya Waziri Mkuu, Abiy Ahmed kutembelea

- Zaidi ya watu 30 waliojeruhiwa wamelazwa, huku baadhi wakiwa na hali mbaya

Soma - https://jamii.app/100KilledET
RAIS MAGUFULI ASHUKU USIRI WA KURUDISHA FOMU ZA MAADILI KWA NJIA YA MTANDAO

> Amesema, Mtu akirudisha fomu kwa njia ya Mtandao na akawepo anayejua β€˜passwords’ anaweza kuangalia na kujua siri za Mhusika au kuharibu kwa kuwa wadukuzi wako wengi

Soma https://jamii.app/DodomaUapishoMaadili
MANYARA: MWENYEKITI WA MTAA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA

- TAKUKURU imesema, Mathias Zebedayo alichukua kiwanja bila kufuata taratibu

- Alipohojiwa na Msimamizi wa Kiwanja, alidai kimetwaliwa na Halmashauri, hivyo atoe 100,000 amsaidie kurejesha

Soma https://jamii.app/MkitiRushwa
AINA MPYA YA VIRUSI VYA CORONA YAGUNDULIWA #NIGERIA

- Mkuu wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) Afrika, John Nkengasong amesema, Virus hivi ni tofauti na vilivyogundulika Uingereza na Afrika Kusini

- Sampuli hizi mpya zinachunguzwa

Soma https://jamii.app/CovidNGR
ARUSHA: WASHUKIWA WAWILI WA UJAMBAZI WAUAWA

> Joseph Bernard (24) na mwingine ambaye hajafahamika wameuawa baada ya kufanya majibizano ya risasi na Polisi

> Wanatuhumiwa kupanga njama za kupora duka, ambapo mmoja wao alikamatwa na kuwafichua

Soma https://jamii.app/Majambazi2Arusha
MICHEZO: PSG YAMFUKUZA KAZI KOCHA WAKE

- Klabu ya Paris Saint Germain imemfuta kazi Kocha Thomas Tuchel (47) kwasababu ya kutoridhishwa na matokeo ya hivi karibuni

- PSG inashika nafasi ya tatu katika Msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 35

#JamiiForums #JFMichezo #Sports
WASHTAKIWA WANNE WA MAUAJI YA 2015 YA ALPHONCE MAWAZO WAHUKUMIWA KIFO

- Washtakiwa wanne katika Kesi ya mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo wamepewa Hukumu ya kifo kwa kosa la kuua kwa kukusudia

Soma - https://jamii.app/4HukumuKifo
RAIS MAGUFULI: KWENDA NYUMBANI SIO DHAMBI

> Rais Magufuli ameruhusu Watumishi wa Serikali kwenda nyumbani kipindi hichi cha sherehe za mwisho wa mwaka

> Wakurugenzi waliozuiwa na Waziri Mkuu hawatakuwa na ruhusa ya kuondoka

Soma https://jamii.app/DodomaUapishoMaadili
SERENGETI: MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMUUA KAKA YAKE KWA DENI LA TSH. 700,000

> Juma Masiaga (38) anatuhumiwa kumchinja kaka yake, Chacha (40) kwa madai ya kutomlipa Tsh. 700,000

> Mtuhumiwa alikimbia, amekamatwa leo na anaendelea na mahojiano

Soma https://jamii.app/AuaKakaYake
ETHIOPIA: WATU 42 WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA WATU 100 WAUAWA

> Watu 42 wanaoshukiwa kufanya mauaji ya watu 100 kwenye Jimbo la Benishangul-Gumuz wameuawa na Wanajeshi wa #Ethiopia

> Nchi hiyo imekuwa na machafuko tangu Abiy Ahmed aingie madarakani

Soma - https://jamii.app/42Ethiopia
- Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watendaji wa JamiiForums tunakutakia Sikukuu njema ya Krismasi

- Kama mteja na mfuatiliaji wa kazi zetu tunatambua mchango na thamani yako kwetu

- Iwe siku ya furaha kwako na kwa uwapendao

#JamiiForums #MerryChristmas
KILIMANJARO: ALIYEMBAKA MTOTO WA MIAKA 11 ASAKWA

> Polisi wanamtafuta Aggrey Andrew anayekadiriwa kuwa na miaka 45-47 kwa kumbaka na kujeruhi Mtoto

> Aggrey alimlaghai Mtoto kutaka kumtuma dukani, akamfanyia unyama na kumtelekeza Mto Tarakea

Soma https://jamii.app/Mtoto11Abakwa
RUVUMA: ASKARI MBARONI KWA KUJERUHI KUTOKANA NA WIVU WA MAPENZI

- Keneth Mkwela anatuhumiwa kumjeruhi Andrew Milanzi na kitu chenye ncha kali

- Tukio limetokea ktk nyumba ya wageni baada ya Mkwela kubaini Milanzi alikuwa akiwasiliana na Mwenza wake

Soma https://jamii.app/AskariMbaroni
KENYA: MADAKTARI WAFIKIA MAKUBALIANO NA SERIKALI, WAMALIZA MGOMO

- Pande hizo zimefikia muafaka baada ya Rais Kenyatta kuingilia kati

- Madaktari wasema, wamerejea kazini ili kuhakikisha Wakenya wanasherehekea Sikukuu bila wasiwasi wa kukosa huduma

Soma https://jamii.app/StrikeOffKE
BURUNDI: RAIS AWASAMEHE WAANDISHI WALIOKUWA JELA

> Wanahabari wanne wa #IWACU walikuwa wanatumikia kifungo cha miaka 2 na nusu jela kwa shutuma za kuhatarisha usalama wa Taifa

> Walifungwa tangu Oktoba 2019 na wameachiwa huru Desemba 24

Soma - https://jamii.app/BurundiWaandishi
RAIS MAGUFULI AHIMIZA WATANZANIA KULIOMBEA TAIFA

- Pamoja na kuwatakia heri ya Sikukuu, ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kumuomba Mungu ailinde Tanzania dhidi ya #COVID19

- Ametoa wito kwa Mataifa kumtanguliza Mungu ktk kupambana na Ugonjwa huo

Soma https://jamii.app/MisaJPMDom
TANGA: DISKO TOTO ZAPIGWA MARUFUKU SIKU YA KRISMASI

> Polisi wamesema baadhi ya waendeshaji wa Disko hizo huzidisha idadi ya Watoto na kuhatarisha usalama wao kwa kipindi hichi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya

Soma - https://jamii.app/DiskoTanga