JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
CUF YAZINDUA KONGAMANO LA KUDAI KATIBA MPYA, YATAKA MAONI YA WANANCHI KUHESHIMIWA

- Prof. Lipumba ametoa rai kwa Rais Magufuli kuwapatia wananchi #Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi

- Amesema, Rais anatakiwa kuzingatia ukomo wa Uongozi

Soma - https://jamii.app/CUFTumeKatiba
GEITA: TPSC KUJENGA TAWI CHATO

> Chuo cha Utumishi wa Umma #Tanzania kinatarajia kujenga Tawi jipya eneo la Rubambangwe ambalo litahudumia Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa

> Tayari fedha za kuanza ujenzi zimeshapatikana, kinachosubiriwa ni hati

Soma - https://jamii.app/ChatoTPSC
UPINZANI WA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI WATAKA UCHAGUZI KUAHIRISHWA

- Muungano wa Upinzani nchini humo wasema Uchaguzi wa Desemba 27 hauwezi kufanyika kutokana na ghasia zinazoendelea

- Serikali imesema lazima zoezi liendelee kama ilivyopangwa

Soma https://jamii.app/UchaguziCAR
WAUZA KUKU WATAKIWA KUUZA KWA UZITO NA SIO KUKADIRIA ILI KUEPUKA HASARA

> Utafiti umegundua jogoo akipimwa urefu na kuku jike akipimwa upana unaweza kukadiria uzito

> Mfugaji anaweza tumia njia hiyo akiona mzani ni gharama kubwa

Soma https://jamii.app/KukuUzito
RUKWA: UHABA WA MADARASA WAPELEKEA WANAFUNZI 564 KUKOSA NAFASI ZA KIDATO CHA 1

> RC Joachim Wangabo amewaagiza watendaji wa Kalambo na Sumbawanga kuhakikisha Madarasa yanapatikana

> Mkoa wa Rukwa una Kata 27 ambazo hazina Shule za Sekondari

Soma https://jamii.app/RukwaMadarasa
SOMALIA NA KENYA ZAHIMIZWA KUMALIZA MVUTANO BAINA YAO

- Mataifa hayo yametakiwa kumaliza mgogoro kupitia mazungumzo

- #Somalia ilivunja uhusiano wa Kidiplomasia na #Kenya na kuishutumu Nchi hiyo kukiuka mipaka inayolinda Uhuru wa Taifa lao

Soma - https://jamii.app/KenyaSomaliaIGAD
MTWARA: UDUMAVU WATAJWA KUCHANGIA WANAFUNZI KUFELI MITIHANI

- Wataalamu wa lishe Mkoani humo waagizwa kufanya Utafiti baada ya Udumavu kuonekana kuwepo kwa kiwango kikubwa

- Mkuu wa Mkoa asema tatizo hilo linarudisha nyuma maendeleo ya Elimu

Soma https://jamii.app/UdumavuElimuMtwr
#CORONAVIRUS: MAELFU WAPIMWA THAILAND BAADA YA MLIPUKO KUIBUKA SOKONI

- Ni baada ya maambukizi mengi kuhusishwa na Soko kubwa zaidi la vyakula vya Baharini

- Kutokana na hali hiyo, Wafanyakazi wa Soko hilo wameagizwa kubaki nyumbani

Soma - https://jamii.app/Covid19-TH
SERIKALI YATOA ONYO KWA WATUMISHI WANAOPIGA RISASI RAIA HIFADHINI

- Watumishi wa Idara ya Wanyamapori wapigwa marufuku kupiga risasi wananchi wanaofanya shughuli mbalimbali ikiwemo ujangili

- Wametakiwa kuacha vitendo hivyo na kutumia Sheria

Soma https://jamii.app/OnyoRisasiRaia
DODOMA: TAWA YAZINDUA BUCHA LA NYAMA PORI

> Hafla za Uzinduzi zilifanyika maeneo ya Chang'ombe ambapo Bucha hiyo imekuwa ya kwanza kati ya Bucha 46 zilizopata usajili

Soma https://jamii.app/DodomaTAWA
TANGA: WAKANDARASI MIRADI YA MAJI WATAKIWA KUACHA SIASA KWENYE KAZI

- Wakandarasi wametakiwa kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuacha siasa

- Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Mahundi amesema, mazoea hayo yanakwamisha malengo ya maendeleo

Soma - https://jamii.app/MiradiMaji
SAUDI ARABIA YAFUNGA ANGA NA MIPAKA KUDHIBITI AINA MPYA YA #COVID19

> Aina mpya ya #COVID19 iliyogundulika Uingereza yaifanya Saudi Arabia kufunga anga na mipaka hadi Desemba 27

> Shughuli za ndani zitaendelea kwa kufuata miongozo ya #Afya

Soma https://jamii.app/COVID19SaudiArabia
#KENYA: MADAKTARI WA HOSPITALI ZA UMMA WAGOMA

- Wameungana na Watumishi wengine wa #Afya kwenye mgomo baada ya mazungumzo na Serikali kugonga mwamba

- Wanalalamikia kutopewa Bima ya Afya na vilevile, kufanya kazi kwenye mazingira magumu

Soma - https://jamii.app/DoctorsStrikeKE
SAYARI ZA JUPITER NA SATURN KUONEKANA KTK UMBO MOJA LEO

> Jupiter na Saturn zitaonekana ktk umbo moja kutoka Duniani tukio ambalo hutokea mara 1 kila baada ya miaka zaidi ya 400

> Ili kushuhudia tukio, utapaswa kuangalia Kaskazini Magharibi

Soma https://jamii.app/JupiterSaturn
POLISI: MAUAJI MENGI YANATOKANA NA WIVU WA MAPENZI

- Jeshi la Polisi limewataka Viongozi wa Dini kutoa Elimu ili kupunguza vifo hivyo

- Matukio mengine yaliyotajwa ktk Ripoti ya Polisi 2020 ni unyang'aji wa kutumia silaha na Shule kuungua

Tazama - https://youtu.be/f8HyTmMTXH4
KIJUE KISIMA CHA AJABU KILICHOPO BAGAMOYO

> Kisima cha miaka zaidi ya 800 kilichopo Kaole kinastaajabisha kutokana na Maji yake kutopungua kwa Majira yote ya Mwaka

> Pia, kinatoa Maji yasiyo na chumvi licha ya kuwa karibu sana na Bahari

Soma https://jamii.app/KisimaKaole
WAKURUGENZI 4 WATAKIWA KUJIELEZA KWA KUZUIA WALIMU KUHUDHURIA MKUTANO

> Wakurugenzi wa Msalala, Kahama, Korogwe na Sikonge wametakiwa kueleza sababu za kutowaruhusu Walimu kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSSA)

Soma https://jamii.app/DEDsKujieleza
JE WAJUA? NCHINI SUDAN MTU MWEUSI HUITWA MTUMWA

> Nafasi nyingi za Kisiasa zinakaliwa na Waarabu na Wanubi ambao ni weupe huku Watu weusi wakifanya kazi za kawaida

> Ndoa kati ya Mtu mweusi na mweupe huonekana kama kitu kibaya kiasi cha Wahusika kukutana na upinzani mkubwa ktk Jamii

Soma - https://jamii.app/SudanUbaguzi
MAREKANI: JOE BIDEN APATIWA CHANJO YA #COVID19

> Rais mteule wa #Marekani Joe Biden amepewa chanjo hiyo 'live' ili kuonesha zoezi hilo ni salama

> Aidha, Rais Trump ambaye mwezi Oktoba alipata Corona, hajasema ni lini atapokea chanjo hiyo

Soma https://jamii.app/ChanjoBiden
WAZIRI MKUCHIKA: AJIRA HAZITATOLEWA KWA UPENDELEO, TARATIBU ZITAFUATWA

- Asema, Serikali imewekeza ktk Teknolojia na maisha ya kupendeleana ili kupata Ajira yamekwisha

- Aonya walio na mazoea ya kuajiriwa kwa kuwaandikia viongozi vikaratasi

Soma https://jamii.app/MfumoAjiraTZ