JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TCRA: WATAKAORUHUSIWA KUTENGENEZA SIMU NI MAFUNDI WENYE LESENI WALIOSOMA VETA AU DIT

> Ili kuwaondoa Mafundi Vishoka TCRA wameanza kutoa leseni kwa mafundi waliokidhi vigezo

> Pia TCRA, ina mpango wa kujenga Kiwanda cha Kutengeneza Simu

Soma https://jamii.app/TCRAMafundi
MITAMBO YA UMEME YA SYMBION POWER KUPIGWA MNADA

- Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi imeamuru hivyo baada ya Symbion kushindwa kuwalipa mishahara Wafanyakazi kwa miaka mitatu

- Baadhi ya Wafanyakazi wamesema wanadai zaidi ya Bilioni 12

Soma - https://jamii.app/MnadaSymbion
WHO YAONDOA HOFU KUHUSU AINA MPYA YA VIRUSI VYA CORONA

- Shirika la Afya limesema halina ushahidi unaoonesha aina hiyo mpya inafanya watu kuumwa zaidi

- Pia, limesema Chanjo za #COVID19 zina uwezo wa kutoa kinga, lakini uchunguzi unaendelea

Soma https://jamii.app/WHOCoronaVirus
TAKRIBAN TSH BILIONI 1.2 ZILITUMIKA KUPAMBANA NA UVUVI HARAMU

> Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul, amewataka wanaojihusisha na Uvuvi usiozingatia Sheria na taratibu kuacha kwasababu Serikali haitakuwa na huruma kwa watakaokamatwa

Soma https://jamii.app/UvuviHaramu
VIONGOZI WA VITUO VYA AFYA WATAKIWA KUHESHIMU FEDHA ZA DAWA

- Waziri wa Afya ametaka fedha kuheshimiwa ili kuondoa kero ya ukosefu wa Dawa

- Asema, yapo maoni mengi kuhusu ukosefu wa dawa hivyo ni lazima kufanya upekuzi wa matumizi ya fedha

Soma https://jamii.app/FedhaDawa
SERIKALI YAAGIZA KURASIMISHWA KWA TAARIFA ZA WANANCHI

- Waziri wa Katiba na #Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza Taarifa za Wananchi ambazo zimesajiliwa ktk Mfumo wa Serikali kurasimishwa ili kuwaondolea usumbufu wa kujisajili mara kwa mara

Soma https://jamii.app/TaarifaWananchi
WADAU WALALAMIKIA UONGOZI WA DAR GROUP, WAIOMBA SERIKALI IICHUNGUZE

> Hospitali ya Dar Group ilikuwa ikiendeshwa chini ya mashirika zaidi ya 100 ambapo mengi kati yao yameshakufa

> Hivi sasa kuna Bodi ya wajumbe ambayo haiwezi kumuwajibisha Mkurugenzi Mkuu wa hospitali

> Hali hiyo imepelekea Mkurugenzi kuwanyanyasa Watendaji wa Hospitali bila kuwa na kumuwajibisha

Mjadala - https://jamii.app/DarGroup
SINGIDA: TSH. MILIONI 88.8 ZA MIKOPO UMIZA ZAREJESHWA

> TAKUKURU imerejesha fedha za Raia walizodhulumiwa na Kampuni za Mikopo zinazofanya shughuli Kinyume cha Sheria

> TAKUKURU imebaini baadhi ya Wakopeshaji hawaandai Mikataba ya Ukopeshaji

Soma https://jamii.app/MikopoUmizaSingida
URUSI NA RWANDA ZAPELEKA MAJESHI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

- Nchi hizo zimefanya hivyo kusaidia kupambana na vurugu kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumapili

- Serikali inamshutumu Rais wa zamani, Francois Bozize, kupanga mapinduzi

Soma https://jamii.app/ElectionsCAR
MANYARA: TAKUKURU YAREJESHA EKARI 27 ZILIZOPORWA KWA MIAKA 10

> Imbori Hando (72) Mkazi wa Kiteto aliporwa eneo lake na aliposhinda kesi Mahakama ya Ardhi ya Kata, Viongozi wa Serikali na Chama walimpuuza

Soma https://jamii.app/PCCBManyara
MADEREVA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA KUTOHATARISHA MAISHA YA WATU

- Serikali imesema hatua zitachukuliwa dhidi ya mabasi yanayokiuka Sheria

- Takwimu zinaonesha vyanzo vikubwa cha ajali ni pamoja na ubovu wa vyombo vya moto na mwendo kasi

Soma https://jamii.app/SheriaMadereva
WAKURUGENZI WATAKAOKUSANYA CHINI YA 50% KUONDOLEWA

> Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, amewaagiza Wakurugenzi wote kufikisha zaidi ya 50% ya makusanyo ya mapato ifikapo Januari 15, 2021

> Januari 15 atatoa taarifa ya miezi 6 ya ukusanyaji

Soma https://jamii.app/MapatoDEDs
ZANZIBAR: WAKURUGENZI WA MANISPAA WASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI

> Mkurugenzi wa Manispaa ya Mjini na Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Magharib 'A' wamesimamishwa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ubadhilifu wa mali za Umma

Soma - https://jamii.app/ZnzDEDs
ATHARI ZA #COVID19: BUNGE LA MAREKANI LAIDHINISHA KUTOA BILIONI 900 KUSAIDIA WANANCHI

- Ktk fedha hizo, zaidi ya Dola Bilioni 300 zitatumika kusaidia Wafanyabiashara

- Rais Trump anatarajiwa kusaini muswada huo kabla haujaanza kutekelezwa

Soma - https://jamii.app/USBungeFedha
MWANZA: MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKEWE

> Benson Oluochi (54) anatuhumiwa kumuua Elizabeth Benson (45) kwa kumshambulia na fimbo sehemu mbalimbali za mwili akimtuhumu kwa Usaliti

> Uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani

Soma - https://jamii.app/AuaMkeFimbo
TABORA: JELA MIAKA 30 KWA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI WA DARASA LA 6

> Rwaki Zakaria anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Januari na Februari 2020

> Kosa lake ni kinyume na Kifungu cha 60 cha Sheria ya Elimu Sura 353 iliyofanyiwa marekebisho 2019

Soma https://jamii.app/TaboraJela30
NADHARIA ZINAWAFANYA WANAOIHITIMU UDAKTARI WAOGOPE DAMU

> Rais wa Chama cha Madaktari amesema, Wanafunzi wanafundishwa nadharia kuliko vitendo

> Mazingira ya ufundishaji yamekuwa magumu, hivyo ubora wa Madaktari wanaozalishwa unakuwa mdogo

Soma https://jamii.app/WahitimuUdaktari
DKT. MWIGULU ATAKA SHERIA ZITAFSIRIWE KWA KISWAHILI

> Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametaka Sheria za Nchi zitafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili ili Wananchi waweze kuzielewa hasa katika Uendeshaji wa kesi na kuelewa hukumu

Soma - https://jamii.app/SheriaKiswahili
MKURUGENZI WA HALOTEL NA WENZAKE 4 WAHUKUMIWA FAINI YA TSH MILIONI 24 AU JELA MWAKA 1

> Walitakatisha fedha na kuisababishia TCRA hasara ya Tsh. bilioni 75

> Pia, Mahakama imeihukumu Halotel kulipa fidia ya Tsh. bilioni 30 ndani ya mwaka 1

Tazama https://youtu.be/0s01K4ZUMtc
#JFLeo
TEMEKE: MKURUGENZI ADAIWA KUTUMIA UBABE KUNUNUA GARI LA TSH. MILIONI 470

> Madiwani wasema Sheria ya manunuzi ya umma haikuzingatiwa ila Kamati ililazimishwa

> Pia, Mkurugenzi anatuhumiwa kunyanyasa Watumishi kwa kuwafungia ndani wakichelewa

Soma https://jamii.app/DEDTMK