JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#UGANDA: MUSEVENI ASEMA ATAPAMBANA NA WAPINZANI WANAOSUMBUA WAFUASI WAKE

- Ametishia kutumia nguvu kukabiliana na Wanasiasa anaodai wanatishia na kuwasumbua wafuasi wa Chama chake

- Asema, Wapinzani wanalazimisha wafuasi wake kuwaunga mkono

Soma https://jamii.app/NRM-Museveni
TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA ZATAKIWA KUJIELEZA KUHUSU UCHANGIAJI WA MFUKO WA SERIKALI

> Waziri Dkt. Mpango ametoa siku 9 kwa Taasisi zilizochangia chini ya 15% kujieleza sababu za kutochangia huduma za Jamii na kutozingatia ukomo wa matumizi

Soma https://jamii.app/WakuuKujieleza
NDUGAI: KUKAA VIJIWENI NA KUSUBIRI AJIRA ZA SERIKALI NI MTAZAMO HASI

- Asema inasikitisha Vijana wanashinda na simu wakati wangeweza kuibua miradi itakayowaondolea Umasikini

- Awataka watumie fursa zilizopo kuibua miradi ya kuwainua kiuchumi

Soma https://jamii.app/VijanaAjira
TAASISI ZA FEDHA ZASHAURIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA RIBA

- Taasisi hizo na Benki zimetakiwa kupunguza gharama za uendeshaji ili kumudu kupunguza riba kwa wateja

- BoT imesema riba kubwa inaathiri wananchi na uendeshaji wa shughuli za kiuchumi

Soma https://jamii.app/RibaBenki
GEITA: WATATU WAFUNGWA MIAKA MITANO KWA UNUNUZI HEWA WA DAWA NA VIFAA TIBA

- Walishtakiwa kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka, kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri, kupata manufaa yasiyostahili na kuisababishia Serikali hasara ya 32,700,000

Soma https://jamii.app/3JelaGeita
PROF. NDALICHAKO AWAONYA MAAFISA ELIMU WANAOSHIRIKI WIZI WA MITIHANI

- Asema, wanaangamiza Taifa kwa kuzalisha Wataalamu wasioweza kutumia Elimu yao, kwani hawakutumia akili kufaulu

- Wakuu wa Shule waliotishwa na Maafisa hao watakiwa kuripoti

Soma https://jamii.app/WiziMitihani
RAIS MAGUFULI AMTEUA MWANGESI KUWA KAMISHNA WA MAADILI

> Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ameteuliwa baada ya Harold Nsekela kufariki Dunia

> Ataapishwa kesho, Desemba 24 asubuhi, Ikulu ya Chamwino

Soma - https://jamii.app/TeuziMaadili
URUSI: RAIS PUTIN ASAINI MUSWADA UNAOMPA KINGA YA KISIASA MILELE

- Chini ya Muswada huo, Rais Vladimir Putin, Marais waliopita na Familia zao hawatafunguliwa mashtaka

- Rais atavuliwa kinga atakaposhutumiwa kufanya kosa kubwa kama uhaini

Soma - https://jamii.app/PutinKingaMuswada
KENYA: UNICEF YATOA ULINZI KWA WATOTO WA KOROGOCHO

> Matukio ya unyanyasaji yameongezeka kwa Watoto wa Korogocho kipindi hiki cha Shule kufungwa kutokana na #COVID19

> UNICEF wamefadhili mafunzo ili kuweza kudhibiti ukuaji wa matukio hayo

Soma https://jamii.app/KorogochoKenya
UN WATOA WITO KWA SERIKALI KULINDA WAANDISHI WA HABARI KIPINDI CHA #COVID19

> UN wamesema Wanahabari wanapata mazuio na adhabu ktk kutimiza wajibu wao kipindi hiki cha COVID19

> Serikali ziwalinde Waandishi ili kukuza uhuru wa habari

Soma https://jamii.app/MediaCOVID19

#PressFreedom
UGANDA: WFP KUPUNGUZA MGAO WA CHAKULA NA FEDHA KWA WAKIMBIZI

- Shirika la Mpango wa Chakula limesema zaidi ya wakimbizi Milioni 1.2 nchini humo watapunguziwa mgao kuanzia Februari

- WFP imesema imepokea nusu ya Fedha inazohitaji kuwahudumia

Soma https://jamii.app/WFPFoodUG
SERIKALI KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA WANANCHI YA KUIBIWA DATA NA VIFURUSHI

> Dkt. Faustine Ndugulile amewaelekeza TCRA-CCC kutathmini malalamiko ya Raia kuwa wanaibiwa vifurushi na Kampuni za Simu

> TCRA-CCC wamekiri kupokea malalamiko mengi

Soma - https://jamii.app/DataWiziTCRA
DAR: ADAIWA KUJINYONGA NDANI YA MAHABUSU YA POLISI

> Stella Moses (30) amejinyonga akiwa kituo cha Polisi Mburahati alipojisalimisha Desemba 20 baada ya kutafutwa

> Inaelezwa alikuwa na madeni mengi ambayo huenda ndiyo sababu ya kujinyonga

Soma - https://jamii.app/SuicideInCustody
#UGANDA: MWANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU AKAMATWA

> Polisi wamekiri kumkamata Nicholas Opiyo kwa tuhuma za kutakatisha fedha

> Wanaharakati wasema sababu za kumkamata ni za kisiasa zinazolenga kuwavunja moyo wa kufuatilia mchakato Uchaguzi

Soma https://jamii.app/ActivistUganda
KILIMANJARO: KIJANA ATUHUMIWA KUMUUA BABA YAKE MZAZI

> James Kimario anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Welanzari Kimario (56) kwa kumkatakata na panga

> Pia, amemjeruhi mama yake mzazi na sababu ya tukio hilo bado haijabainishwa

Soma https://jamii.app/KijanaAua
WAZIRI UMMY MWALIMU AHIMIZA WATANZANIA KULINDA MUUNGANO

- Amesema licha ya changamoto zilizopo, kuna fursa kwa Wananchi kujiletea Maendeleo

- Amesisitiza umuhimu wa kutumia fursa zilizopo #Tanzania Bara na Visiwani #Zanzibar ipasavyo

Soma - https://jamii.app/MuunganoTZ
MGANGA MKUU WA LONGIDO ASIMAMISHWA KAZI KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA FEDHA

> Naibu Waziri wa #Afya, Dkt. Godwin Mollel, amemsimamsha kazi Jastice Munisi kwa kutosimamia fedha zinazotolewa kwa ajili ya Miundombinu na ununuzi wa Dawa na Vifaa Tiba

Soma - https://jamii.app/MgangaAsimamishwa
#UGANDA: VIONGOZI WA DINI WATAKA UCHAGUZI KUAHIRISHWA

- Wamependekeza uahirishwe kwa miaka 3, na Katiba kubadilishwa ili kumruhusu Rais Museveni kubaki madarakani

- Wamesema ni kwasababu ya #COVID19 na mivutano baina ya Wagombea na Polisi

Soma - https://jamii.app/ElectionsUG
DAR: MATUKIO YA UHALIFU YARIPOTIWA KUPUNGUA

> Kuanzia Januari hadi Novemba 2020 kumekuwa na matukio ya jinai 128,064 tofauti na 2019 ambapo yalikuwa 138,024

> Hali hiyo imetokana na doria mbalimbali pamoja na ushirikiano kutoka kwa raia wema

Tazama https://youtu.be/rj4MNGHY25o
#JFLeo
SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUTUMIA TEHAMA KUCHOCHEA UKUAJI UCHUMI

- Waziri Mkuu atoa rai kwa wananchi kutumia vizuri Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kupunguza umaskini

- Serikali itaongeza matumizi ya mawasiliano ya kasi kutoka 45% hadi 80%

Soma https://jamii.app/TEHAMAUchumi