JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#GOOGLE YAPATA SHAMBULIO LA MTANDAO

> Kampuni hiyo imepata shambulio la mtandao lililodumu kwa dakika 45

> Huduma zake mbalimbali kama Gmail na YouTube zilishindwa kupatikana kwa baadhi ya nchi ikiwemo Marekani, Canada, India na Uingereza

Soma https://jamii.app/GoogleIsDown
ZANZIBAR: MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEMBAKA MWANAE, KISA BINTI KAZOEA KUINGILIWA

> Mahakama ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba imemuachia huru Salim Khamis Ali (43) aliyembaka binti yake wa miaka chini ya 13 kwa ushahidi wa vipimo kuwa binti huyo alizoea kuingiliwa

> Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ) kimesema hakiridhishwi na Hukumu za Kesi zinazohusu Ukatili wa Watoto Visiwani humo

Soma https://jamii.app/TAMWAZNZ
#UHOLANZI YATANGAZA LOCKDOWN YA NCHI NZIMA KWA WIKI TANO

> Ni kuanzia Desemba 15, 2020 hadi Januari 19, 2021 hivyo Shule, Maduka na Makumbusho vitafungwa

> Wamefikia hatua hiyo baada ya kuongezeka maambukizi ya #COVID19 wiki mbili zilizopita

Soma https://jamii.app/5WeeksLockdown
SIMIYU: RC AWATAKA MADIWANI KUACHA TABIA YA KUFUKUZA WATUMISHI KIHOLELA

- RC Anthony Mtaka amesema, hatokubali Madiwani wa Halmashauri yoyote kukaa kikao na kuazimia kumfukuza mtumishi wa Serikali awe Mkurugenzi, Mkuu wa Idara au kitengo

Soma - https://jamii.app/DiwaniKufukuza
#Siasa
MUSEVENI: HUWA NAKASIRIKA WATU WAKINIAMBIA NIONDOKE MADARAKANI

- Rais wa #Uganda ambaye anawania muhula wa 6, amesema hajaona mtu mwenye uwezo wa kuongoza, hivyo ataendelea kuwa Madarakani kwasababu Watu wanamuhitaji kuendelea kuongoza

Soma - https://jamii.app/MuseveniMadaraka
#UGElection
TANZIA: MMILIKI WA HOTELI ZA SEA CLIFF NA WHITE SANDS AFARIKI

- M/kiti Mtendaji Motisun Group ambaye ni miongoni mwa Mabilionea Nchini #Tanzania, Subhash Patel amefariki leo

- Pia, alikuwa M/kiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI)

Soma https://jamii.app/SubhashPatelDies
SOMALIA YASITISHA MAHUSIANO NA KENYA, WANADIPLOMASIA WATAKIWA KUONDOKA

> #Somalia imetangaza kusitisha uhusiano wake na #Kenya kwa kuwafukuza Wanadiplomasia wote wa Kenya kuanzia leo

> Pia, nchi hiyo imewataka Wanadiplomasia wake kurejea

Soma - https://jamii.app/KEvsSomalia
JOE BIDEN ATHIBITISHWA RASMI KUWA RAIS WA MAREKANI

- Wajumbe wa Electoral College wamemthibitisha Biden kuwa Rais wa Taifa hilo kwa kura zaidi ya 270

- Donald Trump anakuwa Rais wa 5 kupoteza Madaraka baada ya muhula 1 wa Uongozi

Soma - https://jamii.app/JoeBidenVerified
#USElection
KENYA YAAGIZA DOZI MILIONI 24 ZA CHANJO YA #COVID19

> Dozi hizo zitagharimu Tsh. Bilioni 207.83 na zitatolewa kwa Watumishi walio hatarini kupata maambukizi na Wazee

> #Kenya ni nchi iliyoagiza dozi nyingi zaidi kwa nchi za Afrika Mashariki

Soma https://jamii.app/24DoziCOVID19
TANZIA: MSANII MKONGWE WA MAIGIZO, MZEE JENGUA AFARIKI DUNIA

> Mohammed Fungafunga maarufu Mzee Jengua amefariki leo asubuhi huko Mkuranga, Pwani

> Baadhi ya filamu na tamthilia alizoigiza ni Kidedea, Handsome wa Kijiji na Maneno ya Kuambiwa

Soma https://jamii.app/JenguaAfariki
#JFLeo
RC KUNENGE: ANAYEJIONA HAWEZI KWENDA NA KASI YA SERIKALI HII, AKAE PEMBENI

> Mkuu wa Mkoa wa Dar, Aboubakar Kunenge, amewataka Watendaji wote kuacha kujivuta ktk kusimamia majukumu yao na kuhakikisha miradi inayowalenga Wananchi inakamilika

Soma - https://jamii.app/KunengeKasiWatendaji
UN WATOA WITO KWA NCHI KUTANGAZA DHARURA YA HALI YA HEWA

> Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres, amesema Viongozi wa Duniani wanapaswa kutangaza dharura ya hali ya hewa katika Nchi zao ili kuchochea hatua za kuzuia ongezeko la Joto Duniani

Soma - https://jamii.app/ClimateEmergency
#Climate
MWANASHERIA MKUU WA MAREKANI ATANGAZA KUJIUZULU

> William Barr ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais Donald Trump amesema ataachia rasmi nafasi yake ifikapo Desemba 23

> Barr alisema Idara ya #Sheria haijaona udanganyifu katika Uchaguzi Mkuu

Soma https://jamii.app/AGMarekani
KAGERA: WANAFUNZI 59 WA VETA WAKAMATWA KWA UDANGANYIFU

> Wanashikiliwa na TAKUKURU baada ya kukutwa na Simu ktk chumba cha Mtihani

> Pia, Walimu 3 wanashikiliwa na Tsh. 151,000 zinazodaiwa kuchangwa na Wanafunzi ili kuwapatia Wasimamizi zimekamatwa

Soma https://jamii.app/UdanganyifuVETA
UNICEF: WALIMU WAPEWE KIPAUMBELE KWENYE CHANJO YA #COVID19

> Imesema, Walimu wapewe chanjo baada ya Watumishi wa Afya na wengine walio katika hatari ya maambukizi ya #CoronaVirus

> Hatua hiyo itawezesha Walimu kufundisha ana kwa ana

Soma https://jamii.app/UNICEFChanjoWalimu
JE, SHERIA INASEMA NINI KUHUSU KOSA LA KUTOA RUSHWA ILI KUSHINDA MKATABA WA KUTOA HUDUMA?

Kifungu cha 16 kinatoa Adhabu ya Faini isiyopungua Milioni 1 na isiyozidi Milioni 3 au Kifungo kisichopungua miaka 3 na kisichozidi miaka 5 au vyote kwa pamoja

Pia Mahakama yaweza:

> (i) Kumwamuru mtuhumiwa kumlipa mtu au mwajiri wake kiasi chote au nusu ya pesa au mali aliyopewa rushwa;

> Au (ii) Kutaifisha pesa au mali iliyopokelewa kama rushwa na kuwa mali ya serikali

Soma https://jamii.app/MakosaRushwaAdhabu
MDAU: HUWEZI KUPATA UTAJIRI KAMA WEWE SIO MTU WA KUTUNZA SIRI

> Mdau wa JamiiForums.com anasema, Mipango ya utajiri haisemwi bali hutekelezwa na inakuwa. Mipango inayosemwa kabla haijatekelezwa kwa asilimia kubwa haiwezi kutekelezeka

> Anasema, Ukiona mtu anasema ni tajiri basi tambua huyo sio Tajiri kwasababu utajiri hauna mdomo bali una vitendo

Mjadala - https://jamii.app/KutunzaSiriUtajiri
#Mafanikio
ZANZIBAR: RAIS MWINYI AVUNJA BODI YA MELI NA UWAKALA

> Leo, Desemba 15, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Meli na Uwakala kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa Shirika hilo

Soma https://jamii.app/BodiMamlakaYaMeli
DAR: JELA MAISHA KWA KUMLAWITI BINTI YAKE WA MIAKA 11

> Huruma Mjumbe (54) amekutwa na hatia ya kumlawiti binti yake kati ya Januari 2017 na Februari 2019

> Mahakama ilijiridhisha kwa ushahidi wa Daktari na mdogo wa mtoto huyo

Soma https://jamii.app/LifeSentence
#ChildRights #JFLeo
ACT-WAZALENDO: HATUTAKWENDA UJERUMANI WALA CANADA KULALAMIKIA MASUALA YA TANZANIA

> Mbunge wa Jimbo la Konde, Khatib Haji amesema masuala ya #Tanzania yatazungumzwa Tanzania

> Asema, maridhiano yaliyofanyika ni kwa maslahi ya Wazanzibari

Soma https://jamii.app/UapishoWabungeACT
#JFSiasa