JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
LINDI: MTU MMOJA AKIMBIA NA SANDUKU LA KURA ZA UDIWANI

> Inadaiwa alifika eneo hilo na pikipiki akiwa na mwenzake na kupiga kura kama kawaida. Baada ya kutumbukiza kura yake, alibeba sanduku la kura na kutokomea nalo

Soma - https://jamii.app/UchaguziLindi

#JamiiForums #Uchaguzi2020
MEMBE APIGA KURA CHIPONDA - LINDI

> Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Bernard Membe ametimiza haki yake ya Kikatiba ya kupiga kura katika kijiji cha Chiponda, Lindi

> Bernard Membe amepiga kura hiyo leo asubuhi

#Uchaguzi2020 #TanzaniaDecides2020 #JamiiForums
UN-TANZANIA: MAGARI YALIOONEKANA KWENYE UHALIFU KATIKA JIMBO LA HAI HAYAHUSIANI NASI

> UN imeeleza magari yanaoonekana kwenye tukio la kuvamiwa hoteli ya Mbowe kuwa yana namba za usajili za kughushi. Pia yalikuwa hayatumiwi na Watendaji wao

> Freeman Mbowe alitoa video zikionesha tukio la kutekwa walinzi wake zikiwa na gari zinazofanana na za UN

Soma https://jamii.app/HaiUNResp
HAI: MBOWE AANGUSHWA KATIKA UBUNGE

> Saashisha Mafuwe wa CCM ametangazwa mshindi wa Ubunge katika Jimbo hilo baada ya kupata kura 89,786

> Aliyekuwa Mbunge wa Hai, Freeman A. Mbowe (CHADEMA) amejipatia kura 27,684 katika nafasi ya 2

Soma https://jamii.app/MboweHaiOut

#Uchaguzi2020
SHINYANGA MJINI: MGOMBEA UBUNGE CHADEMA MBARONI KWA KUFANYA FUJO

> Salome Makamba anakabiliwa na tuhuma za kufanya fujo, kuchana karatasi za matokeo ya kura na kumjeruhi Msimamizi wa Uchaguzi wa Kituo cha Shule ya Msingi Bugweto "B"

Soma - https://jamii.app/MgombeaCDMShy

#Uchaguzi2020
MBEYA MJINI: DKT. TULIA ACKSON ATANGAZWA KUSHINDA UBUNGE

- Aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge lililopita, Dkt. Tulia Ackson, kupitia CCM ametangazwa kushinda Ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 75,225

- Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CHADEMA, Joseph Mbilinyi (Sugu) ameshika nafasi ya pili baada ya kupata kura 37,591

Matokeo zaidi, tembelea https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo
NJOMBE MJINI: DEO MWANYIKA (CCM) ATANGAZWA MSHINDI WA UBUNGE

- Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Njombe Mjini amemtangaza Deodatus Mwanyika wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa Ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 29,553

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020 #Tanzania2020
CCM YACHUKUA JIMBO LA MJINI MAGHARIBI - ZANZIBAR

- Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mjini Magharibi - Mtoni amemtangaza Abdul Hafar Idrisa Juma ameshinda nafasi ya Ubunge kwa jimbo hilo baada ya kupata ushindi wa asilimia 73

Matokeo zaidi, tembelea https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020 #Tanzania2020
SENGEREMA: CCM YASHINDA VITI VYOTE VYA UDIWANI

- Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda viti vyote 47 vya Udiwani katika Majimbo ya Sengerema na Buchosa Wilayani Sengerema

- Pia, chama hicho kimeshinda Uchaguzi katika Kata zote 8 za Jimbo la Tarime Mjini katika Uchaguzi

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020 #Tanzania2020
#UCHAGUZI2020: CCM WASHINDA KATA ZOTE HALMASHAURI YA MWANZA

- Msimamizi wa Uchaguzi Mwanza amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda Kata zote 18 kwenye Halmashauri ya Jiji la Mwanza

- Zoezi la kuhesabu kura za Ubunge bado linaendelea na masanduku kutoka sehemu tofauti yanaendelea kuwasili

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#JFSiasa
#UCHAGUZI2020: CCM WASHINDA KATA 24 KATI YA 25 JIMBO LA ARUSHA MJINI

- Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini amesema Chama cha Mapinduzi kimechukua Kata 24 kati ya kata 25 za Udiwani

- Upande wa Ubunge wanaendelea na majumuisho, na wamefikia Kata ya 14 hivyo sio muda mrefu watatoa matokeo ya Ubunge

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#JFSiasa
MOSHI MJINI: PRISCUS TARIMO (CCM) ASHINDA UBUNGE

- Msimamizi wa Uchaguzi wa Moshi Mjini amemtangaza Priscus Tarimo wa CCM kuwa Mbunge wa Moshi Mjini baada ya kupata kura 31,169

- Raymond Mboya kutoka CHADEMA ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 22,555 na nafasi ya 3 imechukuliwa na Buni Abdul Lamole wa ACT Wazalendo kwa kura 374

Matokeo zaidi, tembelea https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020
KATAVI: CCM YASHINDA JIMBO LA NSIMBO

> Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nsimbo amemtangaza Anna Lupembe wa CCM kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge

> Lupembe amepata kura 38,346, na amefuatiwa na Mgombea wa ACT-Wazalendo, Philipo Malaki aliyepata kura 1,292

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020
CCM YASHINDA KATA ZOTE ZA KISARAWE

> Msimamizi wa Uchaguzi Kisarawe amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda Kata zote 17 katika Jimbo la Kisarawe

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#JamiiForums #Uchaguzi2020
NEWALA MJINI: KAPTENI GEORGE MKUCHIKA (CCM) ASHINDA UBUNGE

- Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Newala Mjini Mkoani Mtwara amemtangaza Kapteni Mstaafu George Huruma Mkuchika kuwa Mbunge Mteule wa Newala Mjini kwa kupata kura 18,705

- Issa Juma Chilindima (CHADEMA) mwenye kura 12,546 amekuwa wa pili

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020
CCM YASHINDA UBUNGE MTWARA MJINI

> Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mtwara Mjini amemtangaza Hassan Seleman (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge

> Amepata kura 22,411 huku Mgombea wa CUF Abdallah Nachuma akipata kura 13,586 na Hassani Abdallah wa ACT-Wazalendo amepata kura 1,113

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020
SINGIDA MJINI: RAMADHAN SIMA (CCM) ATANGAZWA MSHINDI

- Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Singida Mjini amemtangaza Sima kuwa mshindi kwa kupata kura 23,220

- CHADEMA kupitia Mgombea wake, Rehema Nkoha aliyepata kura 15,467 imeshika nafasi ya pili

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020
KWAGILWA NHAMALO(CCM) ATANGAZWA MSHINDI UBUNGE HANDENI MJINI

- Ni baada ya kupata kura 15,241

- Nyuma yake amefuatiwa na Sonia Mgalwa wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 6,713

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo
#Uchaguzi2020
SHAMSIA MTAMBA (CUF) ATANGAZWA MSHINDI UBUNGE MTWARA VIJIJINI

- Ni baada ya kupata kura 26,262

- Hawa Ghasia (CCM) ameshika nafasi ya pili baada ya kupata kura 18,505

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020
PATROBAS KATAMBI ASHINDA UBUNGE SHINYANGA MJINI

- Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini amemtangaza Patrobas Katambi wa CCM kuwa Mshindi wa kiti kwa kura 31,831

- Salome Makamba (CHADEMA) aliyepata kura 16,608 ametangazwa kushika nafasi ya pili

Matokeo zaidi https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020