JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NEC: MUDA WOWOTE KUANZIA SASA TUTAANZA KUTANGAZA MATOKEO YA URAIS

- Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera amesema, Tume imeanza kupokea matokeo kutoka Majimboni na kuhakiki

- Amesema, kwa ngazi za Udiwani na Ubunge wenye Mamlaka ya kutangaza ni NEC hivyo Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasaidizi wao ndio watatangaza

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo
ARUMERU MASHARIKI: CCM YASHINDA KATIKA KATA 20

- Wagombea wote wa Udiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Kata 26 wameshinda

- Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo, Emmanueli Mkongo amesema Kata 6 kati ya 26 Wagombea wa CCM walipita bila kupingwa na Jimbo lilikuwa na vituo 521 vya kupiga kura

Matokeo zaidi https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo
#Uchaguzi2020
KENNETH ERNEST NOLLO (CCM) ASHINDA UBUNGE BAHI

> Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Bahi, Dkt. Fatuma Mganga amemtangaza Mgombea Ubunge kupitia CCM, Kenneth Ernest Nollo kushinda kiti cha Ubunge kwa kura 40,628 dhidi ya Godfrey Job wa CUF aliyepata kura 1,756

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo
KAPUFI ASHINDA UBUNGE JIMBO LA MPANDA MJINI

- Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sebastian Kapufi ametangazwa kushinda nafasi ya Ubunge kwa kupata kura 24,020

- Nyuma yake amefuatiwa na Rhoda Kunchela kutoka CHADEMA aliyepata kura 13,611

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo
#Uchaguzi2020
MWITA WAITARA ASHINDA UBUNGE WA TARIME VIJIJINI

> Msimamizi wa Uchaguzi amemtangaza Mwita Waitara (CCM) kuwa mshindi wa Ubunge wa Jimbo hilo akipata kura 35,758 dhidi ya John Heche (CHADEMA) aliyepata kura 18,757

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020
AMSABI MRIMI ASHINDA UBUNGE JIMBO LA SERENGETI

> Mgombea Ubunge wa Jimbo la Serengeti, Amsabi Mrimi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ameshinda kwa kura 47,499

> Catherine Ruge wa CHADEMA amepata kura 19,347

Matokeo zaidi, soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo

#Uchaguzi2020
JESCA MSAMBATAVANGU ATANGAZWA MSHINDI JIMBO LA IRINGA MJINI

- Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Iringa Mjini amemtangaza Mgombea wa CCM kuwa mshindi wa Ubunge ktk Jimbo hilo kwa kupata kura 36,034

- Amefuatiwa na Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMA aliyepata kura 19,331

Matokeo zaidi https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo
#Uchaguzi2020
DAVID SILINDE(CCM) ATANGAZWA MSHINDI JIMBO LA TUNDUMA

- Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Tunduma ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 43,276

- Amefuatiwa na Frank Mwakajoka wa CHADEMA aliyepata kura 12,433

Matokeo zaidi https://jamii.app/Uchaguzi2020Matokeo
#Uchaguzi2020 #TanzaniaElections2020