JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UMOJA WA AFRIKA WATOA WITO KWA #TANZANIA KUFANYA UCHAGUZI WA AMANI

> M/Kiti wa AU ametoa wito kwa Vyama vya Siasa na wafuasi wake kujizuia kufanya vitendo vya ghasia na kuisihi Serikali kuhakikisha kuna mazingira mazuri ya Raia kupiga kura

Soma - https://jamii.app/AUElectionTZ
#TZ2020
JE, WAJUA KUWA SIMU YAKO INAWEZA KUKUJULISHA KITUO CHAKO CHA KUPIGIA KURA?

> Piga *152*00# chagua 9, kisha chagua 1. Weka namba ya kadi ya mpiga kura bila herufi ‘T’ wala alama ‘-‘

> Utapokea ujumbe wenye taarifa na kituo cha kupigia kura

Soma https://jamii.app/SimuKituoKura
#TZ2020
WALINZI WA MBOWE WADAIWA KUTEKWA

> Freeman Mbowe ametoa taarifa kuwa maisha yake yapo hatarini

> Amedai kuwa walinzi wake wawili wametekwa na majambazi wenye silaha nzito saa nane usiku wa kuamkia leo ktk hoteli yao

Soma https://jamii.app/MboweWalinzi
#TZ2020
TANZANIA YAFANYA UCHAGUZI MKUU LEO - OKTOBA 28, 2020

> Waliojiandikisha ni 29,188,347 na jumla ya Vituo vya Kupigia Kura ni 80,155

> Vyama ya Siasa 19 vinashiriki ktk Uchaguzi, Wagombea Ubunge ni 1,257, na Wagombea Udiwani ni 9,237

Soma https://jamii.app/UchaguziTZ

#Uchaguzi2020
KAWE, DAR: Wananchi wamejitokeza ili kutumia haki yao kikatiba kuchagua viongozi

> Pichani ni wananchi wa Kawe, Ukwamani wakiwa katika vituo wakihakiki majina kwanza na kisha kwenda kupiga kura

#TZ2020 #TanzaniaElections2020 #Uchaguzi2020
WAGOMBEA WANAWAKE KATIKA NAFASI YA URAIS, UDIWANI NA UBUNGE

> Kwa mujibu wa NEC, Wagombea wanawake ktk kiti cha Rais ni 2 kati ya 15 sawa na 13% na kwa Makamu wa Rais wanawake ni 5

> Wagombea Ubunge ni 1,257 na Wanawake walioteuliwa ni 294 sawa na 23%. Wagombea Udiwani ni 9,237 na Wanawake walioteuliwa ni 669 sawa na 7.2%

Soma - https://jamii.app/Wanawake2020
#Uchaguzi2020
UCHAGUZI ZANZIBAR: DKT. HUSSEIN MWINYI APIGA KURA, AHIMIZA WAZANZIBARI KUENDELEA KUJITOKEZA

> Mgombea huyo wa Urais (CCM) ametoa rai kwa Wazanzibari kuendelea kujitokeza Vituoni

> Mgombea Mwenza wa Urais JMT, Samia Suluhu naye amepiga kura Zanzibar akisema hali ipo vizuri

Tazama https://youtu.be/bYblLXBN47o
MAALIM SEIF ATIMIZA HAKI YAKE YA KUPIGA KURA

> Amefika ktk Kituo cha Garagara, Jimbo la Mwera na kupiga kura mapema leo

> Asema ametiwa moyo na watu wengi kujitokeza kupigia kura ila Wananchi wengi wana malalamiko ya kutokuona majina yao kwenye vituo

#TanzaniaDecides2020 #Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI NA MKEWE WAPIGA KURA DODOMA

> Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Magufuli na Mama Janet Magufuli wametimiza haki yao ya Kikatiba ya kupiga kura katika kijiji cha Chamwino jijini Dodoma

> Amewasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kufanya maamuzi yaliyomo ndani ya mioyo yao

#Uchaguzi2020
DKT. TULIA ACKSON: NINA UHAKIKA NA USHINDI WA CCM MBEYA MJINI

> Mgombea huyo wa Ubunge asema ana uhakika CCM itaibuka kidedea ktk Jimbo hilo

> Ametaja changamoto kwa baadhi ya Raia kukata tamaa kupiga kura baada ya kukosa Majina yao Vituoni

Soma https://jamii.app/TuliaUshindiCCM
#TZ2020
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MZOZO WATOKEA BAINA YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NA HALIMA MDEE

> Inaelezwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), Halima Mdee, amevutana na Jeshi la Polisi pamoja na Wasimamizi wa Uchaguzi kwa madai ya kuingilia zoezi hilo

> Mgogoro huo umetokea baada ya Mdee kudai kuna mabegi yenye kura feki yanayoingizwa Kituoni hapo

#Uchaguzi2020 #JamiiForums
RC wa Mbeya, Albert Chalamila: Niendelee kuwasisitiza, leo kama ni maandamano basi naomba viongozi wao, nipo chini ya magoti yao, viongozi ndio wawe mbele, ili kama ni kufyatua basi wafyatuliwe vizuri

- Kwasababu itakuwa ni uchokozi, na itakuwa umeletewa kidole mdomoni

#Uchaguzi2020