JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FAHAMU ALAMA INAYOKUBALIKA WAKATI WA KUPIGA KURA NA KUHESABU KURA

- (1) Alama inayokubalika ktk chumba kilichopo wazi kwenye karatasi ya kura ni alama ya vema (√)

- (2) Alama nyingine zinazokubalika ni alama eksi yaani “X”

Zaidi, soma > https://jamii.app/AlamaZaKura

#Uchaguzi2020
CHAUMMA WALALAMIKIA MAWAKALA WAO KUHUJUMIWA

> Msimamizi Jimbo la Rorya aliwaondoa Mawakala wa CHAUMMA baada ya Chama hicho kusema hakitambui Uanachama wao

> Chama hicho kimelalamika kukosa imani kikisema Mkurugenzi wa NEC hapokei simu

Soma - https://jamii.app/MawakalaCHAUMMA
#TZ2020
KITUO CHA KUPIGA KURA KINAWEZA KUFUNGWA KWA SABABU YA VURUGU

- Endapo mchakato wa kupiga kura utaharibiwa na vurugu na bado kuna wapiga kura hawajamaliza kupiga kura, Msimamizi wa kituo ataahirisha zoezi hilo mpaka siku inayofuata

- Baada ya kuahirisha Msimamizi atatoa taarifa haraka kwa Msimamizi mkuu wa Uchaguzi

- Iwapo Upigaji Kura utaahirishwa ktk kituo chochote, masaa ya kupigia kura katika Siku nyingine iliyopendekezwa yatakuwa sawa kama yale ya siku halisi ya kupiga Kura

Soma > https://jamii.app/VuruguKituoni

#Uchaguzi2020
MAJALIWA: WATANZANIA MSICHAGUE VIONGOZI KWA JAZBA AU HASIRA

> Amewataka wananchi kuchagua Chama chenye mwelekeo na kinachojali kutatua shida za watu

> Ametoa wito kwa Watanzania kutoandamana kwa kisingizio cha kutokubali matokeo ya Uchaguzi

Soma https://jamii.app/MajaliwaRuvuma
#TZ2020
UTARATIBU WA KUPIGA KURA KWA MTU ASIYEWEZA KUSOMA, KUANDIKA NA ULEMAVU WA MACHO

- Ibara ya 54 ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi inamruhusu kufanya yafuatayo;-

- Kumchagua Mtu anayemwamini, tofauti na afisa wa #Uchaguzi kumsaidia kupiga kura

Soma > https://jamii.app/WalemavuMacho

#TZ2020
ZANZIBAR: MAALIM SEIF ATANGAZA KUPIGA KURA LEO BADALA YA KESHO

> Mgombea Urais #Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo amesema, uamuzi wake wa kupiga kura ya mapema leo unatokana na ZEC kushindwa kutoa takwimu za Wapiga kura ya mapema

Soma - https://jamii.app/SeifKuraLeo
#Uchaguzi2020
JE, WAJUA UNAWEZA KULALAMIKIA MWENENDO WA UPIGAJI KURA KATIKA KITUO?

> Ikiwa mpiga kura ambaye tayari amekwisha kupiga kura hajaridhishwa na mwenendo wa upigaji kura, anaweza kutoa malalamiko yake kwa Msimamizi wa Uchaguzi kwa kujaza Fomu namba 15

> Baada ya kupokea malalamiko yaliyojazwa katika Fomu namba 15, msimamizi wa uchaguzi anatakiwa kuyatafutia ufumbuzi, kisha kuonesha, katika fomu hiyo hiyo namba 15 ni kwa jinsi gani ameyatafutia ufumbuzi malalamiko ya mpiga kura

Soma > https://jamii.app/KulalamikiaKupigaKura

#Uchaguzi2020 #JamiiForums #JFLeo
SERIKALI YATOA RUHUSA KWA WATUMISHI KUSAFIRI KWENDA KUPIGA KURA

> Imetoa ruhusa ya siku 3 (Oktoba 27-29) kwa Watumishi wa Umma ambao wamejiandikisha kupiga kura kwenye maeneo tofauti na Vituo vyao vya Kazi ili washiriki kupiga kura

Soma - https://jamii.app/RuhusaKuraWatumishi
#TZ2020
ZANZIBAR: MAALIM SEIF AKAMATWA AKIWA KITUO CHA KUPIGIA KURA

> Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na ACT-Wazalendo, Mgombea Urais Zanzibar, Maalim Seif amekamatwa na Vyombo vya Dola wakati akiwa ktk Kituo cha Kupigia kura cha Garagara

Soma https://jamii.app/MaalimAkamatwa
#Uchaguzi2020
ZANZIBAR WAANZA KUPIGA KURA LEO

> Makundi Maalum yatakayoshiriki ni Watumishi wa ZEC, Wasimamizi wa Uchaguzi na Askari Watakaosimamia Uchaguzi

> Mwenyekiti wa ZEC amesema, kura za leo zitahifadhiwa, kulindwa na kujumlishwa na zitakazopigwa kesho

Soma - https://jamii.app/UchaguziZnz

#TZ2020
UMOJA WA MATAIFA WASISITIZA AMANI KATIKA UCHAGUZI MKUU

> Katibu Mkuu wa UN amehimiza Vyama na wafuasi wao kushiriki Uchaguzi kwa amani na kuepuka vurugu

> Mamlaka zimetakiwa kuandaa mazingira salama yatakayoruhusu wananchi kutimiza haki yao

Soma https://jamii.app/UNElectionsTZ
#TZ2020
TUME YA HAKI ZA BINADAMU YATOA TAMKO KUHUSU UCHAGUZI MKUU 2020

> Imetoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi na kutumia vyema #Haki yao ya Kikatiba ya kupiga kura

> Polisi waaswa kuzingatia Maadili, waheshimu #HakiZaBinadamu na waepuke matumizi makubwa ya nguvu

> Wagombea watakaoshindwa wanaombwa wakubali matokeo ili kudumisha Amani ya Nchi

Soma - https://jamii.app/TumeHakiUchg
#Uchaguzi2020
KAMATI YA MAADILI: TUMEKUWA WAKALI KUTOKANA NA AINA YA WAGOMBEA TULIONAO

> Katibu wa Kamati ya Maadili ya Taifa amesema wanalenga kuratibu na kuendesha Chaguzi zinazozingatia #Katiba na #sheria za Uchaguzi ambao ni shirikishi na wa uwazi

Soma - https://jamii.app/AdhabuKamatiUchg
#TZ2020
LISSU: WATANZANIA CHAGUENI VIONGOZI AMBAO SI WASAKA FEDHA

> Amesema baadhi ya Viongozi hawafikirii kutetea maslahi ya Wananchi, wanachoangalia ni kupata fedha

> Amewataka wananchi kutofanya makosa kwa kuchagua viongozi wa aina hiyo kesho

Soma https://jamii.app/LissuViongozi
#TZ2020
TEC WATAKA NEC IHESHIMIWE KWA KUWA NDIYO MRATIBU WA UCHAGUZI

> Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) limewataka Watanzania waiheshimu na kuisikiliza Tume ya Uchaguzi na waongozwe na dhamiri nyoofu kwa kufanya uamuzi sahihi kwa maslahi ya Taifa

Soma - https://jamii.app/TECAmaniUchaguzi
#TZ2020
IGP SIRRO: KUKAA NA KULINDA KURA NI DALILI YA KUFANYA FUJO

> Amesema, kwa mujibu wa Sheria, wanaolinda kura ni Mawakala ambao kila Chama kimepeleka

> Amewataka Wananchi kurudi nyumbani na kuendelea na shughuli zao baada ya kupiga kura

Soma https://jamii.app/KuraUchaguziIGP
#Uchaguzi2020
WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA EAC KUWEPO MIKOA 13

> Watakuwepo Dar, Tanga, Unguja, Pemba, Lindi, Mtwara, Dodoma, Mbeya, Kigoma, Singida, Kilimanjaro, Morogoro na Mwanza

> Baadhi ya madhumuni yao ni kuangalia Uchaguzi na kubaini changamoto

Soma - https://jamii.app/UchaguziWaangaliziEAC
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: MHAMASISHANE MKAPIGE KURA, UKIMALIZA RUDI NYUMBANI

> Amesema “Tarehe 28 tuitumie kujenga umoja wa #Tanzania. Tukapige kura, ukimaliza nenda nyumbani. Fujo hazijengi nchi, Tunataka amani kwasababu kuna maisha baada ya Uchaguzi"

Soma https://jamii.app/MagufuliAmaniTZ
#TZ2020
ZANZIBAR: TAKRIBAN WATU 42 WAKAMATWA KWA MADAI YA KUSHAMBULIA POLISI

> IGP Sirro amesema karibu watu 42 wamekamatwa wakidaiwa kushambulia Polisi waliokuwa wakisambaza masanduku ya kura

> Ameeleza kuwa, mpaka sasa hakuna taarifa ya vifo

Soma https://jamii.app/IGPZanzibar
#TZ2020
POLISI ZANZIBAR: TUMELAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI KTK BAADHI YA MAENEO

> Wamewakamata watu waliochoma matairi barabarani, waliokwenda vituo vya kupigia kura pasipo kuwa makundi maalum na walioyashambulia kwa mawe magari ya Polisi

Soma https://jamii.app/MabomuZbar
#Uchaguzi2020