JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RC KUNENGE AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA FUJO OKTOBA 28

> Mkuu wa Mkoa wa Dar amesema wamejipanga na amewahakikishia usalama Wapiga kura

> Awataka Wananchi wajitokeze bila wasiwasi kupiga kura kwa kuwa Polisi wamejiandaa kudhibiti vurugu

Tazama https://youtu.be/9uAzHABcDiM
#Uchaguzi2020
DAR: AHUKUMIWA MIAKA 2 JELA KWA KUMUUA MKEWE BILA KUKUSUDIA

> Yusuph Ismail (45) alimuua Magdalena Fabian kwa kumchapa fimbo na kumnyonga kwa madai ya kukosa uaminifu

> Wakati tukio linatokea Novemba 2013, wawili hao walikuwa wamelewa

Soma - https://jamii.app/HukumuMauaji
LISSU: VIONGOZI KAMA MAALIM SEIF HAWAZALIWI KILA SIKU

> Akiwa Pemba ktk Mkutano wa kufunga Kampeni za ACT- Wazalendo, amewakata Wazanzibari kumpa kura Maalim ili akamilishe ndoto ya Wazanzibari ya kuwa Taifa lililokuwa kabla ya Muungano

Soma - https://jamii.app/LissuPemba
#TZ2020
MAALIM SEIF: WALIMU WA MADRASA WATAINGIA KWENYE 'PAYROLL' YA SERIKALI

> Mgombea Urais #Zanzibar amesema, ni muhimu kwa Walimu wa Madrasa kuingia kwenye malipo ya Serikali kwasababu wanafanya kazi kubwa katika kuwaandaa watoto kiroho

Soma https://jamii.app/MaalimMadrassaWalimu
#Uchaguzi2020
JOSHUA NASSARI AOMBA RADHI KWA DKT. MAGUFULI

> Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nassari aomba radhi kwa machukizo aliyofanya alipokuwa upinzani

> Nassari alihamia CCM akitokea CHADEMA mwezi Julai 2020

Soma https://jamii.app/NassariVsMagufuli
#Uchaguzi2020
ZEC: MAKOSA KWENYE DAFTARI LA KUPIGA KURA YAMECHANGIWA NA WAPIGA KURA WENYEWE

> Ni kwasababu ya kushindwa kufanya uhakiki wa taarifa wakati zoezi hilo lilipofanyika

> ZEC itatoa msimamo kuhusu Wapiga Kura hao baada ya Kikao cha Uongozi

Soma - https://jamii.app/DaftariWapigaKura
#TZ2020
#CORONAVIRUS: KENYA YAREKODI VISA ZAIDI YA 1,000 NDANI YA SAA 24

> Maambukizi mapya 1,068 yamerekodiwa huku mgonjwa mdogo zaidi akiwa mtoto wa miezi 6

> Idadi ya visa imefikia 47,212, vifo 870 na wagonjwa waliopona hadi sasa ni 33,050

Soma - https://jamii.app/CovidKE
MMANGA: NITAVUNJA UONGOZI WA TFF NA KUINUA SOKA LA WANAWAKE

> Mgombea Urais kupitia Demokrasia Makini, Cecilia Mmanga amesema TFF ni chanzo cha Migogoro kwenye Mpira

> Pia, watafufua #Michezo mingine ikiwemo kufundisha Watoto Bao

Soma https://jamii.app/MmangaTFF
#Uchaguzi2020
SERIKALI YAKOPA TSH BILIONI 136.85 KUKARABATI VIWANJA VYA NDEGE

> Serikali imezindua mradi wa ukarabati na upanuzi wa Viwanja vya Shinyanga, Tabora, Sumbawanga na Kigoma ili viwe vya Kimataifa

> Mkopo umetolewa na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya

Soma https://jamii.app/MkopoNdege136b
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: WEZI SUGU 30 WAKAMATWA NA POLISI

> Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni limekamata wezi hao wakiwa na mali mbalimbali

> Watu wote waliopotelewa/kuibiwa na vitu wametakiwa kufika kituoni na risiti kubaini vitu hivyo kama ni vyao

Soma https://jamii.app/Wizi30Polisi

#JFLeo
PROF. LIPUMBA: TUTAJENGA UCHUMI WENYE USHINDANI KITAIFA NA KIMATAIFA

> Amesema, ukuaji wa uchumi unahitaji uongozi imara, utawala makini na mipango

> CUF itaweka misingi itakayohakikisha uchumi unakua kwa 8%–10% kila mwaka kwa miaka 10 ijayo

Soma https://jamii.app/LipumbaLindi
#TZ2020
AAFP: TUTAKUSANYA ILANI ZA VYAMA VYOTE NA KUUNDA SERIKALI YENYE SERA JUMUISHI

> Mgombea Urais, Seif Maalim Seif amesema dhana ya Chama kitakachoshinda kuchukua kila kitu ni kama ulaghai kwani Watanzania wamegawanyika katika nadharia tofauti

Soma https://jamii.app/SeifMaalimAAFP
#TZ2020
UMOJA WA ULAYA WAZUNGUMZA KUHUSU UCHAGUZI WA TANZANIA

> Umoja wa Ulaya (EU) umesisitiza Vyama vyote kuwajibika ktk kuweka mazingira ya Uwazi na Uchaguzi wa amani

> EU wanategemea hatua hii itajenga ushirikiano mkubwa kati yao na #Tanzania

Soma https://jamii.app/EUUchaguziTZ
#TZ2020
ADC: TUNALENGA KUMPA MTANZANIA MAISHA MAZURI

> Mgombea Urais, Queen Sendiga amesema Wakulima wategemee neema ndani ya Uongozi wa ADC

> Ameahidi kuboresha miundombinu akisema barabara zitatengenezwa kwa kiwango cha kupita nyakati zote

Soma - https://jamii.app/ADCBabati
#Uchaguzi2020
WAANGALIZI WA NDANI WA UCHAGUZI WALALAMIKIA UKOSEFU WA FEDHA

> Mkurugenzi wa Uchaguzi amewashauri Waangalizi kuwa na fedha badala ya kutegemea Wafadhili

> Asema, Serikali haijategemea Wafadhili ktk Uchaguzi huu unaogharimu Tsh. Bilioni 331

Soma https://jamii.app/WatazamajiHela
#TZ2020
SEIF MAALIM: WANANCHI WASISHAWISHIKE NA IDADI YA WATU KATIKA KAMPENI

> Amewataka wananchi kumpigia kura Mgombea mwenye nia ya dhati ya kutatua changamoto zao

> Amesema, Vyama vinavyopiga sana kelele havina ufumbuzi wa matatizo ya wananchi

Soma - https://jamii.app/SeifMaalimAAFP
#TZ2020
UPDATES: MAWAKALA WA CHADEMA WALIOFARIKI KWA AJALI WAFIKIA 6

> Mawakala 9 walipata ajali wakienda kuapishwa baada ya utaratibu kubadilika

> 3 walifariki palepale, 3 wamefariki wakitibiwa, 1 ameruhusiwa na 2 wanaendelea na matibabu

Soma - https://jamii.app/Ajali6Mawakala
#Uchaguzi2020
MWANZA: POLISI WACHUNGUZA KIFO CHA KATIBU KATA WA CCM ALIYEFARIKI BAADA YA KULA MAKANDE

> Deogratias Medard(42) alifariki muda mfupi baada ya kula Makande na Chai akiwa kwenye Kampeni za Mgombea Ubunge Sengerema (CCM), Hamis Tabasamu

Soma - https://jamii.app/KatibuCCMKata
#Uchaguzi2020
UPDP: ADHABU YA KUNYANYASA NA KUDHALILISHA WANAWAKE NI MIAKA 25 JELA

> Mgombea Urais, Twalib Kadege amesema Serikali yake itatoa adhabu hiyo bila huruma

> Chama hicho kimetoa kipaumbele na kuwasimamisha Wagombea Wanawake wengi

Soma - https://jamii.app/UPDPWanawake
#Uchaguzi2020