JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NEC YAONYA WAANGALIZI WA NDANI NA NJE KUINGILIA UCHAGUZI

> Mjumbe wa NEC, Balozi Omar Mapuri amewataka wazingatie Sheria, #Katiba na miongozo ya kufanya wajibu wao, na kuhakikisha hawaingilii mwenendo wa Uchaguzi au kusababisha vurugu

Soma - https://jamii.app/NECWaangalizi
#Uchaguzi2020
KADEGE: NITAANZISHA WIZARA YA MIKOPO NA KUWAPA HALI NZURI KIMAISHA

> Mgombea Urais kupitia UPDP amesema, ataanzisha Wizara ya Mikopo itakayowakopesha fedha Vijana na Wanawake

> Ataongeza kima cha chini cha Mshahara kufikia TSH. 400,000

Soma - https://jamii.app/KadegeUPDP
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: SIKUMFUKUZA GAMBO UKUU WA MKOA

> Amesema hakumfukuza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwenye nafasi hiyo

> Ameeleza, kama angemfukuza asingelipitisha jina la Gambo ili awe Mgombea wa ubunge Jimbo la Arusha Mjini

Soma https://jamii.app/ArushaMjiniJPM
#TZ2020
SAFARI ZA BOTI NA MELI KUSITISHWA SIKU YA UCHAGUZI

> Mamlaka ya Usafiri wa Baharini #Zanzibar(ZMA) imetangaza kusitisha safari zote za Boti na Meli za abiria na mizigo Jumatano ijayo, Oktoba 28, 2020 ili kutoa fursa kwa Wananchi kupiga kura

Soma https://jamii.app/SafariOktoba28
#TZ2020
KADEGE: UPDP ITATOA RUZUKU ZA UCHAGUZI HATA VYAMA VISIVYO NA WABUNGE

> Mgombea Urais wa Chama hicho amesema Ruzuku ya Uchaguzi ni keki ya Taifa, kila Chama lazima kipate

> Wasio na Wabunge watapata ruzuku ili waweze kuzunguka kuomba kura

Soma - https://jamii.app/UPDPRuzukuUchaguzi
#TZ2020
MBOWE: KUNA MAMILIONI YA WAPIGA KURA HEWA NA MAELFU YA VITUO BANDIA

> Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amedai kuna uvurugwaji mkubwa wa Daftari la Wapiga kura

> Ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa maelezo na suluhisho haraka

Soma https://jamii.app/MboweUchaguzi
#Uchaguzi2020
#NIGERIA: MITIHANI YA SHULE ZA SEKONDARI YAHAIRISHWA KUTOKANA NA GHASIA

> Pia, Baraza la Taifa la Mitihani(NECO) limefikia uamuzi huo baada ya baadhi ya Majimbo kuweka amri ya kutotoka nje

> Waandamanaji wanaendelea kupinga ukatili wa Polisi

Soma https://jamii.app/EndSARSNigeria
DPP: YEYOTE ATAKAYEVURUGA AMANI ATASHUGULIKIWA

> Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga amesema jukumu la amani ni la kila Mwananchi

> Taratibu na Sheria zinatakiwa kufuatwa ili kupata Haki, amani na usalama, na Taifa liweze kupata maendeleo

Soma https://jamii.app/DPPAmaniTZ
IVORY COAST: UPINZANI WAKATAA MABADILIKO YA TUME YA UCHAGUZI

> Vyama vya Upinzani vimesema vitaendelea kuasi dhidi ya utekelezaji wa #Sheria ya kumruhusu Rais Alassane kugombea kwa awamu ya 3

> Wamezitaka Taasisi za Kimataifa kuingilia kati

Soma https://jamii.app/ProtestsInIvoryCoast
KAMATI YA AMANI YAOMBA MFUNGO WA SIKU TATU KUOMBEA UCHAGUZI WA AMANI

> Pia, imewataka wazazi na walezi kuwaasa vijana kujiepusha kushawishiwa na wanaoitakia mabaya Tanzania

> Wamesisitiza kuviacha Vyombo ya Uchaguzi vifanye kazi yake

Soma https://jamii.app/KuombeaUchaguzi
#TZ2020
LISSU: MIMI SIO WA KWANZA KUWA NA WAKILI MWINGEREZA

> Tundu Lissu amesema hata Mwl. Nyerere aliwahi kumtumia Wakili kutoka Uingereza

> Amesema hayo alipoulizwa kuhusu kujihusisha na Mataifa ya nje kwani hata Wakili wake ni raia wa Kigeni

Soma https://jamii.app/WakiliMuingereza
#TZ2020
ACT-WAZALENDO WAANDIKA BARUA KWA MSAJILI KUHUSU KUKOMA KIKATIBA KWA UANACHAMA WA ZITTO NA MAALIM

> Wanachama wamesema Maalim Seif na Zitto wamekosa sifa. Katiba yao Ibara ya 13(4) inasema mwanachama atapoteza sifa akiunga mkono chama kingine

Soma https://jamii.app/ZittoVsMaalim
#TZ2020
NEC: MADAI YA UWEPO WA VITUO HEWA NI UZUSHI

> NEC imesema imebaini watu wakiwemo Viongozi wa Vyama vya Siasa ambao wamejipanga kuharibu taswira ya Uchaguzi

> Imetoa onyo ikisema haitosita kuwachukulia hatua kwasababu wanafanya uchochezi

Soma - https://jamii.app/NECViongoziUzushi

#TZ2020
ARUSHA: ADC YAAHIDI KUJENGA CHUMBA CHA KUHIFADHI MAITI NA SOKO

> Queen Sendiga ameahidi kujenga Chumba cha Kuhifadhi maiti ktk Hospitali ya Arumeru endapo atachaguliwa kuwa Rais

> Ameahidi kujenga soko jipya ndani ya miezi 3 ya mwanzo

Soma https://jamii.app/ADCAhadiArumeru
#Uchaguzi2020
MAALIM SEIF: ACT WAZALENDO ITAJALI MAKUNDI MAALUM

> Mgombea Urais Zanzibar, Maalim Seif amesema watahakikisha kuna usawa wa kijinsia kwenye ajira

> Walemavu watawekewa mazingira rafiki, Serikali itawalipia Wazee nauli za daladala

Soma https://jamii.app/MakundiMaalum
#Uchaguzi2020
LISSU: NI KWELI NINA TIKETI YA KWENDA UBELGIJI

> Mgombea Urais wa JMT (CHADEMA), Tundu Lissu amesema atakwenda Ubelgiji Desemba 18 ili akaonane na Daktari wake Desemba 20, 2020

> Amesema hayo akijibu hoja ya Dkt. Magufuli kuwa kuna baadhi ya wagombea wana tiketi za kuondoka Nchini baada ya kusababisha fujo

Soma https://jamii.app/LissuTiketiNdege
#TZ2020
RC CHALAMILA: TUMEJIPANGA KUKABILIANA NA VIJANA WALIOANDALIWA KUFANYA VURUGU

> Amedai wanazo taarifa za Vijana 150 kuandaliwa kila Kata na Upinzani

> Amewataka wananchi kupiga kura na kutobaki Vituoni kwani kulinda kura si jukumu lao

Soma - https://jamii.app/UchaguziMby
#TZ2020
LISSU: JARIBIO LOLOTE LA KUVURUGA UCHAGUZI LITASABABISHA WATU WAPELEKWE 'THE HAGUE'

> Asema kuna uchunguzi unaendelea na ipo orodha ya watu wanaoangaliwa

> Yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi anajiingiza ktk orodha hiyo

Soma https://jamii.app/LissuUchaguzi
#TZ2020