JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DKT. MWINYI: MUUNGANO HAUIUMIZI #ZANZIBAR BALI UNAINUFAISHA

> Mgombea Urais Zanzibar kupitia CCM amesema, Muungano unawafanya Wazanzibari kunufaika kibiashara na kiusalama

> Pia, Wazanzibari wanaitegemea #Tanzania Bara ili kupata mazao mengi

Soma https://jamii.app/ZnzDktMwinyi
#TZ2020
LISSU: MAGUFULI ALIINGIA KWA KURA, ATAONDOKA KWA KURA

> Mgombea Urais kupitia CHADEMA amesema, ifikapo Oktoba 28 wananchi wapige kura kufuta machozi ya miaka 5

> Amesema Maandiko Matakatifu yanasema #Haki huinua Taifa, sio pesa wala barabara

Soma https://jamii.app/LissuHai
#TZ2020
THAILAND: WANANCHI WAANDAMANA KUPINGA UTAWALA WA KIFALME

> Raia wa #Thailand wameandamana kumshinikiza Waziri Mkuu, Prayuth Chan-ocha kujiuzulu na kuukomesha Mfumo wa Kifalme

> Pia, wanadai kuachiliwa kwa waliokamatwa kwasababu za Kisiasa

Soma https://jamii.app/ThailandMaandamano
QUEEN SENDIGA: KAMA KUNA KERO, TUMALIZE HASIRA KWENYE SANDUKU LA KURA

> Mgombea huyo Urais kupitia ADC, amewataka Wananchi kuacha kuingia kwenye ushawishi wa kuchafua Amani na badala yake wenye kero wakamalize hasira kwenye Sanduku la Kura

Tazama https://www.youtube.com/watch?v=DDFNDcdlVAs&feature=youtu.be
#TZ2020
ASKOFU GWAJIMA: NINA JINA LA KIISLAM, NINAITWA RASHID

> Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe(CCM) amesema alipata jina hilo baada ya kutelekezwa Msikitini

> Suala hilo lilimpa sababu ya kuusaidia Uislamu ikiwemo kujenga Visima vya Maji Dar

Tazama https://youtu.be/ieu6HWyR910
#Uchaguzi2020
DKT. BASHIRU: WAGOMBEA WA CCM KUTOENGULIWA NI SUALA LA KUTII SHERIA

> Amesema wana vitengo vya Sheria ambavyo haviruhusu Wagombea kujaza fomu bila kuhakikiwa

> Amesema, kwao suala la kukosea haliwezekani kwasababu CCM ni Chama cha Kitaasisi

Soma https://jamii.app/CCMWagombeaSheria
#TZ2020
ARGENTINA: VISA VYA #CORONAVIRUS VYAFIKIA MILIONI 1

> #Argentina imerekodi visa 1,002,662, ikiwa ni nchi ndogo zaidi kurekodi visa zaidi ya Milioni 1

> Inakuwa nchi ya tano kuathirika zaidi duniani nyuma ya Marekani, India, Brazil na Urusi

Soma - https://jamii.app/COVID-Arg
QUALITY GROUP LIMITED YAAMRIWA KUWALIPA TSH. MILIONI 232 WAANDISHI WAKE

> Mahakama ya Mwanzo ya Migogoro ya Kazi imeamuru Kampuni inayomilikiwa na Yusufu Manji, kuwalipa waliokuwa Waandishi wake kwa kuvunja Mikataba nao bila sababu maalumu

Soma https://jamii.app/ManjiWaandishi
#JFLeo
#NIGERIA: SHULE ZA LAGOS ZAFUNGWA KUTOKANA NA MAANDAMANO

> Kamishna wa Elimu Mjini humo amesema hakuna uhakika wa usalama kwa Wanafunzi na Watumishi

> Maandamano ya kupinga ukatili wa Polisi yanaendelea maeneo mbalimbali nchini humo

Soma - https://jamii.app/SchoolClosureNGR
MOROGORO: MBARONI KWA KUCHANA MABANGO YA WAGOMBEA WA CCM

>Isihaka Exavery (20) anashikiliwa kwa tuhuma za kuchana picha za Mgombea Urais, Dkt. Magufuli na za Mgombea Udiwani, Seif Zahoro Chomoka

> Upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani

Soma https://jamii.app/MoroPichaMagufuli
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: JINA LANGU LIPO NAMBA MOJA, USIHANGAIKE KUANGALIA KWINGINE

> Amewaambia Wananchi wasihangaike kuangalia kwingine kwasababu wale hawawahusu

> Asema, Uchaguzi ni wakati wa kuamua kama wanataka maendeleo au 'blah blah'

Soma - https://jamii.app/JPMKorogwe
#Uchaguzi2020
MAALIM SEIF: TULIKUBALIANA KUMUUNGA MKONO LISSU NA MEMBE AKIWEPO

> Baada ya kuona Kampeni zao zinasuasua, Kamati ya Uongozi ilikutana na Bernard Membe akiwepo

> Membe alitoa tarehe akisema ikifika hajaanza kampeni, ni bora kumuunga Lissu

Soma - https://jamii.app/MaalimMembeLissu
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: NI WAKATI WA KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI

> Amesema "Miaka 5 iliyopita tumeimarisha uchumi, sasa 5 ijayo tutakuwa na jukumu la kuongeza mishahara. Huwezi kupandisha mishahara wakati huna uchumi, wengine wanazungumza tu"

Soma https://jamii.app/MaslahiWafanyakazi
#TZ2020
MAALIM SEIF: WAZANZIBARI WAMECHOKA, WAMEDHAMIRIA KULINDA DEMOKRASIA

> Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo amesema wanakwenda tarehe 27 na 28 wakiwa tayari kwa lolote litakalotokea kulinda #Demokrasia na #Haki ya watu kumchagua Rais wanayemtaka

Soma - https://jamii.app/MaalimHakiZnz
#TZ2020
TUME YA UCHAGUZI: KILA MPIGA KURA ARUDI NYUMBANI BAADA YA ZOEZI HILO

> Ofisa Elimu Kitengo cha Mpiga Kura, amesema hakuna mtu atakayeruhusiwa kukaa Mita 100 kusubiri matokeo

> Amesema ni kosa kukiuka utaratibu uliowekwa siku ya kupiga kura

Soma https://jamii.app/KuraMita100
#TZ2020
NEC YAIFUTA ADHABU YA MBATIA KUFUNGIWA KUFANYA KAMPENI

> Mgombea Ubunge wa Vunjo, James Mbatia alizuiliwa kufanya Kampeni kwa siku 7 mpaka Oktoba 23 kwa kutumia kipeperushi cha Kampeni ambacho hakijaidhinishwa na Msimamizi wa Uchaguzi

Soma https://jamii.app/MbatiaAdhabu
#Uchaguzi2020
MGOMBEA URAIS WA UPDP AAHIDI KUTOA HUDUMA ZA AFYA BURE

> Twalib Kadege amesema #Tanzania ina Rasilimali nyingi kama Madini na Hifadhi za Taifa na Serikali inapaswa kukusanya fedha kwenye vyanzo hivyo ili itekeleze sera ya Matibabu bure

Soma https://jamii.app/UPDPHudumaBure
#Uchaguzi2020
NEC: MSIMAMIZI ATAKAYESABABISHA UCHAGUZI KURUDIWA ATALIPA FIDIA

> NEC itamchukulia hatua Msimamizi atakayefanya vitendo vitakavyosababisha Uchaguzi kuharibika ktk Jimbo au Kata kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Soma https://jamii.app/UchaguziJimbo
#Uchaguzi2020
TAKUKURU: NI MARUFUKU WAPIGA KURA KULA PILAU KWA WAGOMBEA WATAKAOSHINDA

> Mkuu wa TAKUKURU Geita amesema kitendo hicho ni kupokea rushwa ya vyakula

> Pia, aliyeshinda hawezi kuleta maendeleo kwasababu amemalizana na Wananchi kwenye Pilau

Soma - https://jamii.app/TAKUKURUPilauRushwa
#TZ2020
PROF. LIPUMBA: NITABORESHA BEI YA KOROSHO

> Mgombea Urais JMT kupitia CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ameahidi kuboresha sekta muhimu za #Uchumi na #Kilimo

> Asema maendeleo ya Viwanda hutanguliwa au kuambatana na Mapinduzi ya Kilimo

Soma https://jamii.app/LipumbaKorosho
#Uchaguzi2020