JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KILIMANJARO: BWENI LA SHULE YA SEKONDARI YA UCHIRA ISLAMIC LATEKETEA KWA MOTO

> Bweni la Shule hiyo ya Wasichana iliyopo Moshi Vijijini limeteketea jioni ya Oktoba 16

> Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, hakuna kifo kilichoripotiwa

Soma - https://jamii.app/UchiraMoto
#JFLeo
WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU KUWASILI OKTOBA 23

> Waangalizi hao kutoka Jumuiya ya #Afrika Mashariki wataongozwa na Rais Mstaafu wa #Burundi, Sylvestre Ntibantunganya

> Wamo Wabunge wa Bunge la #EAC na Mawaziri wa masuala ya Jumuiya hiyo

Soma - https://jamii.app/WaangaliziEAC
#TZ2020
LIGI KUU ENGLAND: LIVERPOOL NA EVERTON ZATOSHANA NGUVU

- Mchezo wa β€˜Merseyside Derby’ wa mzunguko wa 5 wa Ligi Kuu England kati ya Liverpool na Everton umemalizika kwa timu hizo kufungana goli 2-2

- Mechi inayofuata sasa ni kati ya Chelsea na Southampton na baadaye, Manchester City na Arsenal zitapimana ubavu kabla ya Manchester United kukipiga na Newcastle

#Michezo #Sports #JamiiForums #JFSports #JFMichezo
TUNDU LISSU AWATAKA WATANZANIA KUHAMASISHANA ILI KWENDA KUPIGA KURA

> Mgombea Urais kupitia CHADEMA amesema Uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu kuliko wakati wowote kwa sababu utaunda Serikali itakayolinda Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu

Soma - https://jamii.app/LissuManyoni
#Uchaguzi2020
LIGI KUU ENGLAND: CHELSEA YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI

- Klabu ya Chelsea imetoka sare ya goli 3-3 na Klabu ya Southampton katika mchezo wa Ligi hiyo mzunguko wa 5

- Mchezo unaofuata ni kati ya Manchester City na Arsenal na kisha Manchester United itapambana na Newcastle

#JamiiForums #JFSports #JFMichezo #Michezo #Sports
NEC: WAANGALIZI WA UCHAGUZI WASIWE WASEMAJI WA UCHAGUZI

> Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema, Waangalizi wa Uchaguzi wajibu wao ni kutazama tu namna shughuli zinavyoendeshwa ili kupata fursa ya kuandaa ripoti na kutoa mapendekezo

Soma https://jamii.app/JukumuWaangalizi
#Uchaguzi2020
WATOTO KUTOKWA NA HAJA KUBWA BILA KUJIJUA NI TATIZO KATIKA UTUMBO MPANA

> Kitaalamu Ugonjwa huo unaitwa Hirschsprung’s Disease, na unawakabili watoto wengi

> Ni Ugonjwa unaochukuliwa kama tabia, lakini ni tatizo lililo nje ya uwezo wa mtoto

Soma https://jamii.app/UgonjwaKujinyea
#JFAfya
TCRA: WANAWAKE HUDHALILISHWA SANA MITANDAONI KUTOKANA NA KUPIGA PICHA TATA

> Kwa mujibu wa kesi wanazozipokea, waathirika hubainika walihusika kuchapisha maudhui hayo ya ngono

> Suala hilo linachangiwa na ugawaji wa nywila kwa watu wa karibu

Soma https://jamii.app/SocialMediaBullying
RIPOTI: WATUMIAJI WA INTANETI TANZANIA WAFIKIA MILIONI 27.1

> Kwa mujibu wa takwimu mpya za TCRA, Watumiaji wamefikia idadi hiyo Juni kutoka Milioni 26.8 ya mwezi Machi

> Hii inaashiria ongezeko la fursa mtandaoni kama biashara na maarifa

Soma - https://jamii.app/WatumiajiIntaneti
#JFLeo
KAGERA: MBARONI KWA KUUA AKIJARIBU KUTOA MIMBA

> Frodius Protace (24) anatuhumiwa kumuua Saraiya Idd (25) kwa kujaribu kumtoa mimba ya miezi sita

> Mtuhumiwa alikiri kushiriki mafunzo ya kozi fupi ya Ufamasia lakini hajawahi kuajiriwa

Soma https://jamii.app/TuhumaZaKuua
RAIS MAGUFULI AMKABIDHI NYUMBA MZEE MWINYI
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli amemkabidhi nyumba Rais Mstaafu, Ally Hassan Mwinyi
-
Mzee Mwinyi amekuwa akiishi kwenye nyumba aliyojenga mwenyewe iliyoko Mikocheni jijini Dar, nyumba ambayo ipo karibu na Nyumba ya Mwalimu Nyerere
-
Ally Hassan Mwinyi ni Rais wa Pili wa Tanzania, aliyeongoza tangu mwaka 1985 hadi mwaka 1995
-
#JFLeo #JamiiForums #JFSiasa
KENYA YASHUKU KUPIGWA NA WIMBI LA PILI LA #CORONAVIRUS

> Kenya imethibitisha watu 685 kuambukizwa #CoronaVirus ndani ya saa 24

> Jumla ya walioambukizwa ni 44,881 huku 28 wakiwa mahututi. Wizara imetahadharisha wananchi kufuata kanuni

Soma https://jamii.app/SecondWaveKE
#JFLeo
MAJALIWA: MCHAGUENI DKT. MAGUFULI KWANI SIO MLALAMISHI

> Amesema, Wananchi wanatakiwa kumchagua mgombea huyo kwa kuwa ana uwezo wa kusimamia kazi ipasavyo

> Amewataka wananchi kutofanya makosa kwa kuchagua wagombea wasioweza kuwatumikia

Soma - https://jamii.app/MajaliwaKigoma
#TZ2020
ZANZIBAR: AAFP YAAHIDI KUWATOLEA MAHARI VIJANA

> Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya AAFP, Said Soud Said amesema atahakikisha vijana wanaoa na mahari itatolewa na Serikali

> Amesema hatua hiyo itapunguza tabia ya ubakaji

Tazama https://youtu.be/khS5kPLW2AA
#Uchaguzi2020
PROF. LIPUMBA: NITATEUA MA-DC WATAKAOSIMAMIA MAENDELEO YA WANANCHI, SIO WANASIASA

> Endapo atachaguliwa, Mgombea huyo wa Urais kupitia CUF amesema atahakikisha Wakuu wa Wilaya wanapoteuliwa wanakuwa na vigezo vyote vya Utumishi wa Serikali

Soma https://jamii.app/LipumbaUteuziDCs
#TZ2020
JE, SHERIA YA UCHAGUZI INASEMA NINI KUHUSU MGOMBEA KUFARIKI?

> Endapo Msimamizi wa Uchaguzi atajiridhisha kuwa Mgombea amefariki kabla ya muda wa mwisho wa upigaji kura, basi atasitisha Uchaguzi katika Jimbo

Zaidi, soma > https://jamii.app/MgombeaKufariki

#Uchaguzi2020 #TZ2020
DKT. BENHAJJ: ELIMU YA UENDESHAJI WA MASHAURI YA UCHAGUZI ILETE MABADILIKO CHANYA

> Jaji wa Mahakama Kuu amesema, Wananchi wanaamini Mahakamani ni mahali pa kupata #Haki

> Amewaomba Watendaji kufanya kazi kwa kuzingatia mwongozo wa #Sheria

Soma https://jamii.app/ElimuUchaguzi
#TZ2020
DKT. KALEMANI: TANESCO HAKIKISHENI UMEME HAUKATIKI WAKATI WOTE WA UCHAGUZI

> Amewataka Mameneja wa TANESCO kuhakikisha umeme haukatiki

> Amesisitiza zaidi usikatike Oktoba 28, kwasababu wanataka wananchi wapige kura kwa uhuru na uhakika

Soma - https://jamii.app/UmemeUchaguzi
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: WANAOTAKA MUANDAMANE WAMESHAKATA TIKETI ZA KWENDA ULAYA

> Amesema "Vijana msidanganywe na vitu vya bure vya kuambiwa mjipange barabarani. Usijiangalie wewe tu, mwangalie mdogo/mama yako kama ataweza kukimbia kama wewe"

Soma - https://jamii.app/JPMBagamoyo
#Uchaguzi2020
CECILIA MWANGA: KATIKA UONGOZI WANGU SITAWAACHA SALAMA WABAKAJI

> Mgombea Urais kupitia Demokrasia Makini amesema, atahakikisha watuhumiwa wa ubakaji na ulawiti wanapewa adhabu kali kwasababu vitendo hivyo vinasababisha mmomonyoko wa Maadili

Soma https://jamii.app/CeciliaKampeniPwani
#TZ2020