JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
NEC YATAKA VYAMA VYA SIASA KUZINGATIA MAADILI YA UCHAGUZI
-
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka Vyama vya Siasa na Wagombea kuendelea kufuata Maadili ya Uchaguzi na kunadi Sera kwa kufuata utaratibu wa ratiba ambayo imepangwa
-
Pia, Vyama vya Siasa vimetakiwa kukwepa maneno ya uchochezi, kukwepa kuhamasisha watu kufanya vurugu, badala yake vihamasishe watu kwa amani kwenda kupiga kura
-
NEC imesisitiza kwamba Sheria za nchi zipo na zinapaswa kuendelea kufuatwa

#JFLeo #JamiiForums #Uchaguzi2020 #TZ2020
ASKOFU SHOO: VIONGOZI WA DINI KUEGEMEA CHAMA KIMOJA CHA SIASA KUNAWAGAWA WANANCHI

> Kiongozi wa Kanisa la KKKT amesema, "Maandiko yanaelekeza namna ya kusimama na kama kuna mahali pa kukemea kutokana na ukiukwaji wowote, fanya bila ubaguzi”

Soma - https://jamii.app/ViongoziDiniSiasa
#TZ2020
SAMIA SULUHU: HATA UKIPIGIA KURA KWINGINE, CCM ITAUNDA SERIKALI

> Amesema kupigia kura Chama kingine ni sawa na kuweka sukari Ziwa Victoria

> Amewaambia wananchi wakifanya hivyo, hawatakuwa sehemu ya maendeleo yatakayoletwa na CCM

Soma - https://jamii.app/SamiaChunya
#Uchaguzi2020
TUNDU LISSU: NITAONGOZA NCHI KWA KUFUATA KATIBA MPYA ITAKAYOPATIKANA

> Mgombea Urais kupitia CHADEMA amesema, Nchi inahitaji #KatibaMpya ili kurudisha Mamlaka kwa Wananchi kujichagulia Viongozi kwenye maeneo yao na kuwawajibisha wanapokosea

Soma https://jamii.app/LissuSimiyu
#TZ2020
SHINYANGA: VIJANA 2 MBARONI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 6

> Jeshi la Polisi linawashikilia vijana 2 wenye umri chini ya miaka 18 kwa tuhuma za kumbaka mtoto kwa zamu baada ya kumlaghai kuwa watamnunulia pipi pamoja na kumpatia hela

Soma - https://jamii.app/VijanaKubakaMtoto
SERIKALI YAHIMIZA WAANDISHI KUSHIRIKI MASHINDANO YA SADC KWA WAANDISHI WA HABARI 2021

> Mashindano hayo yanahusisha washiriki kutoka nchi zote wanachama wa SADC

> Yatakuwa katika makundi manne ambayo ni Picha, Uchapishaji, Runinga na Radio

Soma - https://jamii.app/MashindanoSADC
NEC: VYAMA VIWASILISHE ORODHA YA MAWAKALA SIKU SABA KABLA YA UCHAGUZI

> Pia, imevikumbusha Vyama kuwa, Mawakala ambao vyama vyao havitawapangia vituo hawataapishwa

> NEC imesema kuwa, hakutakuwa na uchelewaji wa vifaa ktk vituo

Soma https://jamii.app/UchaguziMawakala
#TZ2020
WAUGUZI WATAKIWA KUACHA KUTUMIA LUGHA CHAFU KWA WAGONJWA

> Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga amesema, kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wauguzi na Wakunga kutoa maneno yasiyofaa kwa wagonjwa jambo linaloharibu taswira ya Sekta ya Afya

Soma - https://jamii.app/LughaChafuWauguzi
WHO: AFRIKA HAIWEZI KUHIMILI WIMBI LA PILI LA #CORONAVIRUS

> Shirika la Afya Duniani limesema mlipuko huo hautaweza kudhibitiwa kama mataifa barani Afrika hayatachukua tahadhari

> Wimbi la pili la #COVID19 litakuwa na athari kubwa kiuchumi

Soma - https://jamii.app/CoronaAfrica
PROF. LIPUMBA: SITISHIKI NA WATU KUJAA KWENYE MIKUTANO YA WAGOMBEA WENGINE

> Mgombea Urais (CUF) amesema anachokifanya yeye ni kwenda Vijijini ambako kuna changamoto kubwa za wananchi na sio kukusanya watu na kuwapeleka kwenye mikutano

Soma https://jamii.app/LipumbaMikutano
#Uchaguzi2020
SIKU YA CHAKULA DUNIANI: KILA BAADA YA SEKUNDE 5 MTOTO 1 HUFARIKI KWA NJAA

> Watu Milioni 690 wanakabiliwa na njaa, ikiwa ni ongezeko la watu Milioni 10 tangu 2019

> Chakula kilichoharibiwa duniani kila mwaka kinaweza kulisha watu Bilioni 2

Soma https://jamii.app/WorldFoodDay
#JFLeo
DR CONGO: WATU MILIONI 22 WANAKABILIWA NA UKOSEFU WA CHAKULA

> Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo limesema vita, migogoro inayosababishwa na vikundi vyenye silaha na #COVID19 ni kati ya sababu zilizopelekea ukosefu wa chakula

Soma - https://jamii.app/DRC22Million
#JFLeo
NJIA ZA KUHAKIKISHA WATOTO NJITI WANAWEKWA KWENYE MAZINGIRA BORA

> Moja ya njia ni kuhakikisha ngozi ya Mtoto inakuwa imegusana na ngozi ya Mama yake(Kangaroo Mother Care)

> Njia nyingine ni kuwaweka Watoto ktk mashine maalum

Soma https://jamii.app/MatunzoWatotoNjiti

#WatotoNjiti #PrematureBabies
DAR: AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 5 KWA KUKEKETA WATOTO WAKE

> Mahakama imemtia hatiani Cosmas Chacha kwa makosa 3. Mbali na kifungo, pia atalipa faini ya Milioni 3

> Desemba 2018, Mtuhumiwa aliwakeketa watoto wake 3 walio chini ya miaka 18

Soma https://jamii.app/Jela5KwaUkeketaji
#JFLeo
UGANDA: WAFUASI 132 WA BOBI WINE KUFIKISHWA MAHAKAMA YA KIJESHI

> Wafuasi hao wa Chama cha NUP waliokamatwa siku 2 zilizopita watafikishwa katika Mahakama ya Kijeshi kujibu mashtaka ya kupatikana na vitu vinavyodaiwa kuwa sare za Jeshi

Soma - https://jamii.app/BobiWineSupporters
#JFLeo
ZITTO KABWE: NITAMPIGIA KURA LISSU KUWA RAIS WA TANZANIA

- Amewaomba Wana-ACT katika Kata au Jimbo ambapo ACT wana Wagombea, wawapigie Kura wagombea hao

- Ambapo hakuna Wagombea wa ACT wanachama wampigie kura Mgombea wa Upinzani mwenye nguvu

Soma https://jamii.app/ZittoKuraLissu
#TZ2020
MGOMBEA URAIS WA ADC ADAI KUPIGWA MAKOFI NA KUVUNJIWA KIOO CHA GARI

> Queen Sendiga amedai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake la matangazo akiwa Stendi ya zamani ya Manispaa ya Iringa akiendelea na Kampeni

Soma - https://jamii.app/MakofiMgombeaADC
#TZ2020
JAMES MBATIA ASIMAMISHWA KUFANYA KAMPENI KWA SIKU 7

- Kamati ya Maadili imemsimamisha Mgombea huyo wa Ubunge wa Vunjo kupitia NCCR Mageuzi kufanya kampeni kuanzia Oktoba 17, 2020

- Ni kwa kutumia kipeperushi cha kampeni ambacho hakijaidhinishwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Vunjo

Soma https://jamii.app/MbatiaAsimamishwaKampeni

#Uchaguzi2020
TANAPA: MOTO MLIMA KILIMANJARO UMEDHIBITIWA

> Ukaguzi wa anga umebaini moto wote umedhibitiwa. Hata hivyo vikosi vya askari vimetawanywa kwa tahadhari

> Moto ulizuka Oktoba 11 na kuathiri 5% ya eneo lote la hifadhi lenye km za mraba 1700

Soma https://jamii.app/TANAPAMotoKLM
#JFLeo
LISSU: NIKISHINDWA KWA HAKI NITAKIRI KUSHINDWA

> Mgombea Urais kupitia CHADEMA amesema wakishinda lazima NEC itangaze kwa heri au kwa shari

> Amesisitiza wanataka Uchaguzi wa amani lakini hawatakuwa tayari kugeuza shavu la pili waumie zaidi

Soma https://jamii.app/LissuHakiUchaguzi
#TZ2020