JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: WATOTO WOTE WA KIKE WATAKIWA KURUDI SHULENI HATA WENYE MIMBA

> Makamishna wa Kaunti wametakiwa kuchunguza Wanafunzi walioshindwa kuripoti Shuleni na kuwarudisha

> Wenye Mitihani ya Taifa watafanya bila kujali ni Wajawazito au La!

Soma - https://jamii.app/PregnantSchoolResume
DAR: SOKO LA MAHAKAMA YA NDIZI LATHIBITISHWA KUMILIKIWA NA WANANCHI

> Akifanya Kampeni Mburahati, Dkt. Magufuli amesema Soko hilo litakuwa chini ya wananchi

> Ni baada ya Mgombea Ubunge wa Ubungo (CCM), Prof. Mkumbo kuomba soko kurasimishwa

Soma https://jamii.app/MabiboSokoWananchi
#JFLeo
ZANZIBAR: CHAUMMA YATANGAZA KUMUUNGA MKONO MAALIM SEIF

> Mgombea Urais wa CHAUMMA, Ali Juma amewataka Wanachama kumpigia kura Maalim Seif

> Amesema Vyama hivyo vina ushirikiano wa kindugu katika historia ya siasa za #Zanzibar na #Tanzania

Soma https://jamii.app/UraisCHAUMMA

#TZ2020
UDP YASEMA HAITAKUWA NA MIKUTANO YA HADHARA

> Naibu Katibu Mkuu, Juma Khamis Faki amesema kutokana na ukata, Chama hicho kitatangaza Sera zake nyumba kwa nyumba

> UDP imesema ni njia rahisi kuwafikia walengwa katika kuwaomba kura

Soma - https://jamii.app/KampeniUDP

#Uchaguzi2020
PROF. LIPUMBA: HUWEZI KUWA NA UCHUMI MZURI BILA MFUMO MZURI WA FEDHA

> Mgombea Urais kupitia CUF amesema β€œHali ya upatikanaji wa fedha ni ngumu na baadhi ya biashara zinafungwa

> Ameahidi kufufua viwanda na kuongeza ujazo wa fedha

Soma - https://jamii.app/LipumbaMfumoFedha
#Uchaguzi2020
TLP: TUNAENDELEA KUMUUNGA MKONO MGOMBEA URAIS WA CCM

> Makamu M/kiti wa TLP, Domina Rwechungura amesema β€œSisi tulishasema tangu mwezi wa 5 tutamuunga mkono Rais Magufuli, hivyo Msajili kauli yake kwamba tumesitisha uamuzi wetu hatuitambui”

Soma - https://jamii.app/TLPMagufuli2020
#TZ2020
MADHARA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA DAR ES SALAAM
-
Hali ilivyo katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam baada ya mvua kuendelea kunyesha tangu asubuhi ya leo
-
Ni muhimu kuchukua tahadhari

Tazama https://youtu.be/w64m0ECpuSA
LISSU: UCHAGUZI HAUTAKUWA RAHISI, KURA HII NI YA UKOMBOZI WA NCHI

> Mgombea Urais (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kwa miaka 5 baadhi ya Wananchi wamepitia changamoto mbalimbali na Oktoba 28 ndiyo wakati wa Ukombozi kwa Watanzania

Soma - https://jamii.app/LissuUkomboziNchi
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI: HATUKUNUFAIKA NA MADINI KUTOKANA NA UDHIBITI MBOVU

> Rais Magufuli amesema udhibiti mdogo katika usafirishaji wa madini ghafi, wizi na utoroshaji wa madini ulifanya Tanzania isifaidike na madini

> Amesema Serikali ya awamu ya tano ilichukua hatua kudhibiti hayo ikiwemo kusitisha usafirishaji wa mchanga

Soma https://jamii.app/SerikaliGawio
#CORONAVIRUS: WAKENYA WAKASIRISHWA NA TUKIO LA WANAFUNZI KUPULIZIWA DAWA

> Wanafunzi wamepuliziwa dawa kama njia ya kuepuka Virusi hivyo baada ya kufungua Shule

> Shirika la Afya (WHO) limesema njia hiyo ina madhara kimwili na kisaikolojia

Tazama https://youtu.be/Xy0rojmFt-s
#JFLeo
LISSU: TUTATENGENEZA NCHI YA WATU WALIO HURU

> Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu amesema watatengeneza nchi ya watu huru na yenye haki, ambayo hakuna Kiongozi atakayeogopwa kuliko Mungu

> Amewataka wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba 28

Tazama https://youtu.be/N2gbO75rV64

#TZ2020
MARA: IGP SIRRO AWATAKA WANASIASA KUTOWATUMIA WANANCHI VIBAYA

> Amewaonya baadhi ya wanasiasa kutumia shida za vijana kwa manufaa yao

> Amewataka wananchi wa Mara kuwa mfano wa siasa za busara, kwa kuwa wao ndio waanzilishi wa siasa nchini

Tazama https://youtu.be/A1-l4ppk1SI
#JFLeo
USAJILI WA MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA KUHITIMISHWA APRILI 2021

> Benki Kuu Tanzania (BoT) inaendelea kupokea maombi ya usajili/leseni kwa watoa huduma ndogo za fedha hadi Aprili 30, 2021

> Wahusika wawasilishe maombi yanayoendana na sheria

Soma https://jamii.app/UsajiliMadukaFedha
#JFLeo
OKTOBA 14: SIKU YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWALIMU NYERERE

> Leo ni Kumbukizi ya Kitaifa ya miaka 21 ya kifo cha Mwalimu Nyerere kilichotokea Oktoba 14, 1999

> Alikuwa muasisi wa Tanzania, alishiriki kulikomboa Taifa kutoka kwa wakoloni

Soma https://jamii.app/NyerereDay

#NyerereDay
PWANI: MAHABUSU ALIYEKUWA NA KESI YA MAUAJI AFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI

> Mahabusu Musa Haji Mchana amefariki na wafungwa wanne wamejeruhiwa kwa radi ktk gereza la Mng'aro

> Polisi wamesema hakuna mfungwa aliyetoroka na ulinzi umeimarishwa

Soma https://jamii.app/MahabusuRadi
#JFLeo
RWANDA YARUHUSU KILIMO CHA BANGI KWA SABABU ZA KIBIASHARA

> Serikali imehalalisha kulimwa na kuuzwa kwa bangi nje ya nchi ili kunufaika kiuchumi

> Soko la zao hilo duniani lina thamani ya Dola Bilioni 345 (takriban Tsh. Trilioni 800)

Soma https://jamii.app/RwandaBangi
#JFLeo
HALIMA MDEE: NATUHUMIWA KUMCHONGANISHA GWAJIMA NA MADHEHEBU MENGINE

> Mgombea Ubunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Halima Mdee amesema atakata rufaa NEC dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Maadili ambayo yamemsimamisha kufanya kampeni kwa siku 7

Soma https://jamii.app/AdhabuMdee
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI: SIJAWAHI KUOMBWA KUWASAIDIA WANANCHI WA KAWE

> Akiwa eneo la Basihaya lililopo Boko jijini Dar, Dkt. John Magufuli amesema jana alipigiwa simu na Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Josephat Gwajima kuhusu adha ya maji

> Amesema wakimchagua Gwajima atawatengea Tsh. Bilioni 5 ili kukarabati mitaro ya Jimbo hilo

Soma https://jamii.app/MagufuliKaweDsm
#Uchaguzi2020
DKT: MAGUFULI: VYAMA VYENYE BENDERA ZILIZO NA RANGI NYEKUNDU VINAASHIRIA MABAYA

> Ameeleza kuwa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata Uhuru wa nchi hii bila kumwaga damu, ndio sababu bendera ya taifa haina rangi nyekundu

> Amesema kuna baadhi ya vyama vya siasa vina bendera zenye rangi nyekundu ambayo haiashirii dalili nzuri

Soma https://jamii.app/MagufuliKaweDsm
#Uchaguzi2020