JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UCHAGUZI 2020: IJUE HAKI YA VYAMA VYA SIASA NA WAGOMBEA KUTEUA MAWAKALA

> Chama kinaruhusiwa baada ya kupata ridhaa ya Mgombea/Wagombea kuteua na kuwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi majina ya mawakala siku 7 kabla ya siku ya #Uchaguzi

Soma > https://jamii.app/UteuziMawakala

#TZ2020
KIKWETE ASHAURI GHARAMA ZA MAZOEZI KWA WATOTO WENYE USONJI ZIPUNGUZWE

> Amesema kila zoezi moja ambalo watoto hufanyiwa ni Tsh. 20,000 Hospitali ya Muhimbili na Tsh. 50,000 Hospitali binafsi

> Mtoto anatakiwa kufanyiwa mazoezi 6 kila siku

Soma https://jamii.app/GharamaUsonji
#JFLeo
DKT. BASHIRU: SIFA YA MAENDELEO YA WATU NI KUJITAWALA WENYEWE

> Katibu Mkuu wa CCM Taifa, amesema maendeleo ya watu ni uwezo wa kujitawala, kuchapa kazi na kuwa na mahusiano mazuri

> Pia, amemsifu Dkt. Magufuli kwa kuleta maendeleo ya watu

Soma https://jamii.app/MagufuliKaweDsm
#TZ2020
TUNDU LISSU ALAZIMIKA KUTUMIA MTUMBWI KUFIKA UKEREWE

> Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na msafara wake wamelazimika kutumia Mitumbwi kufika Ukerewe kwa ajili ya Kampeni baada ya kuambiwa Kivuko cha Kisorya-Ngoma ni kibovu

Tazama https://youtu.be/hjbVHnKcOJ8
#Uchaguzi2020
ALI KIBA AOMBA MWALIMU NYERERE ATENGENEZEWE β€˜DOCUMENTARY’

> Msanii huyo amemuomba Dkt. Magufuli atenge fedha kwa ajili ya documentary ya Baba wa Taifa

> Amesema itasaidia kukuza tasnia ya filamu nchini na kufanya Nyerere afahamike kwa vijana

Soma https://jamii.app/NyerereDocumentary
#JFLeo
#UCHAGUZI2020: FACEBOOK KUDHIBITI TAARIFA ZA UPOTOSHAJI

> Facebook imezindua programu za kukabiliana na taarifa potofu ili kulinda Demokrasia kipindi hiki cha Uchaguzi

> Itahakikisha matangazo ya Kampeni yanathibitishwa kwa ajili ya uwazi

Soma https://jamii.app/FacebookUchaguzi
#JFLeo
BAKWATA MKOANI MTWARA YAMUUNGA MKONO MGOMBEA URAIS WA CCM

> Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Wilaya ya Mtwara Mjini limetoa tamko la kumuombea na kumuunga mkono Dkt. Magufuli ili achaguliwe kuwa Rais wa #Tanzania kwa awamu nyingine

Soma https://jamii.app/BakwataKuraMagufuli
#TZ2020
UCHAGUZI MKUU 2020 NA UDHALILISHWAJI WA WAGOMBEA WANAWAKE

> Inaelezwa Mgombea Ubunge Tarime Mjini, Esther Matiko (CHADEMA) amekuwa akidhalilishwa na baadhi ya watu huku wengine wakiwa ni viongozi kama Polisi anayedaiwa kumtukana juzi

Soma - https://jamii.app/MilaWagombeaKe
#Uchaguzi2020
DR CONGO: WANASAYANSI WATAHADHARISHA KUHUSU MLIPUKO WA VOLKANO

> Kuna hatari ya Mlima Nyiragongo uliopo Goma, Mashariki mwa nchi hiyo kulipuka ndani ya miaka minne

> Januari mwaka 2002, Mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya watu 250

Soma - https://jamii.app/VolcanoDRC
#JFLeo
TUNDU LISSU: MAGUFULI AMEBAKIZA SIKU 14 KUKAA IKULU

> Akiwa Ukerewe amesema akichaguliwa kuwa Rais manyanyaso dhidi ya Wavuvi yatakuwa mwisho

> Ataboresha Sheria za uvuvi, kupanua Bandari ya Nansio na kujenga daraja la Kisorya-Ukerewe

Soma https://jamii.app/LissuUkerewe
#Uchaguzi2020
TUNDU LISSU KUJIBU MASWALI YA WANANCHI KUPITIA JAMIIFORUMS

> Mwanachama wa JamiiForums na Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu atajibu maswali ya Wananchi kupitia JamiiForums

> Ni kesho Oktoba 15, 2020 kuanzia saa 2 hadi 4 asubuhi

Uliza swali lako hapa https://jamii.app/LissuOnJF
DKT. MAGUFULI: NATAMANI KUFIKA KILA ENEO KUFANYA KAMPENI LAKINI SIWEZI

> Amesema hawezi kwasababu na yeye ni binadamu

> Amesema mbali na kuwa Mgombea, yeye pia ni Rais ambaye anapaswa kufanya majukumu ya Serikali ambayo bado yanamkabili

Soma - https://jamii.app/DktJPMKawe
#TZ2020
ZANZIBAR: ADA-TADEA YAAHIDI KUINUA SEKTA YA MICHEZO ILI ISITEGEMEE WAFADHILI

> Mgombea Urais wa Chama hicho, Juma Khatib amesema ataweka bajeti maalum kuendesha Ligi Kuu

> Wafadhili watapewa nafasi, lakini bajeti ya Serikali haitaondolewa

Soma https://jamii.app/ADATADEA
#TZ2020
NIGERIA: WANANCHI WAENDELEA NA MAANDAMANO KUPINGA UKATILI WA POLISI

> Licha ya Serikali kufuta kikosi cha #SARS kilichopewa kazi ya kupambana na wahalifu, wananchi wanasema hawajaridhika na hatua hiyo na wanachokitaka ni Mageuzi kwenye Jeshi

Soma https://jamii.app/NigeriaProtests
UPDATE: Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kumuuliza maswali Lissu; imebidi apate muda kuyapitia maswali yote (takriban 1,000)

> Tunatarajia kufikia kesho atakuwa ameyapitia maswali hayo na yote yatajibiwa

> Shukrani kwa wote walioshiriki
MAALIM SEIF ATAKIWA KUFIKA MBELE YA KAMATI YA MAADILI LEO

> Mgombea wa Urais wa #Zanzibar (ACT-Wazalendo) anadaiwa kukiuka maadili ya Uchaguzi kutokana na kuwaambia watu wakapige kura Oktoba 27 badala ya Oktoba 28 iliyopangwa na ZEC

Soma - https://jamii.app/SeifKamatiMaadili
#Uchaguzi2020
SIKU YA KIMATAIFA YA KUNAWA MIKONO: OSHA MIKONO OKOA MAISHA

> Oktoba 15 ni Siku ya Kimataifa ya Unawaji Mikono. Ni siku maalum ya kuhamasisha watu kunawa mikono ili kuepuka maradhi

> Kaulimbiu ya Kitaifa ni β€˜Osha Mikono Okoa Maishaβ€˜

Soma - https://jamii.app/KunawaMikono