JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UCHAGUZI 2020: JINSI MPIGA KURA ANAVYOWEZA KUTAMBUA KITUO CHAKE CHA KUPIGIA KURA

> Orodha ya wapiga kura kwa kila kituo itabandikwa siku nane (8) kabla ya Siku ya Uchaguzi

> Kujua jinsi ya kuhakiki kituo chako cha kupigia kura, fungua > https://jamii.app/HakikiKituoKura

#Uchaguzi2020
SERIKALI KUTUMIA HELIKOPTA KUZIMA MOTO MLIMA #KILIMANJARO

> Waziri wa Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema wanatazamia kutuma Helikopta kuuzima moto unaowaka kwa siku ya 5 sasa

> Changamoto ni upepo mkali na kukauka kwa nyasi na vichaka

Soma - https://jamii.app/NdegeMotoKLM
MICHEZO: Wachezaji wa Klabu ya #Juventus wameamua kujiweka Karantini baada ya Kiungo wa Timu hiyo, Weston McKennie kuthibitika kuwa na maambukizi ya #CoronaVirus

> Taarifa za Weston zinakuja ikiwa ni siku 2 tangu Cristiano Ronaldo athibitike kuwa na Virusi hivyo

#JFSports
#UGANDA: POLISI WADAIWA KUIBA NYARAKA ZA BOBI WINE KUGOMBEA URAIS

> Amesema nyaraka za uteuzi wake wa kugombea Urais zimepotea baada ya uvamizi kutoka Vikosi vya Usalama jana mchana

> Timu yake tayari ilikuwa imeshakusanya sahihi Milioni 6

Soma - https://jamii.app/BobiOfficeRaid
UNICEF: WATU BILIONI 3 DUNIANI HAWANA VIFAA VYA KUNAWIA MIKONO

> Takriban robo tatu ya watu katika nchi masikini wanakosa vifaa hivyo

> Aidha 43% ya Shule hazina vifaa vya kunawia mikono, na hivyo kuwaathiri watoto wapatao Milioni 818

Soma - https://jamii.app/UNICEFTakwimu
GEITA: POLISI KUWASAKA WALIOVAMIA NYUMBA 3 ZA WAGOMBEA WA CHADEMA

> Watu zaidi ya 10 wanatuhumiwa kuchoma moto Bajaji 2, kuvunja vioo vya madirisha kwa mawe pamoja na kubomoa madirisha 2 ya nyumba usiku wa kuamkia Oktoba 13

Soma - https://jamii.app/BajajiMotoCDM
#Uchaguzi2020
NEC YAKABIDHI NAKALA YA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA VYAMA VYA SIASA

> Vyama vimekabidhiwa nakala tepe ya daftari la wapiga kura na orodha ya vituo vya kupigia kura

> Pia, Tume imevikabidhi Karatasi ya mfano ya kupigia kura

Soma https://jamii.app/NECWapigaKura
#Uchaguzi2020
DAR: MVUA YA OKTOBA 13 YAPELEKEA VIFO VYA WATU 8

> Miili 5 imeokotwa Mto Msimbazi, 2 imeokotwa maeneo ya Buguruni na mmoja Mto Mvule uliopo Ukonga

> Wawili kati ya waliofariki dunia ni watoto ambao walipoteza maisha wakiokoana Mto Msimbazi

Soma - https://jamii.app/MvuaMaafaDar
WIZARA YA AFYA YATOA TAHADHARI YA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKANA NA MAFURIKO

> Wananchi wanaaswa kuchemsha Maji ya kunywa au kutibu kwa dawa kabla ya kuyatumia na kuongeza usimamizi wa usafi ktk maeneo ya mikusanyiko kama Shuleni, Vyuo, Masoko

Soma https://jamii.app/MafurikoMagonjwa
TANZANIA MSHINDI WA TATU TUZO ZA BIASHARA DUNIANI

> Tanzania imepata Tuzo za Taasisi zinazosimamia Biashara Duniani (WTPO 2020) ktk kipengele cha matumizi bora ya ushirikiano ktk huduma ya kliniki ya biashara inayosimamiwa na TanTrade

Soma https://jamii.app/TzYa3Biashara
#JFBiashara
SHEIKH JONGO: VIONGOZI WA DINI MSIPIGIE CHAPUO VYAMA VYA SIASA MNAPOHUBIRI

> Afisa wa Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Thabiti Jongo
amewashauri kutoonesha mahaba ya vyama misikitini ili kutowagawa waumini

> Amewataka wahubiri amani

Soma https://jamii.app/DiniSiasaPemba
#Uchaguzi2020
NJOMBE: MBARONI KWA KUUA NA KUMWAGA UBONGO WA BABU YAKE

> Imani Mbilinyi (25) anatuhumiwa kumuua Elia Mbilinyi (90)

> Baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alimuuliza Mwenyekiti kama angeweza kumlinda. Mwenyekiti akawaita Mgambo na kutaarifu Polisi

Soma https://jamii.app/MauajiBabuNjombe
UHOLANZI YARUHUSU KIFO CHA MAPEMA KWA WATOTO WENYE MAGONJWA YASIYOPONA

> Serikali ya #Uholanzi imeidhinisha mpango wa kuruhusu kifo cha mapema kwa watoto wenye mwaka 1 mpaka miaka 12

> Lengo ni kuzuia watoto kuteseka kwa maumivu wanayopitia

Soma https://jamii.app/EuthanasiaHoland
MAALIM SEIF AFUNGIWA KUFANYA KAMPENI KWA SIKU 5

> Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemfungia Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo kuanzia kesho hadi Oktoba 20 kwa kuwashawishi watu wapige kura Oktoba 27 badala ya Oktoba 28

Soma - https://jamii.app/MaalimSeifAfungiwa5
#TZ2020
JAJI MSTAAFU: WASAIDIZI WA SHERIA MJIEPUSHE NA USHABIKI WA KISIASA

> Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman amewataka Wasaidizi wa Sheria wa Majaji kutumia taaluma na kuzingatia weledi katika uendeshaji wa mashauri ya Uchaguzi

Soma https://jamii.app/SheriaWelediUchaguzi
#TZ2020
MDAU: CHUKI NI CHANZO CHA MACHAFUKO, NI MUHIMU KUIEPUKA

> Mdau wa Jamiiforums.com anasema chuki hutokana na hasira inayochochewa na fitina au taarifa mbaya

> Chuki huaribu familia hadi mataifa, ameshauri kujifunza ili kuiepuka

Soma - https://jamii.app/KuepukaChuki
#JFMaarifa
MOROGORO: WATATU MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

> Rajabu Ramadhani, Athumani Ramadhani na Daniel William wanashikiliwa kwa mauaji ya Bernadetha Kibwana na Zabibu Maulidi

> Bernadetha ameuawa kwa shoka na Zabibu alipigwa na mchi kichwani

Soma - https://jamii.app/TuhumaMauaji
#JFLeo
BAKWATA: VIONGOZI WA DINI WASIFANYE KAMPENI KWENYE NYUMBA ZA IBADA

> Baraza za Ulamaa BAKWATA Taifa limewasihi viongozi wa dini kubaki kuwa wasuluhishi na wapatanishi

> Limewataka waislamu kuiombea nchi ili Uchaguzi Mkuu upite salama

Soma https://jamii.app/BAKWATAUchaguzi
#Uchaguzi2020
WIZARA YA AFYA: WAUGUZI WAZOEFU MUWASIMAMIE WATARAJALI

> Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Ziada Sellah amesema watarajali (interns) wasifanye kazi wenyewe

> Amesema, si sahihi wakiachwa peke yao kuwahudumia wagonjwa hospitalini

Soma - https://jamii.app/WauguziWatarajali
#JFLeo