JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UCHAGUZI 2020: ZANZIBAR KUFUNGA SHULE KUANZIA OKTOBA 24

> Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar, Dkt. Idrissa Muslim amesema Shule zote zitafungwa kuanzia Oktoba 24 na kufunguliwa Novemba 2, 2020 ili kupisha Uchaguzi Mkuu, Oktoba 28

Soma - https://jamii.app/ShuleUchaguzi
#Uchaguzi2020
NEC YATAJA KAMPUNI ILIYOSHINDA ZABUNI YA KUTENGENEZA KARATASI ZA KUPIGIA KURA

> NEC imesema Jamana Printers haikuhusika kwenye mchakato wa zabuni

> Aidha, walitangaza zabuni kwa mujibu wa Sheria ambapo Ren-Form CC ya Afrika Kusini ilishinda

Soma https://jamii.app/NECKaratasi
#TZ2020
UGANDA: RAIS MUSEVENI AJIONGEZEA JINA JIPYA

> Ni baada ya Tume kuwataka Wagombea wa Uchaguzi kuhakikisha majina kwenye Hati za Uteuzi yanalingana na yaliyo ktk rekodi za masomo

> Kwa sasa anatambulika kama Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni

Soma https://jamii.app/RaisMuseveni
MDAU: DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI SIO UADUI NA SIO MAPAMBANO YA WATU

> Anasema Chama chochote cha Siasa kikishinda kwenye Uchaguzi #Tanzania Bara au #Zanzibar haimaanishi Watanzania watapoteza uzima au Mlima Kilimanjaro utahamia Nchi nyingine

> Anafafanua kuwa, mpaka sasa mbegu za chuki, ubaguzi na ugomvi zimeshapandwa, na Wananchi wamekaa mkao wa kusubiria mavuno yake

Kwa Mjadala - https://jamii.app/DemokrasiaSiasa
#Uchaguzi2020
KIGOMA: WANNE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI NA RUSHWA

> Watatu kati ya watuhumiwa hao walikuwa watumishi wa TPA

> Wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutakatisha fedha na kuisababisha Mamlaka hasara ya zaidi ya Milioni 600

Soma https://jamii.app/UhujumuTPA
#JFLeo
UGANDA: MFUMO WA MIAMALA WA KAMPUNI YA SIMU WADUKULIWA, TSH. BILIONI 7.4 ZAIBWA

> Wadukuzi wametumia zaidi ya kadi za simu 2,000 kuingilia mifumo ya malipo kwa njia ya simu kisha wakaiamuru mifumo ya benki kuzilipa kadi hizo

Soma > https://jamii.app/MTNUgandaUdukuzi

#UlinziWaTaarifa
UGANDA: MCHEZA MPIRA WA MIGUU AUAWA KWA KUSABABISHA GOLI

> Churchill Owaci (22) ameuawa na wachezaji wenzake baada ya kuisababishia timu yao ya mtaani kufungwa

> Watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji hayo na uchunguzi unaendelea

Soma https://jamii.app/UgandaKifoMpira
#JFLeo
TUNDU LISSU: CHAGUENI BARAZA LA MADIWANI KUTOKA CHADEMA

> Amesema Baraza la Madiwani litakaloongozwa na CHADEMA ktk Halmashauri ni muhimu ili mambo yaende

> Pia, atajenga nchi yenye uhuru ili wananchi waendeshe maisha yao bila kubugudhiwa

Soma - https://jamii.app/LissuNzega
#TZ2020
MAARIFA: UFAHAMU MLIMA UNAOWAKA KWA MIAKA TAKRIBAN 6,000

> Eneo hilo lililopo Kaskazini mwa Jiji la Sydney nchini Australia limekuwa likijulikana kama 'Mlima Unaoteketea'

> Kwa asili inaaminika kuwa mlima huo ni wa volkano

Soma > https://jamii.app/MlimaMoto

#BurningMountain
RAIS TRUMP AREJEA KWENYE KAMPENI SIKU KADHAA TANGU ALIPOGUNDULIKA KUWA NA #COVID19

> Amefanya mkutano ktk Jimbo la #Florida ambapo aliwasili bila kuvaa Barakoa

> Amesema vizuizi vilivyowekwa kukabiliana na maambukizi ni vikali kupita kawaida

Soma https://jamii.app/TrumpBackCampaign
KENYA: WATOTO WOTE WA KIKE WATAKIWA KURUDI SHULENI HATA WENYE MIMBA

> Makamishna wa Kaunti wametakiwa kuchunguza Wanafunzi walioshindwa kuripoti Shuleni na kuwarudisha

> Wenye Mitihani ya Taifa watafanya bila kujali ni Wajawazito au La!

Soma - https://jamii.app/PregnantSchoolResume
DAR: SOKO LA MAHAKAMA YA NDIZI LATHIBITISHWA KUMILIKIWA NA WANANCHI

> Akifanya Kampeni Mburahati, Dkt. Magufuli amesema Soko hilo litakuwa chini ya wananchi

> Ni baada ya Mgombea Ubunge wa Ubungo (CCM), Prof. Mkumbo kuomba soko kurasimishwa

Soma https://jamii.app/MabiboSokoWananchi
#JFLeo
ZANZIBAR: CHAUMMA YATANGAZA KUMUUNGA MKONO MAALIM SEIF

> Mgombea Urais wa CHAUMMA, Ali Juma amewataka Wanachama kumpigia kura Maalim Seif

> Amesema Vyama hivyo vina ushirikiano wa kindugu katika historia ya siasa za #Zanzibar na #Tanzania

Soma https://jamii.app/UraisCHAUMMA

#TZ2020
UDP YASEMA HAITAKUWA NA MIKUTANO YA HADHARA

> Naibu Katibu Mkuu, Juma Khamis Faki amesema kutokana na ukata, Chama hicho kitatangaza Sera zake nyumba kwa nyumba

> UDP imesema ni njia rahisi kuwafikia walengwa katika kuwaomba kura

Soma - https://jamii.app/KampeniUDP

#Uchaguzi2020
PROF. LIPUMBA: HUWEZI KUWA NA UCHUMI MZURI BILA MFUMO MZURI WA FEDHA

> Mgombea Urais kupitia CUF amesema β€œHali ya upatikanaji wa fedha ni ngumu na baadhi ya biashara zinafungwa

> Ameahidi kufufua viwanda na kuongeza ujazo wa fedha

Soma - https://jamii.app/LipumbaMfumoFedha
#Uchaguzi2020
TLP: TUNAENDELEA KUMUUNGA MKONO MGOMBEA URAIS WA CCM

> Makamu M/kiti wa TLP, Domina Rwechungura amesema β€œSisi tulishasema tangu mwezi wa 5 tutamuunga mkono Rais Magufuli, hivyo Msajili kauli yake kwamba tumesitisha uamuzi wetu hatuitambui”

Soma - https://jamii.app/TLPMagufuli2020
#TZ2020
MADHARA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA DAR ES SALAAM
-
Hali ilivyo katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam baada ya mvua kuendelea kunyesha tangu asubuhi ya leo
-
Ni muhimu kuchukua tahadhari

Tazama https://youtu.be/w64m0ECpuSA
LISSU: UCHAGUZI HAUTAKUWA RAHISI, KURA HII NI YA UKOMBOZI WA NCHI

> Mgombea Urais (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kwa miaka 5 baadhi ya Wananchi wamepitia changamoto mbalimbali na Oktoba 28 ndiyo wakati wa Ukombozi kwa Watanzania

Soma - https://jamii.app/LissuUkomboziNchi
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI: HATUKUNUFAIKA NA MADINI KUTOKANA NA UDHIBITI MBOVU

> Rais Magufuli amesema udhibiti mdogo katika usafirishaji wa madini ghafi, wizi na utoroshaji wa madini ulifanya Tanzania isifaidike na madini

> Amesema Serikali ya awamu ya tano ilichukua hatua kudhibiti hayo ikiwemo kusitisha usafirishaji wa mchanga

Soma https://jamii.app/SerikaliGawio
#CORONAVIRUS: WAKENYA WAKASIRISHWA NA TUKIO LA WANAFUNZI KUPULIZIWA DAWA

> Wanafunzi wamepuliziwa dawa kama njia ya kuepuka Virusi hivyo baada ya kufungua Shule

> Shirika la Afya (WHO) limesema njia hiyo ina madhara kimwili na kisaikolojia

Tazama https://youtu.be/Xy0rojmFt-s
#JFLeo