JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NDUGAI: HII NI AWAMU YANGU YA MWISHO, SITARAJII KUGOMBEA UBUNGE TENA

> Job Ndugai ambaye amekuwa Mbunge wa Kongwa tangu mwaka 2000 ametoa kauli hiyo leo akiwa Kanisani

> Amewataka wenye nia njema ya kuongoza Jimbo hilo kujiandaa na kujipanga

Soma https://jamii.app/NdugaiUbunge
JE, UNAFAHAMU RUSHWA YA NGONO NI NINI?

> Rushwa ya ngono ni pale ambapo Mtu aliye katika mamlaka na katika kutekeleza mamlaka yake akitaka au akiweka upendeleo wa ngono kama kigezo cha kutoa ajira, cheo, haki, au huduma ya upendeleo

Soma > https://jamii.app/NgonoRushwa

#KemeaRushwa
JE, UNAIFAHAMU ADHABU YA KUOMBA/KUTOA RUSHWA YA NGONO?

> Mtu atakayethibitika kuomba au kutoa rushwa ya ngono atakuwa amefanya kosa, ataadhibiwa kwa faini isiyozidi Tsh. Mil 5 au kifungo cha miaka isiyozidi 3 au vyote kwa pamoja.

Soma > https://jamii.app/NgonoRushwa

#KemeaRushwa
MOTO WAUNGUZA SEHEMU YA MLIMA KILIMAJARO

- Inaelezwa kuwa moto huo unaoteketeza sehemu ya Mlima huo umezuka leo mchana

- Mamlaka zimesema zinaendelea na juhudi za kuzima moto huo na taarifa zaidi zitatolewa

Soma > https://jamii.app/MotoKilimanjaro

#JFLeo #MotoKilimanjaro
HALIMA MDEE AFUNGIWA KUFANYA KAMPENI KWA SIKU 7

> Mgombea Ubunge katika Jimbo la Kawe kupitia CHADEMA, Halima Mdee amefungiwa kufanya Kampeni kwa siku saba kuanzia leo, Oktoba 12 mpaka 18 akidaiwa kukiuka maadili ya Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/KampeniBanMdee
#Uchaguzi2020
UNYANYASAJI WA KIJINSIA BADO NI CHANGAMOTO ZANZIBAR

> Ndani ya miaka 3, watoto 88 wamepewa ujauzito na 50 kati yao wameozeshwa

> Kuanzia Januari 2019 - Agosti 2020 kuna kesi 761 za watoto kunyanyaswa huku 147 wakiingiliwa kinyume na maumbile

Soma https://jamii.app/UkatiliWatotoZbar
WANAFUNZI WATAKIWA KUSHIRIKI KUZIMA MOTO HIFADHI YA KILIMANJARO

> Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka wameombwa kufanya hivyo ili kuudhibiti moto kwa haraka

> Sehemu ya Msitu wa Mlima Kilimanjaro ilianza kuungua tangu jana

Soma https://jamii.app/CAWMSOMotoKlmn
UTAFITI: #CORONAVIRUS INAWEZA KUISHI KWENYE FEDHA, VIOO VYA SIMU KWA SIKU 28

> Utafiti wa Shirika la Kisayansi la Taifa la Australia pia umebaini kuwa, Virusi hivyo vinaweza kuishi kwa siku 17 kwenye mazingira ya nyuzi joto 20C na kwenye giza

Soma https://jamii.app/COVID19Siku28
NIGERIA: SERIKALI YAKIFUTA KIKOSI CHA KUKABILIANA NA UHALIFU

> Uamuzi huo umekuja baada ya maandamano ya Wananchi kutokana na madai ya vitendo vya ukatili toka kwa kikosi hicho

> Serikali imetangaza uchunguzi na kuwachukuliwa hatua wahusika

Soma - https://jamii.app/SARSDissolved
#SARSENDED
WATOTO BILIONI 1.3 WAMEACHA SHULE KUTOKANA NA #COVID19

> UNESCO imeonya kuwa, huenda baadhi yao wakashindwa kurudi Shule kutokana na hali ya kiuchumi ya nchi zao

> Mpango wa kupata Dola Bilioni 5 utazinduliwa ili kusomesha watoto masikini

Soma https://jamii.app/WanafunziShule
KUMBILAMOTO AMUOMBA RADHI DKT. MAGUFULI KWA KUMUHUJUMU

> Omar S. Kumbilamoto aliyekuwa Naibu Meya wa Ilala amesema, alipokuwa UKAWA walihujumu miradi ya Manispaa ili wasimpe 'kiki'

> Amewaomba radhi CCM, Viongozi wa Ilala na wananchi

Soma - https://jamii.app/KumbilamotoKampeni
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: MUNGU NDIYE ALIYENIPA KAZI YA URAIS

> Akiwa Kinyerezi, Dkt. John Magufuli anayegombea kuongoza muhula wa pili amesema, Mungu ndiye aliyempa kazi hiyo

> Amesema hakutoa rushwa ili kuwa Rais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015

Soma - https://jamii.app/MagufuliKinyerezi
#Uchaguzi2020
SERIKALI: TUKIO LA MOTO KTK SHULE YA KALOLENI LILIPANGWA

> Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi amesema wanaamini matukio hayo ni mpango unaoratibiwa na baadhi ya watu

> Baadhi ya wanafunzi wamesema walihisi harufu ya kiberiti kabla ya kuona moto

Soma https://jamii.app/HujumaKaloleni
#JFLeo
RUKWA: MTOTO ACHOMWA MIKONO AKIDAIWA KUIBA TSH. 400 YA SADAKA

> Jeshi la Polisi linamshikilia Stella Kangoza (29) kwa kumchoma moto mikononi binti yake mwenye miaka 9 akimtuhumu kumuibia Tsh. 400 aliyopanga kuitoa kama sadaka Kanisani

Soma - https://jamii.app/MotoMtotoSadaka
ZANZIBAR: MZEE ALIYETUHUMIWA KUWAONESHA WATOTO PICHA ZA NGONO AFUTIWA MASHTAKA

> Ni baada ya upande wa Mashtaka kuchukua muda mrefu bila kupeleka mashahidi

> Hamad Nassor (73) alituhumiwa kuwaonesha watoto picha za ngono

Soma https://jamii.app/ZnzWatotoNgono
RC SINGIDA: HATUTASITA KUMCHUKULIA HATUA ANAYEHATARISHA AMANI YA NCHI

> Dkt. Rehema Nchimbi amesema "Kuna watu wanazungumza maneno yenye viashiria vya uvunjifu wa amani wakidhani huenda kipindi hiki cha Kampeni Serikali haipo kazini"

Soma - https://jamii.app/NchimbiAmaniTZ
#Uchaguzi2020
UCHAGUZI 2020: ZANZIBAR KUFUNGA SHULE KUANZIA OKTOBA 24

> Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar, Dkt. Idrissa Muslim amesema Shule zote zitafungwa kuanzia Oktoba 24 na kufunguliwa Novemba 2, 2020 ili kupisha Uchaguzi Mkuu, Oktoba 28

Soma - https://jamii.app/ShuleUchaguzi
#Uchaguzi2020
NEC YATAJA KAMPUNI ILIYOSHINDA ZABUNI YA KUTENGENEZA KARATASI ZA KUPIGIA KURA

> NEC imesema Jamana Printers haikuhusika kwenye mchakato wa zabuni

> Aidha, walitangaza zabuni kwa mujibu wa Sheria ambapo Ren-Form CC ya Afrika Kusini ilishinda

Soma https://jamii.app/NECKaratasi
#TZ2020
UGANDA: RAIS MUSEVENI AJIONGEZEA JINA JIPYA

> Ni baada ya Tume kuwataka Wagombea wa Uchaguzi kuhakikisha majina kwenye Hati za Uteuzi yanalingana na yaliyo ktk rekodi za masomo

> Kwa sasa anatambulika kama Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni

Soma https://jamii.app/RaisMuseveni
MDAU: DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI SIO UADUI NA SIO MAPAMBANO YA WATU

> Anasema Chama chochote cha Siasa kikishinda kwenye Uchaguzi #Tanzania Bara au #Zanzibar haimaanishi Watanzania watapoteza uzima au Mlima Kilimanjaro utahamia Nchi nyingine

> Anafafanua kuwa, mpaka sasa mbegu za chuki, ubaguzi na ugomvi zimeshapandwa, na Wananchi wamekaa mkao wa kusubiria mavuno yake

Kwa Mjadala - https://jamii.app/DemokrasiaSiasa
#Uchaguzi2020