JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: MUSWADA WA KURUHUSU POLISI KUSIKILIZA MAWASILIANO YA SIMU WAPENDEKEZWA

> Muswada huo unaopendekezwa na Mbunge wa Kiambaa unaomba idhini kwa Polisi kusikiliza mawasiliano ya simu iwapo watakushuku unahusika na biashara ya #DawaZaKulevya

Soma https://jamii.app/PolicePhoneConv
MAREKANI: MATATIZO YA NDANI YAPELEKEA CITIBANK KUTOZWA FAINI YA DOLA MILIONI 400

> Mamlaka zimesema Benki imeshindwa kutatua changamoto ambazo zimekuwepo kwa miaka kadhaa, kitendo kinachoashiria imeshindwa kuwa na mkakati wa kudhibiti majanga

Soma https://jamii.app/CitibankFineUS
MBEYA: ACHOMWA KISU BAADA YA UGOMVI WA KUTOA SIRI ZA MICHEPUKO KWA WATU

> Tabia Abdalah (38) amechomwa kisu shingoni na Salome Buya (23) baada ya kuzuka ugomvi uliomtuhumu Salome kuwatangaza wenzake kwa watu pindi wakichepuka nje ya ndoa zao

Soma https://jamii.app/KisuMichepuko
PROF. LIPUMBA: UKUAJI WA UCHUMI HAUJAPUNGUZA WATU MASIKINI

> Mgombea Urais kupitia CUF, amesema ukuaji wa Uchumi wa #Tanzania haujaambatana na kasi kubwa ya kupungua kwa watu masikini, bali idadi ya watu masikini imeongezeka

Soma - https://jamii.app/LipumbaTarakea
#Uchaguzi2020
WHO: WATOTO MILIONI 2 HUFIA TUMBONI KILA MWAKA

> Ripoti ya WHO, UNICEF na washirika wake imesema vifo vinatokea zaidi kwenye nchi zinazoendelea

> Mkurugenzi wa UNICEF amesema kila sekunde 16, mjamzito hupata matatizo ya mtoto kufia tumboni

Soma - https://jamii.app/2milStillbirth
MAREKANI: TRUMP KUTOSHIRIKI MDAHALO WA WAGOMBEA URAIS KUPITIA MTANDAO

> Amesema hatoshiriki kwakuwa uamuzi huo unalenga kumlinda Joe Biden

> Tume imesema imebadili mfumo kulinda afya za washiriki baada ya Rais Trump kupata #COVID19

Soma - https://jamii.app/TrumpDebateUS
MANYARA: MWALIMU MKUU MBARONI KWA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI YA DARASA LA 7

> Oscar Waluye anatuhumiwa kuwalazimisha Wanafunzi wawili wa Darasa la 6 kufanya mitihani hiyo badala ya Watahiniwa, ambao uwezo wao darasani ni wa kiwango cha chini

Soma https://jamii.app/MwlMitihani7
BRAZIL: VISA VYA #CORONAVIRUS VYAFIKIA MILIONI 5

> Wizara ya Afya imetangaza visa vipya 31,553 na idadi ya wenye Virusi hivyo imefikia 5,000,694

> Wataalamu wana hofu ya kutokea kwa awamu ya pili ya maambukizi kabla ya kwanza haijadhibitiwa

Soma - https://jamii.app/COVID19Updates
DKT. MAGUFULI KUFANYA KAMPENI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

> Mgombea Urais wa #Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Magufuli anatarajiwa kufanya Mkutano wa Kampeni leo Oktoba 09, kuanzia saa 2 asubuhi katika Uwanja wa Mkapa, Temeke

Soma - https://jamii.app/MagufuliDar
#Uchaguzi2020
DKT. MWINYI AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI

> Amesema Serikali inawathamini wawekezaji kwasababu wanasaidia ukuaji wa Pato la Taifa

> Aahidi kuwawekea mazingira bora akiingia madarakani ili wafanye kazi bila ya kikwazo

Soma - https://jamii.app/DktMwinyiZNZ
#Uchaguzi2020
#CORONAVIRUS: KENYA KUANZA MAOMBI YA KITAIFA YA SIKU 3 LEO

> Wakenya wametakiwa kuliombea Taifa huku wakizingatia taratibu za kujikinga na maambukizi

> Hii ni mara ya pili kwa Kenya kufanya maombi tangu kuanza kwa mlipuko huo

Soma - https://jamii.app/NationalPrayerKE
NEC: ALIYEHAMA MAHALI ALIPOJIANDIKISHA HATAWEZA KUPIGA KURA SEHEMU NYINGINE

> Mjumbe wa NEC, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema kama watu husafiri kuja Dar ili kuangalia mpira wa Simba na Yanga, basi suala la kupiga kura ni la muhimu zaidi

Soma https://jamii.app/VituoKupigaKura
#Uchaguzi2020
ZANZIBAR: MAALIM SEIF KUKOMESHA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA

> Amesema Kikosi cha Kupambana na #DawaZaKulevya kimekuwa kinafanya kazi ya kuwakamata wauzaji wadogo, huku wahusika wakubwa wakiendelea na biashara hiyo bila wasiwasi

Soma - https://jamii.app/MaalimMadawa
#Uchaguzi2020
MATUMIZI HOLELA YA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO YAONGEZA SARATANI YA MATITI KWA MABINTI

> Taasisi ya Saratani(ORCI) imesema kuna ongezeko la Saratani kwa mabinti kuanzia miaka 25, na inachochewa na matumizi ya vidonge hivyo kinyume na taratibu

Soma https://jamii.app/SarataniMabinti
DKT. MAGUFULI: NIMESIKIA MALALAMIKO YA UPANA WA BARABARA YA KIMARA, SIONI UBAYA

> Akiwa kwenye Kampeni katika Uwanja wa Mkapa Mgombea Urais wa CCM amesema amesikia Mgombea mmoja wa Urais akilaumu upana wa Barabara ya Kimara-Kibaha

> Amesema, "Majibu yake ni mawili tu; Kwanza si kweli kwamba Barabara hii ni pana kuliko zote duniani, lakini hata kama ingekuwa kweli, mimi sioni ubaya wowote"

Soma - https://jamii.app/JPM-MkapaStadium
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI: TUSHIRIKIANE NA WAKENYA KUWAOMBEA #CORONA IONDOKE

> Dkt. Magufuli amesema ameongea na Rais wa #Kenya, Uhuru Kenyatta ambapo wameamua kufanya maombi ya siku 3 ili ugonjwa huo uondoke

> Amesema, "Ninawaomba ndugu zangu Watanzania tushirikiane katika maombi haya na wenzetu wa Kenya ili ugonjwa wa Corona uondoke nchini kwao"

Soma - https://jamii.app/JPM-MkapaStadium
#Uchaguzi2020
KAGERA: RAIA WA PAKISTAN AINGIA NCHINI KINYEMELA KWA KISINGIZIO CHA #COVID19

> Idara ya Uhamiaji inamshikilia Raia huyo aliyeingia nchini baada ya kusikia tangazo #Tanzania hakuna #Corona

> Alikaa Lockdown nchini #Uganda kwa takriban miezi 6

Soma https://jamii.app/MhamiajiCorona
TUZO YA AMANI YA NOBEL 2020 YAENDA KWA SHIRIKA LA WFP

> Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limetunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel kufuatia jitihada zake za kupambana na njaa na kuboresha mazingira ya amani katika maeneo yanayokabiliwa na vita

Soma - https://jamii.app/NobelPrize2020
#JFLeo
TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI KWA AWAMU YA 2

> Awamu ya 2 ya Udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2020/2021 itaanza Oktoba 12 hadi 18

> Waliodahiliwa Chuo zaidi ya kimoja wanahimizwa kuthibitisha Udahili wao kabla ya Oktoba 17

Soma https://jamii.app/UdahiliVyuo2
WIZARA YA AFYA: ZAIDI YA WATU MILIONI 2 TANZANIA WANA MATATIZO YA KUONA

> Mkurugenzi wa Tiba, Dkt. Grace Magembe amesema watu Milioni 2.4 wana matatizo hayo

> Wanaokaa kwenye Runinga na Kompyuta kwa muda mrefu wapo hatarini kupata upofu

Soma - https://jamii.app/MatatizoMachoTZ