JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ARUSHA: KADA WA CHADEMA ADAIWA KUSHAMBULIWA NA KUTUPWA BARABARANI

> Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoani humo, Elias Mungure amesema walimuokota Evarist Rite kando ya Barabara huku akivuja damu kwenye ulimi, mikono, sehemu za siri na kuvunjwa meno 2

Soma https://jamii.app/KadaCDMShambulio
MAALIM SEIF: ELIMU YA ZANZIBAR IMESHUKA CHINI YA CCM

> Amesema idadi kubwa ya Wanafunzi darasani hupelekea washindwe kuelewa na kufeli

> Serikali ya ACT-Wazalendo itatoa kipaumbele ktk kuongeza majengo ili Wanafunzi wasizidi 35 darasani

Soma https://jamii.app/ElimuZNZ
#TZ2020
IGP SIRRO: WANASIASA PAMBANENI NA SIASA, MSIWAINGIZE VIJANA KWENYE UHALIFU

> Amewataka baadhi ya Viongozi kuacha kuwatumia Vijana na kuwaingiza kwenye uhalifu

> Ametoa wito kwa Vijana kutokubali kutumiwa na kubeba matatizo ya wengine

Soma https://jamii.app/SirroSiasaVijana

#Uchaguzi2020
FAHAMU MAADILI YA UCHAGUZI KWA VIONGOZI WA SERIKALI

> Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni miongoni mwa Watendaji wa Serikali ambao hawatakiwi kuingia katika vituo vya kupiga, kuhesabu au kujumlishia kura

> Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawaruhusiwi kuchanganya ziara za kikazi na shughuli za kiuchaguzi

Soma - https://jamii.app/WatendajiUchaguzi
#Uchaguzi2020
PROF. LIPUMBA: NITAHAKIKISHA KILA MWANANCHI ANAPATA MILO 3 KWA SIKU

> Akiwa Tanga, Mgombea huyo wa CUF amesema atahakikisha kila Mwananchi ana uwezo au anawezeshwa katika hilo

> Pia, amesema hatua zitachukuliwa ili wajawazito wapate lishe bora

Soma https://jamii.app/LipumbaKorogwe
#TZ2020
IGP SIRRO: HATUA ZA KINIDHAMU ZITACHUKULIWA IKIGUNDULIKA KOSA KWA ASKARI ALIYEMWAMBIA MBOWE β€˜HASHINDI’

> Timu kutoka makao makuu ipo wilayani Hai kuchunguza tukio hilo

> IGP Sirro amesema si kazi ya askari kusema huyu atashinda au hatashinda

Tazama https://www.youtube.com/watch?v=ckRR_9eX2JY
MAJALIWA: TUSIMCHAGUE MTU KWASABABU AMEPANDA JUKWAANI KWA MBWEMBWE

> Amesema ni lazima kupata Kiongozi atakayeunganisha Watanzania wote

> Amewataka Watanzania kuchagua CCM kwakuwa ni Taasisi yenye uwezo wa kuwatumikia wananchi bila kujali itikadi

Soma https://jamii.app/UchaguziViongozi
#TZ2020
TUNDU LISSU KUENDELEA NA KAMPENI LEO MKOANI SINGIDA

> Mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amemaliza kutumikia adhabu ya kutofanya kampeni kwa siku 7 iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi na leo anatarajiwa kuwa Mikoa ya Singida na Dodoma

Soma https://jamii.app/KampeniLissu
#Uchaguzi2020
ASKOFU AWATAKA UPINZANI WAONDOE HOFU YA KUIBIWA KURA

> Askofu wa AICT Dayosisi ya Mwanza, Philipo Mafuja amewataka wananchi kuelewa, sio Viongozi wote wanaogombea wanaweza kuwa Viongozi hivyo wakubaliane na matokea pindi kura zisipotosha

Soma https://jamii.app/AskKuibaKura
#TZ2020
WANAUME WAATHIRIKA ZAIDI NA MAGONJWA YA AKILI

> Daktari wa Magonjwa ya Akili (Muhimbili) Dkt. Fileuka Ngakongwa amesema, sababu za wanaume wengi kuugua matatizo ya akili katika umri mdogo ni msongo wa mawazo, ugumu wa maisha na kuweka vitu moyoni

Soma - https://jamii.app/MagonjwaAkili
MAALIM SEIF: TUTATOA KIPAUMBELE KWA WANAWAKE WASIBAKI KUWA WASINDIKIZAJI

> Amesema, ACT-Wazalendo itahakikisha nafasi nyingi za Uongozi zinashikiliwa na Wanawake

> Amesema, Wanawake ni jeshi kubwa linalotegemewa kuleta ushindi ktk Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/ACTWanawakeUongozi
#TZ2020
DKT. SHEIN: KIWANGO CHA ELIMU ZANZIBAR HAKIJASHUKA

> Amepinga hoja zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa, kiwango cha elimu kimeshuka

> Amesema kuna idadi kubwa ya Wanafunzi wanafaulu vizuri na kuzungumza Lugha za kigeni ikiwemo Kiingereza

Soma - https://jamii.app/SheinElimuZnz
#JFLeo
USHAURI WA MAMBO YA KUFANYA ILI KUKUSAIDIA UJIFUNGUE KWA NJIA YA KAWAIDA

> Jitahidi kufanya mazoezi kila siku kipindi chote wa ujauzito ili uwe tayari kuhimili changamoto zote za kujifungua. Kataa kuishi maisha ya 'stress' kila wakati

> Jitahidi kuutunza uzito wako. Zuia kuongezeka uzito uliopitiliza (Obesity). Anza kujifunza na kufuatilia taarifa zinazohusu namna gani ya kukabiliana na uchungu

Zaidi, soma - https://jamii.app/KujifunguaKawaida
LISSU (BAHI): CHADEMA ITARUDISHA UHURU WA KUONGEA ITAKAPOCHUKUA NCHI

> Itafanya hivyo kwasababu uhuru wa kuongea, kuhoji masuala ya maendeleo unakosekana

> Amewataka wananchi kupiga kura kukataa kodi na wizi wa Vitambulisho vya Ujasiriamali

Soma https://jamii.app/KampeniLissu
#TZ2020
MDAU: MTOTO WA MASIKINI AMBAYE SILAHA YAKE PEKEE NI ELIMU ATAJIAJIRI VIPI?

> Mdau wa JamiiForums.com anasema, japokuwa Tanzania kuna fursa mbalimbali, bado kumekuwa na wimbi kubwa la watu ambao hawana ajira

> Anasema wengi wanaowaambia vijana wajiajiri ni Wanasiasa na watu waliofanikiwa ambao wanapigana vikumbo kuwatafutia watoto wao ajira kwenye mashirika yanayolipa vizuri

Zaidi, soma - https://jamii.app/VijanaMafanikio
SIFA BAINIFU ZA WATOTO WALIOZALIWA KABLA YA KUHITIMU MUHULA (NJITI)

> Baadhi ya sehemu za mfumo wao wa neva hazijakua vyema

> Watoto hawa wana kiwango kidogo cha mafuta ya ngozi, hasa mafuta ya rangi ya kahawia

Soma > https://jamii.app/UzaziMtotoNjiti
WEMA SEPETU KUWANIA TUZO ZA HAPAWARDS 2020

> Msanii huyo wa Filamu anawania Tuzo za Hollywood And African Prestigious Awards za nchini Marekani katika kipengele cha Muigizaji Bora wa Kike wa Tamthilia za Kiafrika kupitia Tamthilia ya Karma

Soma - https://jamii.app/SepetuHAPAwards
MGOMBEA ADC: KAZI YA SERIKALI NI KUPANGA NJIA BORA ZA MATUMIZI YA RASILIMALI

> Mgombea Urais kupitia ADC, Queen Sendiga akiwa Mtwara ameahidi kurejesha ujenzi wa Kiwanda cha Gesi kama CCM ilivyoahidi awali na baadaye ikafanya tofauti

Soma - https://jamii.app/ADCRasilimali
#Uchaguzi2020
SABAYA: POLISI NAO NI BINADAMU, HUWA WANACHUKIA

> Mkuu wa Wilaya ya Hai amesema "Jeshi la Polisi ni Chombo cha Dola na wanaolitumikia ni binadamu, nao wanafika mahali wanakasirika"

> Amesema, Mbowe alitaka kufanya Kampeni eneo lisilotakiwa

Soma - https://jamii.app/HasiraPolisi