JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020: SIFA ZA MTU ANAYESTAHILI KUPIGA KURA

- (i) Awe amejiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura:

- (ii) Awe ana Kadi ya Mpiga Kura iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi

- (iii) Awe katika kituo alichojiandikisha kupiga kura

Zaidi, soma > https://jamii.app/KupigaKura

#Uchaguzi2020 #TZ2020 #JamiiForums
NEC: SHERIA ZA NCHI ZISIVUNJWE KWA KIGEZO CHA UCHAGUZI

> Tume imesema wakati huu nchi inapoelekea katika Uchaguzi, Sheria nyingine hazijasimama

> Wagombea wametakiwa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi na kuepuka lugha za kashfa na uchochezi

Soma https://jamii.app/NECVyamaSheria
#TZ2020
JE, UTARATIBU GANI UTATUMIKA SIKU YA KUPIGA KURA? (28.10.2020)

> Mpiga Kura anatakiwa kwenda kwenye kituo cha kupigia kura alichojiandikisha akiwa na kadi yake

> Anatakiwa kupanga mstari na kusubiri hadi zamu yake

Soma > https://jamii.app/KupigaKura

#Uchaguzi2020 #TZ2020 #Siasa
JE, UTARATIBU GANI UTATUMIKA SIKU YA KUPIGA KURA? (28.10.2020)

> Mpiga kura anatakiwa afuate maelekezo yote atakayopewa na msimamizi wa kituo muda wote akiwa kituoni

> Baada ya kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kurudi nyumbani

Soma > https://jamii.app/KupigaKura

#Uchaguzi2020
PROF. LIPUMBA: NITAKUWA RAIS WA WANYONGE, WAVUVI WATAPATA STAHIKI ZAO

> Akiwa Mkoani Mwanza, Mgombea huyo amesema atawasimamia wavuvi ili wapate stahiki zao

> Pia, atahakikisha kila mvuvi aliyenyang'anywa na kuchomewa nyavu analipwa fidia

Soma https://jamii.app/ProfLipumbaMWZ
#TZ2020
RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA DKT. SEMAKAFU

> Alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

> Nafasi yake itajazwa baadaye

Soma > http://jamii.app/AvemariaOut
DKT. MWINYI: KILA NITAKAYEMTEUA ATAWAJIBIKA KUTIMIZA MAJUKUMU YAKE

> Mgombea Urais Zanzibar (CCM) amesema atajenga mawasiliano na wafanyakazi ili kusikiliza changamoto zao na kuzitatua

> Hatakuwa na huruma kwa wabadhirifu na wala rushwa

Soma - https://jamii.app/UwajibikajiMwinyi
#TZ2020
ZEC: KURA YA MAPEMA HAITAHUSISHA ASKARI WOTE

> Tume ya Uchaguzi imesema watakaopiga kura Oktoba 27 ni watu maalum ikiwemo Watumishi wa Tume, Wasimamizi wa Uchaguzi na Askari ambao watahusika katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28

Soma https://jamii.app/KuraMapemaZNZ

#Uchaguzi2020
NEC: VYAMA VYA SIASA VIMERUHUSIWA KUWEKA WAKALA KILA KITUO OKTOBA 28

> NEC imesema, tayari vyama vyote vinavyoshiriki Uchaguzi vimepata nakala tepe ya orodha ya wapiga kura ili kuwawezesha Mawakala kuhakiki wapiga kura wanaofika kituoni

Soma - https://jamii.app/WakalaUchaguzi
#TZ2020
MAMBO YASIYOTAKIWA KUFANYWA NA WATENDAJI WA SERIKALI WAKATI WA UCHAGUZI

> Mawaziri, RC na DC kuchanganya ziara za kikazi na shughuli za kiuchaguzi

> Kutangaza katika vyombo vya habari au kwa namna yoyote misaada au ahadi ya aina yoyote

> Kutoa ahadi za shughuli za maendeleo ya jamii

> Kutumia madaraka au rasilimali za Serikali kwa shughuli za kampeni za uchaguzi

Soma > https://jamii.app/UchaguziMaadili

#TZ2020
MAREKANI: RAIS TRUMP ATOKA HOSPITALI, AWATAKA WATU WASIOGOPE #COVID19

> Rais Donald Trump amesema anajisikia vizuri na amewataka watu wasiruhusu #CoronaVirus itawale maisha yao

> Pia, Rais huyo amesema atarejea kufanya kampeni hivi karibuni

Soma https://jamii.app/TrumpCovidUS
SHAMBULIO LA WESTGATE, KENYA: HUKUMU YA WATUHUMIWA WA UGAIDI KUTOLEWA LEO

> Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa leo baada ya kuahirishwa jana

> Watu 67 walifariki ktk shambulio hilo la Septemba 2013, ambalo kundi la Al-Shabaab lilidai kuhusika

Soma https://jamii.app/WestgateCase
MALAWI: RAIS ATENGUA AHADI YA KUTOA AJIRA MILIONI MOJA

> Rais Chakwera aliyetoa ahadi hiyo ktk Kampeni amesema Serikali inaweza kuajiri watu 200,000

> Amesema, Serikali pekee haiwezi kutengeneza ajira na inahitaji msaada kutoka Sekta Binafsi

Soma https://jamii.app/RaisMalawiAjira
WANAFUNZI ZAIDI YA MILIONI 1 KUANZA MITIHANI YA KUMALIZA DARASA LA 7 KESHO

> Katibu Mtendaji wa NECTA amesema Watahiniwa 1,024,007 nchi nzima wanatarajiwa kufanya mitihani

> Mitihani itafanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 07 hadi 08, 2020

Soma - https://jamii.app/MitihaniDrs7
JKCI YATOA TAHADHARI YA ONGEZEKO LA WENYE MATATIZO YA MOYO

> Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imesema wagonjwa wanaofika Kliniki kwa siku ni 200 - 400

> Wengi wao wana shida ya Mishipa ya Damu kuziba, ambapo ikiziba husababisha kifua kuuma

Soma https://jamii.app/WagonjwaMoyo
ZANZIBAR: JESHI LAWATAKA VIONGOZI WA VYAMA KUACHA KUTOA VITISHO

> CP Mohamed Haji Hassan amesema Jeshi linaona baadhi ya matamshi kuwa ni maandalizi ya uvunjifu wa amani

> Jeshi litachukua hatua kali kuhakikisha Amani inalindwa

Soma - https://jamii.app/PolisiAmaniZNZ

#Uchaguzi2020
ZITTO KABWE APATA AJALI YA GARI KIGOMA

> Kiongozi huyo wa Chama cha ACT-Wazalendo amepata ajali wakati akitokea Kalya kuelekea Lukoma kwaajili ya kampeni

> Alikuwa na watu watano kwenye gari na wote wapo salama licha ya kupata majeraha

Soma - https://jamii.app/ZittoAjali
TFF YATAMBULISHA JEZI MPYA ZITAKAZOTUMIWA NA TAIFA STARS

> Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetambulisha jezi mpya ikiwemo jezi ya nyumbani, ya ugenini na jezi namba 3

> Oktoba 11, 2020 Tanzania itacheza mchezo wa kirafiki na Burundi

Soma https://jamii.app/JeziTaifaStars
AFISA HABARI WA ACT-WAZALENDO ATUHUMIWA KUSAMBAZA MAUDHUI YA NGONO TWITTER

> Dotto Rangimoto amefikishwa Mahakama ya Kisutu akidaiwa kutenda kosa hilo kwa jina la James Michael

> Amepata dhamana (Mdhamini 1 ambaye ni Mkazi wa Dar) na Bondi ya Tsh. Milioni 5

Soma https://jamii.app/DottoKizimbani
MAJALIWA: TANZANIA INAHITAJI KIONGOZI ANAYEWEZA KUPAMBANA NA MAFISADI

> Amesema Kiongozi anatakiwa kusimamia Serikali na kuhakikisha aliowateua wanatekeleza majukumu

> Amewataka wananchi wasichague viongozi kwa ushabiki ili wasije kujilaumu

Soma https://jamii.app/MajaliwaKiongoziTZ
#TZ2020