JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TUNDU LISSU ATAKIWA KURIPOTI POLISI

> IGP Simon Sirro amemtaka Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA kuripoti Kituo cha Polisi Kilimanjaro ili aeleze aliyofanya jana

> Amesema ameona mara kadhaa Lissu akigombana na viongozi wa Polisi

Angalia - https://youtu.be/ylpcJW4hG6Q
DKT. MAGUFULI: MKINICHANGANYIA MBUNGE SILETI MRADI WA MAJI

> Mgombea Urais kupitia CCM amesema wana mipango ya kutoa maji Ileje kwenda Tunduma Muhula ujao

> Amewataka wananchi kumchagua Silinde (CCM) na hii ni mara ya mwisho kuwabembeleza

Tazama https://youtu.be/xjJ1nLDvm9k
#TZ2020
KAMPUNI YA INDIANA YAFUNGUA KESI YA MADAI YA TAKRIBANI TSH. BILIONI 220 DHIDI YA TANZANIA

> Indiana Resources inadai fidia baada ya kuathirika na mabadiliko ya Sheria ya Madini nchini

> Tanzania ilizifuta leseni za uhifadhi zilizotolewa kabla ya 2018

Soma https://jamii.app/MadaiBilion220
LISSU: BARUA YA POLISI HAIKUELEZA KOSA, NAENDELEA NA RATIBA ZANGU

> Lissu amedai barua haikutaja kosa na imeelekezwa kwa Mwenyekiti wa Chama, hivyo ataendelea na ratiba zake

> Jana, IGP Sirro alimshutumu Lissu kugombana na Wakuu wa Polisi

Soma https://jamii.app/BaruaPolisiRatiba
#Uchaguzi2020
PROF. LIPUMBA: BAJETI YA KILIMO ITAKUWA 15% YA BAJETI YOTE

> Mgombea huyo amesema, Dira ya mabadiliko ya CUF inatoa kipaumbele kwa Kilimo ktk mikakati ya kukuza Uchumi na kuondoa umasikini ili kuhakikisha Tanzania ina chakula cha kutosha

Soma https://jamii.app/LipumbaSimiyu
#Uchaguzi2020
RAIS TRUMP NA MKEWE WAKUTWA NA #COVID19

> Rais Trump alifanyiwa vipimo baada ya Msaidizi wake kukutwa na maambukizi na tayari wanaanza kukaa Karantini

> Hali hii itasababisha ugumu wa yeye kuendelea na Kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Novemba 3

Soma https://jamii.app/COVID19TrumpAndWife
#JFLeo
MKOA WA NJOMBE WAONGOZA KWA TATIZO LA UDUMAVU KWA WATOTO

> Njombe inakabiliwa na udumavu kwa 53.6%, Rukwa 47.9%, Iringa 47.1%, Songwe 43.3% na Kigoma 42.3%

> Serikali imeandaa mpango mkakati wa kitaifa wa masuala ya lishe kuondoa tatizo hilo

Soma https://jamii.app/UdumavuWatoto
SIKU YA KIMATAIFA YA KUTOKUWA NA VURUGU DUNIANI

> #NonViolenceDay huazimishwa kila Oktoba 2 na iliazimiwa na Umoja wa Mataifa 2007

> Pia, ni siku ya kuzaliwa ya Mahatma Gandhi anayetajwa kama Mwasisi na Kiongozi wa kudai haki bila vurugu

Soma https://jamii.app/NonViolenceDay
UBALOZI WA MAREKANI: HATUMUUNGI MKONO MGOMBEA YEYOTE

> Ubalozi huo umesema matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa #Tanzania ni muhimu kwa kanda nzima ya #Afrika Mashariki

> Wamesema wanaunga mkono mchakato wa Kidemokrasia, Uhuru, Haki na Uwazi

Soma https://jamii.app/MarekaniUchaguziTZ
#Uchaguzi2020
KATAVI: AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUCHANA MABANGO YA CCM

> Augustino Laurent (27) anatuhumiwa kuchana bango lenye picha ya Mgombea Urais na tangazo la Mgombea Ubunge na Udiwani

> Amekosa dhamana na ameendelea kuwekwa chini ya ulinzi

Soma https://jamii.app/MabangoCCM

#Uchaguzi2020
NEC YAMFUNGIA TUNDU LISSU KUFANYA KAMPENI KWA SIKU 7

> Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemfungia Mgombea huyo wa Urais wa JMT kufanya kampeni kwa siku saba

> NEC imefikia uamuzi huo kwa madai ya kuwa Lissu amekiuka Maadili ya Uchaguzi

Soma > https://jamii.app/LissuVsNEC

#Uchaguzi2020
#NAMIBIA: WANAFUNZI ZAIDI YA 300 WAKUTWA NA #CORONAVIRUS

> Wizara ya Afya nchini humo imesema wanafunzi walioambukizwa wengi wao wanasoma Shule za Bweni

> Mpaka sasa #Namibia imethibitisha kuwa na jumla ya maambukizi 11,373 vya #CoronaVirus

Soma https://jamii.app/COVID19Namibia
ORCI: WAGONJWA WENGI WA SARATANI WANAKIMBILIA KWA WAGANGA NA IBADANI

> Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), amesema sababu kubwa ni kurubuniwa na matangazo yasiyo rasmi kuhusu dawa katika Mitandao ya Kijamii

Soma https://jamii.app/SarataniTibaWaganga
SAMIA: HAMNA HAJA YA KUPOTEZA NGUVU ZENU KUPIGIA KURA UPANDE MWINGINE

> Amesema "Ni sawa na kwamba unachukua fedha yako unatia shimoni. Haina faida, haina tija"

> Amewataka wananchi waipigie kura CCM ili kuendelea na safari ya maendeleo

Soma https://jamii.app/SamiaSingida
#TZ2020
LISSU: UAMUZI WA NEC HAUKUBALIKI, KAMPENI ZITAENDELEA JUMAPILI

> Amesema hajapokea malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi na hajawasilisha utetezi wake

> Pia, amesema hajapokea nakala ya kusimamishwa japokuwa ipo mitandaoni

Soma - https://jamii.app/LissuVsTume
#Uchaguzi2020
KENYATTA: NABADILI KATIBA KUWEKA UMOJA WA KITAIFA SIO KUBAKI MADARAKANI

> Rais wa #Kenya amekanusha kutaka kugombea kwa muhula wa 3

> Mabadiliko yanayopendekezwa ni kuundwa Ofisi ya Waziri Mkuu mwenye Mamlaka na Rais atakayechaguliwa na Bunge

Soma https://jamii.app/KenyattaKatiba
#TAKUKURU: UDSM INAONGOZA KWA RUSHWA YA NGONO

> Utafiti uliofanyika kuhusu rushwa ya ngono ktk Chuo cha Dar na Dodoma umegundua UDSM inaongoza kwa 40.5% na UDOM 38.6%

> Mbinu zinazotumika kurubuni ni ahadi ya kuolewa, Cheo na kuongezewa ufaulu

Soma https://jamii.app/RushwaNgonoVyuoni
#COVID19-UGANDA: WAGONJWA WASIOONESHA DALILI KUTOKA HOSPITALI BILA KUPIMWA

> Ni baada ya Serikali kurekebisha mwongozo wake wa kukabiliana na Virusi hivyo

> Awali, wagonjwa walipimwa mara 2 kabla ya kutoka, hatua ambayo baadhi waliilalamikia

Soma https://jamii.app/Corona-UG
MSAJILI: NI MUHIMU KUEPUKA MIGONGANO NA SERIKALI SIKU ZILIZOSALIA

> Jaji Mstaafu Francis Mutungi amewataka wenye malalamiko kufika Tume ya Uchaguzi

> Amesema hafurahishwi na baadhi ya kauli za Wagombea zinazoenda kinyume na Kanuni

Soma - https://jamii.app/MsajiliUchaguzi
#Uchaguzi2020