JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SIASA SIO UADUI, LEMA NA GAMBO WAPIGA PICHA YA PAMOJA

> Wagombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo (CCM) na Godbless Lema (CHADEMA) wamepiga picha ya pamoja

> Tukio hili linadhihirisha Siasa sio sababu ya kuchukiana au kutoana uhai

Soma https://jamii.app/SiasaSioUadui
#JFSiasa
KATIBU MKUU WA UN: HATUTAKIWI KUYASAHAU MAISHA YA MTU ALIYETUTOKA

> Antonio Guterres: Dunia haitakiwi kuyasahau maisha ya hata mtu mmoja aliyefariki kutokana na #COVID19

> Hadi sasa vifo vinavyotokana na #CoronaVirus vimezidi watu milioni 1

Soma > https://jamii.app/GuterresCovid19
LIJUE GEREZA AMBALO WAFUNGWA WANAJITAFUTIA CHAKULA

> Gereza la Sanganer lililopo India hutoa sehemu ya kulala tu kwa wafungwa, nao hulazimika kufanya kazi ili kupata mahitaji ya kila siku

> Wanaharakati wanataka magereza kama hayo yaongezeke

Soma https://jamii.app/GerezaSanganer
#JFLeo
PROF. LIPUMBA: MAZINGIRA YA KUFANYIA BIASHARA NI MAGUMU SANA TANZANIA

> Amesema ni kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mazingira ya Kufanya Biashara ya mwaka 2020 ambapo Tanzania ni ya 141 kati ya nchi 190

Soma > https://jamii.app/LipumbaBiasharaTz

#Uchaguzi2020 #TZ2020 #JamiiForums
NEC: WENYE MAHITAJI MAALUM WAMEANDALIWA MAZINGIRA RAFIKI KUSHIRIKI UCHAGUZI

> Watu hao ni Wajawazito, Wanaonyonyesha, Wazee na Walemavu

> Aidha, Wasioona (Wasiotumia Nukta Nundu) na wasiojua kusoma wanaruhusiwa kuwa na wanayemuamini

Soma https://jamii.app/WalemavuUchaguzi

#TZ2020
SEPTEMBA 30, SIKU YA KIMATAIFA YA KUFASIRI

> UN inatambua umuhimu wa kufasiri ktk kuleta mataifa pamoja

> Tamko la Haki za Binadamu Duniani linashikilia rekodi ya kuwa nyaraka iliyofasiriwa zaidi

Soma https://jamii.app/InternationalTranslationDay
#JFLeo
MBEYA: DKT. MAGUFULI AMUOMBA KURA 'SUGU'

> Mgombea huyo amesema, "naomba kura kwa watu wote, hata Sugu ninamuomba kura"

> Ameongeza kuwa, Dhamira yake ni kuibadilisha Mbeya kabla muda wake haujaisha ili liwe Jiji la mfano kitaifa na kimataifa

Soma https://jamii.app/MagufuliSugu

#JFLeo
LISSU: HATUNA MASLAHI NA URAIS ZANZIBAR, NDIO MAANA TUNAMUUNGA MKONO MAALIM SEIF

> Tundu Lissu amesema hawatatangaza Muungano bali wataungana mkono ktk maeneo ambayo hawana maslahi

> Amesema hiyo haikatazwi kisheria kwa kuwa sio Muungano

Soma https://jamii.app/PoliticalCoalition
#JFLeo
DKT. MAGUFULI: HAMKUWA NA MBUNGE WA KUWASEMEA BALI MLIPATA MSANII

> Mgombea Urais wa JMT kupitia CCM amewaambia wananchi wa Mbeya kwamba hawakuwa na Mbunge wa kuwasemea bali walikuwa na Msanii (Sugu) ambaye sio mkali kama Diamond na Alikiba

Soma https://jamii.app/MagufuliSugu
#JFLeo
MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI YASEMA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR UPO KIHALALI

> Wanaharakati walifungua kesi kuhoji uhalali wa Muungano

> Kanuni ilitaka malalamiko yawasilishwe siku 60 tangu tukio lilipotokea lakini imeshapita miaka 56

Soma https://jamii.app/MuunganoTanzania
#JFLeo
LISSU: KILA MTU ANA HAKI YA KULINDWA FARAGHA YAKE

> Amesema, #Katiba ya Tanzania inatamka wazi kuwa kila mtu ana haki ya kulindwa faragha yake

> Amesema, Maisha ya chumbani na mkeo au yeyote yule ni marufuku kwa Serikali kuchungulia

Soma https://jamii.app/PoliticalCoalition
#Uchaguzi2020
SHIRIKA LA NDEGE LA QATAR AIRWAYS LAINGIA MAKUBALIANO NA AIR TANZANIA

> Abiria wataweza kusafiri kwa urahisi kati ya Afrika na Doha kwa kuunganisha na Asia, Pasifiki, Amerika, Ulaya na Mashariki ya Kati

Soma > https://jamii.app/AirTzVsQatarAir

#AirTanzania #QatarAirways #JFLeo
KESI YA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA KUSIKILIZWA TANZANIA

> Mahakama ya Rufaa nchini Ufaransa imekubali Felicein Kabuga kushtakiwa Tanzania

> Kabuga alikamatwa baada ya kujificha kwa miaka 26. Anatuhumiwa kufadhili mauaji ya 1994

Soma https://jamii.app/KabugaKushtakiwa
#JFLeo
PROF. LUHANGA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA CHUO KIKUU MZUMBE

> Rais Magufuli amemteua Prof. Matthew Luhanga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe kwa Kipindi cha Pili

> Uteuzi huo unaanza Septemba 30, 2020

Soma https://jamii.app/LuhangaMwenyekiti
#JFLeo
LISSU: DUNIA HAIHITAJI TANZANIA ILA TANZANIA INAIHITAJI DUNIA

> Amesema bidhaa kama Dhahabu, Korosho na Chai zinaweza kupatikana ktk nchi nyingine hivyo, Serikali yake (CHADEMA) itahakikisha inashirikiana vyema na Mataifa mengine

Soma https://jamii.app/PoliticalCoalition

#TZ2020
SIKU YA WAZEE DUNIANI: DUNIA NA JAMII TUWAJIBIKE KUWATUNZA WAZEE

> Oktoba 1 kila mwaka, ni Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani inayotumiwa kutambua Ustawi wa Wazee

> Tanzania imefanikiwa kupunguza mauaji na kuboresha Huduma na Vituo vya Wazee

Soma https://jamii.app/SikuYaWazee
MTU WA KWANZA KUTIBIWA UKIMWI, AFARIKI KWA SARATANI

> Raia wa Marekani, Timothy Ray Brown (54), alipata UKIMWI 1995, alipandikizwa Uboho (Bone Marrow) wa mtu aliyekuwa na kinga ya VVU

> Njia iliyotumika kumtibu ni ghali sana lakini ilileta tumaini Duniani

Soma https://jamii.app/UKIMWISaratani
ZANZIBAR: MAALIM SEIF AAHIDI MUUNGANO WA SERIKALI 3

> Akiwa Pemba, amewataka wananchi kumpa kura na kumuwezesha kuleta mabadiliko

> Pia, amesema akipewa ridhaa, atazungumza na Serikali ya Muungano kuhusu muundo wa Jeshi la Polisi

Soma - https://jamii.app/MaalimKampeniZNZ

#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI: SERIKALI IKO PAMOJA NA WAZEE

> Ktk kuadhimisha Siku ya Wazee(Oktoba 1) amesema, Serikali imehakikisha Wazee wanatibiwa bure kwenye hospitali za Serikali

> Changamoto chache zilizobaki watazishughulikia miaka 5 inayokuja

Soma https://jamii.app/MagufuliMbalizi
#Uchaguzi2020
DAR: SERIKALI YAZINDUA CHUO CHA MAFUNZO YA ELIMU YA MICHEZO NA UKOCHA

> Chuo hicho cha Maendeleo ya Michezo kinatoa Stashahada ya Utawala na Uongozi ktk #Michezo na Stashahada ya Ukocha nchini kwa kuzingatia Mitaala iliyopitishwa Kimataifa

Soma https://jamii.app/ChuoMichezo