JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UCHAGUZI MAREKANI: MIKE POMPEO AKATALIWA KUONANA NA PAPA FRANCIS

> Wanadiplomasia wa juu wa Vatican wamesema uamuzi huo umefikiwa kwasababu Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliweka wazi kuwa Wanasiasa hawatapokelewa kipindi cha Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/PompeoVatican
VYAMA VINAVYOTAKA KUUNGANA OKTOBA 03 VYATAKIWA KUACHA MPANGO HUO

> Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa amevitaka kutofanya hivyo kwasababu ni ukiukwaji wa Sheria

> Amesema, Ofisi yake imeshaviandikia barua vyama hivyo

Soma - https://jamii.app/MsajiliVyamaOkt3
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI AAHIDI TSH. MILIONI 5 YA KUJENGEA MADARASA YA SHULE YA MSINGI ULANGA

> Ameahidi hela hiyo baada ya mwanafunzi aliyekuwa kwenye mkutano kutaja madarasa kuwa changamoto

> Amesema hakutoa palepale kuepuka rushwa ya Uchaguzi

Soma https://jamii.app/MagufuliTshMil5
#Uchaguzi2020
πŸ‘1
MAGANJA: TANZANIA INGEONGOZWA VIZURI TANGU UHURU BASI INGEKUWA UJERUMANI YA AFRIKA

> Mgombea Urais wa JMT kupitia NCCR, Yeremia Maganja amesema chanzo cha haya ni utekelezaji wa Azimio la Arusha ambao haukuzingatia mazingira ya watu wake

Soma - https://jamii.app/MgombeaNCCR
#Uchaguzi2020
GUINEA: VIKOSI VYA USALAMA VYALAUMIWA KUUA WATU 50 KATIKA MAANDAMANO

> Ripoti zinataja watu 50 kuuawa, 200 kujeruhiwa na 70 kuzuiliwa kinyume cha Sheria mwaka 2019

> Ni katika maandamano ya kupinga Rais Alpha CondΓ© kuongeza Muhula wa Tatu

Soma https://jamii.app/Maandamano50Guinea
RAIS MAGUFULI AFUTA TOZO YA TSH. 50,000 KWA WAJAWAZITO WANAOCHELEWA KLINIKI

> Amesema kumekuwa na malalamiko dhidi ya kampeni ya Mama Kamandoo ya kuwatoza wajawazito wanaochelewa kujiandikisha kliniki Tsh. 50,000

> Amewataka Viongozi wa Serikali na Wizara ya Afya kusimamia utekelezaji wa agizo hilo kuhusu tozo

Angalia https://youtu.be/4OQ-dYNWxOI
#Uchaguzi2020
#COVID19: AFRIKA KUSINI YAFUNGUA MIPAKA KWA NCHI ZA AFRIKA

> Wasafiri kutoka nchi zenye idadi kubwa ya visa na vifo kuliko Afrika Kusini hawataruhusiwa kuingia kwa ajili ya utalii

> Nchi hiyo ina visa 674,339, vifo 16,734 na 608,112 wamepona

Soma https://jamii.app/SAOpensBorders
JESHI LA POLISI LAWATAKA WANANCHI KUTII SHERIA

> Wakati huu wa Uchaguzi, Jeshi limetoa rai kwa wananchi kuepuka matusi, kujichukulia Sheria mkononi na kutotoa taarifa za uongo ambazo zinalenga kuleta chuki miongoni mwa Watanzania

Soma - https://jamii.app/SheriaPolisiUchaguzi
#Uchaguzi2020
LISSU: CHADEMA YA LEO SIO ILE YA 2015, TUTAWEKA MAWAKALA KILA MAHALI

> Amesema hivi sasa wana uongozi na matawi kwenye takriban kila Kijiji

> Amesema hawatokubali Mawakala wao wasiapishwe, watatumia mbinu zote kuhakikisha wanaapishwa

Soma https://jamii.app/CHADEMAPress
#Uchaguzi2020
DPP AIDHINISHA MASHTAKA YA KUUAWA KWA KADA WA CCM IRINGA

> DPP Biswalo Mganga ameidhinisha mashtaka dhidi watuhumiwa 4 (3 ni Makada wa CHADEMA) ambao wamekiri kumteka na kumuua Emmanuel Mlelwa, aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Vyuo Vikuu Iringa

Soma https://jamii.app/DPPMauajiMlelwa
TUNDU LISSU ATAKIWA KURIPOTI POLISI

> IGP Simon Sirro amemtaka Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA kuripoti Kituo cha Polisi Kilimanjaro ili aeleze aliyofanya jana

> Amesema ameona mara kadhaa Lissu akigombana na viongozi wa Polisi

Angalia - https://youtu.be/ylpcJW4hG6Q
DKT. MAGUFULI: MKINICHANGANYIA MBUNGE SILETI MRADI WA MAJI

> Mgombea Urais kupitia CCM amesema wana mipango ya kutoa maji Ileje kwenda Tunduma Muhula ujao

> Amewataka wananchi kumchagua Silinde (CCM) na hii ni mara ya mwisho kuwabembeleza

Tazama https://youtu.be/xjJ1nLDvm9k
#TZ2020
KAMPUNI YA INDIANA YAFUNGUA KESI YA MADAI YA TAKRIBANI TSH. BILIONI 220 DHIDI YA TANZANIA

> Indiana Resources inadai fidia baada ya kuathirika na mabadiliko ya Sheria ya Madini nchini

> Tanzania ilizifuta leseni za uhifadhi zilizotolewa kabla ya 2018

Soma https://jamii.app/MadaiBilion220
LISSU: BARUA YA POLISI HAIKUELEZA KOSA, NAENDELEA NA RATIBA ZANGU

> Lissu amedai barua haikutaja kosa na imeelekezwa kwa Mwenyekiti wa Chama, hivyo ataendelea na ratiba zake

> Jana, IGP Sirro alimshutumu Lissu kugombana na Wakuu wa Polisi

Soma https://jamii.app/BaruaPolisiRatiba
#Uchaguzi2020
PROF. LIPUMBA: BAJETI YA KILIMO ITAKUWA 15% YA BAJETI YOTE

> Mgombea huyo amesema, Dira ya mabadiliko ya CUF inatoa kipaumbele kwa Kilimo ktk mikakati ya kukuza Uchumi na kuondoa umasikini ili kuhakikisha Tanzania ina chakula cha kutosha

Soma https://jamii.app/LipumbaSimiyu
#Uchaguzi2020
RAIS TRUMP NA MKEWE WAKUTWA NA #COVID19

> Rais Trump alifanyiwa vipimo baada ya Msaidizi wake kukutwa na maambukizi na tayari wanaanza kukaa Karantini

> Hali hii itasababisha ugumu wa yeye kuendelea na Kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Novemba 3

Soma https://jamii.app/COVID19TrumpAndWife
#JFLeo
MKOA WA NJOMBE WAONGOZA KWA TATIZO LA UDUMAVU KWA WATOTO

> Njombe inakabiliwa na udumavu kwa 53.6%, Rukwa 47.9%, Iringa 47.1%, Songwe 43.3% na Kigoma 42.3%

> Serikali imeandaa mpango mkakati wa kitaifa wa masuala ya lishe kuondoa tatizo hilo

Soma https://jamii.app/UdumavuWatoto
SIKU YA KIMATAIFA YA KUTOKUWA NA VURUGU DUNIANI

> #NonViolenceDay huazimishwa kila Oktoba 2 na iliazimiwa na Umoja wa Mataifa 2007

> Pia, ni siku ya kuzaliwa ya Mahatma Gandhi anayetajwa kama Mwasisi na Kiongozi wa kudai haki bila vurugu

Soma https://jamii.app/NonViolenceDay
UBALOZI WA MAREKANI: HATUMUUNGI MKONO MGOMBEA YEYOTE

> Ubalozi huo umesema matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa #Tanzania ni muhimu kwa kanda nzima ya #Afrika Mashariki

> Wamesema wanaunga mkono mchakato wa Kidemokrasia, Uhuru, Haki na Uwazi

Soma https://jamii.app/MarekaniUchaguziTZ
#Uchaguzi2020