JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TANZIA: SAID MABERA WA MSONDO NGOMA AFARIKI DUNIA, ATAZIKWA LEO SAA 10 ALASIRI

> Gwiji huyo wa kupiga Gitaa la Solo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda wa zaidi ya miezi 2

> Alijiunga na Msondo Ngoma mwaka 1973

Soma https://jamii.app/RIPMabela
#RIPMabera
NJOMBE: MAKADA 3 WA CHADEMA WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI

> Makada hao ni Tadei Mwanyika, George Sanga, Optatus Mkwera wakishirikiana na Goodluck Mfuse (Dalali wa Magari) ambao wanatuhumiwa kumuua Emmanuel Mlelwa (UVCCM) Iringa

Soma https://jamii.app/CHADEMAMauajiUVCCM
#JFLeo
MDAU: UKIAMUA KUJIAJIRI NI LAZIMA UWE NA NIDHAMU YA KAZI ZAIDI YA ULIVYOKUWA UMEAJIRIWA

> Anasema, kuna watu wanadhani kuajiriwa ni utumwa na kutokana na uzembe wanaona ni bora wawe na biashara ili waweze kuamka saa 5 asubuhi

> Kama bosi utatakiwa kuwa mfano wa kutunza muda, mazingira na kuonesha vile ambavyo unahitaji wafanyakazi wako wawe. Hii inahitajika nidhamu zaidi kuliko ile ya mtu aliyeajiriwa

Soma https://jamii.app/NidhamuKujiajiri
#JFBiashara
FAHAMU CHANGAMOTO ZINAZOMKABILI MTOTO NJITI

> Mtoto Njiti anaweza kuwa na changamoto ya kupumua hivyo punde tu baada ya kuzaliwa, anatakiwa kupatiwa huduma ya upumuaji

> Hawezi kuhimili baridi hivyo lazima ahifadhiwe kwenye chumba chenye joto la kutosha

> Wana hatari kubwa ya kupata maambukizi kwasababu kinga yao ya mwili haijakomaa

Soma - https://jamii.app/WatotoNjiti

#JFAfya
DKT. MAGUFULI AAHIDI KUJENGA UWANJA WA NDEGE NJOMBE

> Mgombea huyo wa Urais amesema, watu wa Njombe ni wakulima wazuri hivyo watatumia ndege hizo kusafirisha ulanzi

> Pia, amesema atakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Njombe

Soma https://jamii.app/MagufuliMakambako
#Uchaguzi2020
#ZIMBABWE: UPINZANI WADAIWA KUSHIRIKIANA NA NCHI ZA MAGHARIBI KUMPINDUA RAIS MNANGAGWA

> Waziri wa Usalama wa Kitaifa amedai wapinzani nchini humo wanashirikiana na nchi za Magharibi kuingiza silaha kimagendo ili kumuondoa Madarakani Rais wao

Soma https://jamii.app/UasiZimbabwe
#JFLeo
SIKU YA KIMATAIFA YA UELIMISHAJI KUHUSU UPOTEVU WA CHAKULA

> FAO inakadiria hasara ya Tsh. Trilioni 9.28 kila mwaka kwa nchi za Afrika kutokana na upotevu wa chakula

> Upotevu huo hutokana na namna duni ya kuhifadhi chakula kisichokaa muda mrefu

Soma https://jamii.app/ChakulaUN
#JFLeo
UMUHIMU WA KUPIGA KURA KWENYE NCHI YA KIDEMOKRASIA

> Uzuri wa Demokrasia ni pale wale wanaoonekana wachache kupata nafasi ya kufanya maamuzi yao kwa kura

> Demokrasia iliyo hai inaonekana pale Wananchi wanaposhuhudia Serikali waliyoipigia kura inavyoendesha nchi

Soma > https://jamii.app/UmuhimuKupigaKura

#Uchaguzi2020
SHERIA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI NAMBA 6(2010)

> Kifungu cha 24 kifungu kidogo cha 4 kinaeleza kuwa; Iwapo Msajili wa Vyama vya Siasa ataridhika kuwa mgombea ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au chama chake cha siasa kimefanya vitendo vilivyokatazwa na Sheria ambapo kwa hilo mgombea huyo au chama chake kimepoteza sifa ya kushiriki kwenye mchakato wa uteuzi, msajili atafanya yafuatayo:

> (a) Kama ni mgombea, Msajili atakitaarifu chama chake kuteua mgombea mwingine kama mbadala wa huyo aliyekosa sifa

> (c) Kama ni chama, Msajili atakitaarifu chama hicho kuwa kimezuiliwa kumdhamini mgombea ndani ya Kata, Jimbo au nafasi ya Urais

Soma > https://jamii.app/UchaguziGharama

#KemeaRushwa #Uchaguzi2020
NJOMBE: DKT. MAGUFULI NA WAGOMBEA WA CCM WAPIGA MAGOTI KUOMBA KURA

> Walifanya hivyo baada ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya kusema kuwa kwa tamaduni za Njombe ni kawaida watu kuomba vitu wakiwa wamepiga magoti

Fuatilia > https://youtu.be/ZUfImtTVRww

#Uchaguzi2020 #TZ2020 #JamiiForums #JFLeo
SIASA SIO UADUI, LEMA NA GAMBO WAPIGA PICHA YA PAMOJA

> Wagombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo (CCM) na Godbless Lema (CHADEMA) wamepiga picha ya pamoja

> Tukio hili linadhihirisha Siasa sio sababu ya kuchukiana au kutoana uhai

Soma https://jamii.app/SiasaSioUadui
#JFSiasa
KATIBU MKUU WA UN: HATUTAKIWI KUYASAHAU MAISHA YA MTU ALIYETUTOKA

> Antonio Guterres: Dunia haitakiwi kuyasahau maisha ya hata mtu mmoja aliyefariki kutokana na #COVID19

> Hadi sasa vifo vinavyotokana na #CoronaVirus vimezidi watu milioni 1

Soma > https://jamii.app/GuterresCovid19
LIJUE GEREZA AMBALO WAFUNGWA WANAJITAFUTIA CHAKULA

> Gereza la Sanganer lililopo India hutoa sehemu ya kulala tu kwa wafungwa, nao hulazimika kufanya kazi ili kupata mahitaji ya kila siku

> Wanaharakati wanataka magereza kama hayo yaongezeke

Soma https://jamii.app/GerezaSanganer
#JFLeo
PROF. LIPUMBA: MAZINGIRA YA KUFANYIA BIASHARA NI MAGUMU SANA TANZANIA

> Amesema ni kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mazingira ya Kufanya Biashara ya mwaka 2020 ambapo Tanzania ni ya 141 kati ya nchi 190

Soma > https://jamii.app/LipumbaBiasharaTz

#Uchaguzi2020 #TZ2020 #JamiiForums
NEC: WENYE MAHITAJI MAALUM WAMEANDALIWA MAZINGIRA RAFIKI KUSHIRIKI UCHAGUZI

> Watu hao ni Wajawazito, Wanaonyonyesha, Wazee na Walemavu

> Aidha, Wasioona (Wasiotumia Nukta Nundu) na wasiojua kusoma wanaruhusiwa kuwa na wanayemuamini

Soma https://jamii.app/WalemavuUchaguzi

#TZ2020
SEPTEMBA 30, SIKU YA KIMATAIFA YA KUFASIRI

> UN inatambua umuhimu wa kufasiri ktk kuleta mataifa pamoja

> Tamko la Haki za Binadamu Duniani linashikilia rekodi ya kuwa nyaraka iliyofasiriwa zaidi

Soma https://jamii.app/InternationalTranslationDay
#JFLeo
MBEYA: DKT. MAGUFULI AMUOMBA KURA 'SUGU'

> Mgombea huyo amesema, "naomba kura kwa watu wote, hata Sugu ninamuomba kura"

> Ameongeza kuwa, Dhamira yake ni kuibadilisha Mbeya kabla muda wake haujaisha ili liwe Jiji la mfano kitaifa na kimataifa

Soma https://jamii.app/MagufuliSugu

#JFLeo
LISSU: HATUNA MASLAHI NA URAIS ZANZIBAR, NDIO MAANA TUNAMUUNGA MKONO MAALIM SEIF

> Tundu Lissu amesema hawatatangaza Muungano bali wataungana mkono ktk maeneo ambayo hawana maslahi

> Amesema hiyo haikatazwi kisheria kwa kuwa sio Muungano

Soma https://jamii.app/PoliticalCoalition
#JFLeo
DKT. MAGUFULI: HAMKUWA NA MBUNGE WA KUWASEMEA BALI MLIPATA MSANII

> Mgombea Urais wa JMT kupitia CCM amewaambia wananchi wa Mbeya kwamba hawakuwa na Mbunge wa kuwasemea bali walikuwa na Msanii (Sugu) ambaye sio mkali kama Diamond na Alikiba

Soma https://jamii.app/MagufuliSugu
#JFLeo
MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI YASEMA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR UPO KIHALALI

> Wanaharakati walifungua kesi kuhoji uhalali wa Muungano

> Kanuni ilitaka malalamiko yawasilishwe siku 60 tangu tukio lilipotokea lakini imeshapita miaka 56

Soma https://jamii.app/MuunganoTanzania
#JFLeo