JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WFP: WAKIMBIZI WENGI WA #MSUMBIJI WANAKIMBILIA #TANZANIA KUTOKANA NA MAPIGANO

> Makadirio ya Shirika la Chakula Duniani ni kuwa, idadi ya wakimbizi hao ni takriban 1000 ambapo inasemekana baadhi hutumia boti huku wengine wakiogolea Mto Ruvuma

Soma - https://jamii.app/WakimbiziMsumbiji
AMBER RUTY, MUMEWE NA JAMES DELICIOUS WAHUKUMIWA MIAKA 5 JELA

> Wamehukumiwa kifungo hicho au kulipa faini (Amber Rutty milioni. 3, Mume wa Amber milioni. 3 na James milioni. 5)

> Wameshindwa kulipa faini na hivyo kupelekwa gerezani

Soma - https://jamii.app/HukumuAmberRuty
Bodi, Menejimenti na Watendaji wa Jamii Forums tunatuma salamu za pongezi katika maadhimisho ya miaka 25 ya kulinda na kutetea haki za binadamu kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Tunawatakia kila lililo jema katika muendelezo wa kazi zote mnazozifanya.

"Haki ni maendeleo, simamia haki."

#HakiZaBinadamu #JamiiForums #LHRC
DAR: BAADHI YA VIONGOZI WA ACT-WAZALENDO WADAIWA KUCHUKULIWA NA POLISI

> Inaelezwa Arodia Peter, Dotto Rangimoto (Afisa Msaidizi Kitengo cha Habari) na Dahlia Majid, wamechukuliwa na Polisi huku Dotto akituhumiwa kwa Makosa ya Kimtandao

Soma - https://jamii.app/PolisiViongoziACT
UKRAINE: 22 WAFARIKI DUNIA BAADA YA NDEGE YA KIJESHI KUANGUKA

> Watu 27 walikuwemo katika ndege hiyo, wawili wamejeruhiwa vibaya na wengine 3 bado wanatafutwa

> Chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea

Soma - https://jamii.app/UkraineCrash
ACT-WAZALENDO YATAKA POLISI KUWAACHIA MAAFISA WAO

> Imetaka waachiwe bila masharti au wafikishwe Mahakamani kama kuna kosa

> Arodia Peter, Dotto Rangimoto na Dahlia Majid walikamatwa jana katika Ofisi za Chama hicho zilizopo Magomeni

Soma - https://jamii.app/ACTMaafisaPolisi
TOGO: WAZIRI MKUU NA SERIKALI YAKE WAJIUZULU

> Taarifa ya Rais Faure Gnassingbe imesema Komi Klassou amejiuzulu pamoja na Serikali yake

> Kumekuwa na matarajio ya mabadiliko ktk Serikali baada ya Rais huyo kushinda Uchaguzi mapema mwaka huu

Soma https://jamii.app/TogoGovtResigns
SERIKALI: WANANCHI KUWENI MAKINI KABLA YA KUNUNUA MAGARI JAPAN

> Ubalozi wa Tanzania nchini Japan umesema ni vigumu kwa fedha ambayo imeshatumwa kurejeshwa

> Wanaoagiza magari wametakiwa kuangalia tovuti zaidi ya moja kufahamu bei za wastani

Soma https://jamii.app/MagariJapan
KAMATI YA AMANI YAPIGA MARUFUKU NYUMBA ZA IBADA KUTUMIKA KISIASA

> Kamati ya Amani inayoongozwa na Sheikh Mkuu wa Dar imepiga marufuku Makanisa na Misikiti kutumika kumfanyia kampeni mgombea wa kisiasa kwani ni kuwanyima haki waumini

Soma - https://jamii.app/KampeniNyumbaIbada
#Uchaguzi2020
MAUAJI YA WAZEE YAPUNGUA. IMANI POTOFU NI CHANZO KIKUBWA

> Yamepungua kutoka 557 mwaka 2014 hadi 74 mwaka 2019 na mwaka huu idadi inatarajiwa kuwa chini ya 10

> Kipindi cha Uchaguzi hali huwa mbaya hata kwa walemavu kutokana na Imani potofu

Soma https://jamii.app/MauajiWazee
WHO: VIFO VYA #CORONAVIRUS VINAWEZA KUFIKIA MILIONI 2

> WHO imesema takwimu zinaweza kuwa kubwa zaidi kusipokuwa na mpango wa pamoja wa kimataifa

> Hadi sasa vifo 981,548 vimerekodiwa, 22,260,044 wamepona na maambukizi yamefikia 32,164,141

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
ZANZIBAR: KATIBU WA TAWI WA ACT-WAZALENDO AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUWAKATA MAPANGA WANACCM

> Ni Katibu wa Tawi la Kosovo, Shehia ya Kangani, Hassan Hamad Hassan (56) anayeshikiliwa kwa tuhuma ya kuwashambulia kwa mapanga wanachama wa CCM

Soma https://jamii.app/KatibuACTMapanga
#TZ2020
LUKUVI: HAKUNA KIONGOZI ALIYEPORA ARDHI. UMILIKI WA ARDHI HUFUATA SHERIA

> Waziri wa Ardhi amekanusha uvumi huo kutokana na baadhi ya kauli ambazo zimetolewa na viongozi wa Vyama vya Siasa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020

Soma https://jamii.app/ArdhiViongozi
MICHEZO: Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 3 kwa 2 dhidi ya Brighton & Hove Albion

> Mabao ya Man U yamefungwa na Lewis Dunk(aliyejifunga), Rashford na Bruno Fernandes

> Magoli ya Brighton & Hove Albion yamefungwa na Noel Maupay na Solly March

#EPL #BHAMUN
TUNDU LISSU AWAPONGEZA POLISI KWA KUSIMAMIA ULINZI WA MIKUTANO YAKE

> Pia, amesema ktk Uongozi wake kutakuwa na Uhuru kamili wa Vyombo vya Habari na marejesho ya Mikopo kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu itarudi kuwa 3% kama ilivyokuwa mwanzo

Soma https://jamii.app/PongeziPolisi
#TZ2020
DAR: MGOMBEA WA ADC AHIMIZA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

> Akiwa Kinondoni, Queen Cuthbert Sendiga amesema ana uwezo mkubwa wa kusimamia mifumo mizuri ya kuiletea maendeleo Tanzania na kuwaomba wananchi wampigie kura ifikapo Oktoba 28

Soma https://jamii.app/ADC-Dar

#Uchaguzi2020
WAZIRI MKUU MTEULE WA LEBANON AJIUZULU

> Mustapha Adib ameachia madaraka kutokana na kushindwa kuunda Serikali mpya isiyoegemea upande wowote wa kisiasa

> Serikali ya awali ilijiuzulu kufuatia mlipuko mkubwa uliotokea Agosti 04

Soma - https://jamii.app/AdibResigns
PROF. LIPUMBA AAHIDI KUONGEZA MZUNGUKO WA FEDHA

> Mgombea Urais wa CUF amesema Hali ya umasikini inazidi na yeye ndiye mwenye glisi ya kulegeza vyuma vilivyokaza

> Ataboresha huduma kwa Wajawazito ikiwemo wataalam na vifaa tiba vya kutosha

Soma https://jamii.app/MzungukoFedhaLipumba
VISA VYA #CORONAVIRUS VYAFIKIA 32,435,527

> Nchi zilizoathirika zaidi ni Marekani-6,659,143, India-5,992,532, Brazil-4,718,115, Urusi-1,143,571 na Colombia-806,038

> Wagonjwa wapatao 22,450,261 wamepona na vifo vimefikia 986,471

Soma - https://jamii.app/COVID19Updates
ILANI: SERIKALI YA CHADEMA ITAFANYA NINI SIKU 100 ZA MWANZO?

> Itapunguza kiwango cha marejesho ya Mikopo ya Elimu ya Juu hadi 3% ya mshahara

> Itarejesha Uhuru wa Vyombo vya Habari na kufuta sheria zinazokiuka #HakiZaBinadamu nchini

Soma https://jamii.app/IlaniCDM

#Uchaguzi2020