JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
POLEPOLE: TUME YA UCHAGUZI IMEWAPENDELEA UPINZANI

> Msemaji wa CCM, Humphrey Polepole amesema, Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ingefuata Sheria bila kutumia Hekima wagombea wasingerudishwa kwenye Uchaguzi Mkuu

Soma https://jamii.app/PolepoleNEC
#Uchaguzi2020
MANYARA: TAKUKURU YAAGIZA KUONDOLEWA KWA MILANGO 83 YA KITUO CHA AFYA KWA KUKOSA UBORA

> Milango hiyo inayodaiwa kuwa ni mipya ktk kituo cha Hirbada imeonekana kupasuka huku mingine ikiwa imepinda na kuvunjika kabla ya kituo kuanza kutumika

Soma - https://jamii.app/MilangoUbora
FAHAMU SABABU ZA MAMA KUJIFUNGUA MTOTO NJITI

- Umri mdogo wa Mama unaweza kupelekea ajifungue kabla ya miezi tisa kutimia kwasababu maumbile yao yanakuwa hayapo tayari kubeba mtoto

- Magonjwa au maambukizi aliyonayo Mama yanaweza kuathiri ujauzito na kusababisha ajifungue mapema

Soma - https://jamii.app/WatotoNjiti
#JFAfya
LISSU: TUTASHINDA UCHAGUZI HUU, OLE WAO WALIOENGUA WAGOMBEA WETU

> Amesema, Serikali ya CHADEMA haitakaa na mtu ambaye hajachaguliwa na Wananchi

> Amesema, Uchaguzi utarudiwa kwa Majimbo na Kata zote ambazo wagombea wao wameenguliwa

Soma - https://jamii.app/KampeniMisungwi
#Uchaguzi2020
MBEYA: MWALIMU MKUU MBARONI KWA RUSHWA YA NGONO

> Adelhard Mjingo (44) anashikiliwa kwa kuomba rushwa ya ngono kwa Mwanafunzi (14)

> Aliahidi kumsaidia Mtihani wa Darasa la 7 huku akitishia kuwa, akikataa atahakikisha hafaulu

Soma - https://jamii.app/RushwaMwl-MBY

#KemeaRushwa
SHIBUDA: VYAMA VIJENGE HOJA, UONGO WA SIASA HUZAA DHULUMA

> Mwenyekiti huyo wa Baraza la Vyama vya Siasa amesema mfumo wa vyama vingi ni kichocheo cha maendeleo sio mafarakano

> Amewataka wagombea kuepuka kupandikiza chuki ktk taifa

Soma https://jamii.app/ShibudaVyamaHoja

#Uchaguzi2020
MAADILI YA UCHAGUZI: KUKOSOANA KWA WAGOMBEA/VYAMA KUJIKITE KATIKA SERA

> Hairuhusiwi kubeba sanamu/kinyago kinachoonesha kudhalilisha, kebehi au kufedhehesha chama kingine cha siasa, kiongozi wake au Serikali katika mkutano wa kisiasa

Soma - https://jamii.app/MaadiliUchaguzi
#Uchaguzi2020
WFP: WAKIMBIZI WENGI WA #MSUMBIJI WANAKIMBILIA #TANZANIA KUTOKANA NA MAPIGANO

> Makadirio ya Shirika la Chakula Duniani ni kuwa, idadi ya wakimbizi hao ni takriban 1000 ambapo inasemekana baadhi hutumia boti huku wengine wakiogolea Mto Ruvuma

Soma - https://jamii.app/WakimbiziMsumbiji
AMBER RUTY, MUMEWE NA JAMES DELICIOUS WAHUKUMIWA MIAKA 5 JELA

> Wamehukumiwa kifungo hicho au kulipa faini (Amber Rutty milioni. 3, Mume wa Amber milioni. 3 na James milioni. 5)

> Wameshindwa kulipa faini na hivyo kupelekwa gerezani

Soma - https://jamii.app/HukumuAmberRuty
Bodi, Menejimenti na Watendaji wa Jamii Forums tunatuma salamu za pongezi katika maadhimisho ya miaka 25 ya kulinda na kutetea haki za binadamu kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Tunawatakia kila lililo jema katika muendelezo wa kazi zote mnazozifanya.

"Haki ni maendeleo, simamia haki."

#HakiZaBinadamu #JamiiForums #LHRC
DAR: BAADHI YA VIONGOZI WA ACT-WAZALENDO WADAIWA KUCHUKULIWA NA POLISI

> Inaelezwa Arodia Peter, Dotto Rangimoto (Afisa Msaidizi Kitengo cha Habari) na Dahlia Majid, wamechukuliwa na Polisi huku Dotto akituhumiwa kwa Makosa ya Kimtandao

Soma - https://jamii.app/PolisiViongoziACT
UKRAINE: 22 WAFARIKI DUNIA BAADA YA NDEGE YA KIJESHI KUANGUKA

> Watu 27 walikuwemo katika ndege hiyo, wawili wamejeruhiwa vibaya na wengine 3 bado wanatafutwa

> Chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea

Soma - https://jamii.app/UkraineCrash
ACT-WAZALENDO YATAKA POLISI KUWAACHIA MAAFISA WAO

> Imetaka waachiwe bila masharti au wafikishwe Mahakamani kama kuna kosa

> Arodia Peter, Dotto Rangimoto na Dahlia Majid walikamatwa jana katika Ofisi za Chama hicho zilizopo Magomeni

Soma - https://jamii.app/ACTMaafisaPolisi
TOGO: WAZIRI MKUU NA SERIKALI YAKE WAJIUZULU

> Taarifa ya Rais Faure Gnassingbe imesema Komi Klassou amejiuzulu pamoja na Serikali yake

> Kumekuwa na matarajio ya mabadiliko ktk Serikali baada ya Rais huyo kushinda Uchaguzi mapema mwaka huu

Soma https://jamii.app/TogoGovtResigns
SERIKALI: WANANCHI KUWENI MAKINI KABLA YA KUNUNUA MAGARI JAPAN

> Ubalozi wa Tanzania nchini Japan umesema ni vigumu kwa fedha ambayo imeshatumwa kurejeshwa

> Wanaoagiza magari wametakiwa kuangalia tovuti zaidi ya moja kufahamu bei za wastani

Soma https://jamii.app/MagariJapan
KAMATI YA AMANI YAPIGA MARUFUKU NYUMBA ZA IBADA KUTUMIKA KISIASA

> Kamati ya Amani inayoongozwa na Sheikh Mkuu wa Dar imepiga marufuku Makanisa na Misikiti kutumika kumfanyia kampeni mgombea wa kisiasa kwani ni kuwanyima haki waumini

Soma - https://jamii.app/KampeniNyumbaIbada
#Uchaguzi2020
MAUAJI YA WAZEE YAPUNGUA. IMANI POTOFU NI CHANZO KIKUBWA

> Yamepungua kutoka 557 mwaka 2014 hadi 74 mwaka 2019 na mwaka huu idadi inatarajiwa kuwa chini ya 10

> Kipindi cha Uchaguzi hali huwa mbaya hata kwa walemavu kutokana na Imani potofu

Soma https://jamii.app/MauajiWazee
WHO: VIFO VYA #CORONAVIRUS VINAWEZA KUFIKIA MILIONI 2

> WHO imesema takwimu zinaweza kuwa kubwa zaidi kusipokuwa na mpango wa pamoja wa kimataifa

> Hadi sasa vifo 981,548 vimerekodiwa, 22,260,044 wamepona na maambukizi yamefikia 32,164,141

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
ZANZIBAR: KATIBU WA TAWI WA ACT-WAZALENDO AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUWAKATA MAPANGA WANACCM

> Ni Katibu wa Tawi la Kosovo, Shehia ya Kangani, Hassan Hamad Hassan (56) anayeshikiliwa kwa tuhuma ya kuwashambulia kwa mapanga wanachama wa CCM

Soma https://jamii.app/KatibuACTMapanga
#TZ2020
LUKUVI: HAKUNA KIONGOZI ALIYEPORA ARDHI. UMILIKI WA ARDHI HUFUATA SHERIA

> Waziri wa Ardhi amekanusha uvumi huo kutokana na baadhi ya kauli ambazo zimetolewa na viongozi wa Vyama vya Siasa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020

Soma https://jamii.app/ArdhiViongozi