JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AIDAN EYAKUZE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MWENZA WA ASASI ZA KIRAIA KATIKA OGP

> Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mweza wa Asasi za Kiraia katika Open Government Partnership (OGP)

> Muhula wake kwa kushirikiana na Serikali ya Italia utaanza mwaka 2021. Hii ni mara ya pili kwa Tanzania na Twaweza kutoa Mwenyekiti Mwenza

Soma - https://jamii.app/AidanCo-ChairOGP
#CORONAVIRUS-UK: VISA ZAIDI YA 6,600 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

> Visa vipya 6,634 vimerekodiwa, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuripotiwa tangu kuanza kwa mlipuko

> Mapema wiki hii Waziri Mkuu alitangaza masharti mapya ili kudhibiti maambukizi

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
KISUTU, DAR: KESI ZA TUNDU LISSU KUSIKILIZWA BAADA YA UCHAGUZI

> Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Augustina Mmbando amekubali ombi lililowasilishwa na Wakili wa utetezi na kuahirisha kesi hizo hadi Novemba 6 ambapo zitasikilizwa mfululizo

Soma https://jamii.app/LissuKesiNov6
MALI: RAIS WA MPITO KUAPISHWA LEO

> Bah Ndaw (70) ataongoza Serikali ya Mpito kwa miezi 18. Kanali Assimi Goita atakuwa Makamu wa Rais

> Ndaw alikuwa Waziri wa Ulinzi katika utawala wa Rais aliyepinduliwa na Jeshi, Ibrahim Boubacar Keita

Soma - https://jamii.app/RaisMaliKiapo
PROF. LIPUMBA: UCHAGUZI USIWE CHANZO CHA UVUNJIFU WA AMANI

> Mgombea Urais kupitia CUF amesema, Tanzania imekuwa Kisiwa cha Amani kwa kipindi kirefu hivyo watanzania wanao wajibu wa kuhakikisha amani hiyo inadumu hasa kipindi hiki

Soma - https://jamii.app/LipumbaAmaniTZ
#Uchaguzi2020
MUHAS YATAJWA KAMA CHUO NO.1 TANZANIA

> Ni kwa mujibu wa University Ranking by Academic Performance (URAP)

> Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kinashika nafasi ya 1,551 duniani, huku UDSM ikiwa ya 2,047 na SUA 2,206

Soma https://jamii.app/URAPRankings
MAJALIWA: KITI CHA URAIS SIO MCHEZO, KINAHITAJI MTU MAKINI

> Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema, β€œUongozi wa nchi siyo jambo la mchezo, linataka kiongozi makini, anayetetea rasilimali na anayetetea wanyonge dhidi ya rushwa na ufisadi"

Soma https://jamii.app/KitiUraisMajaliwa
#Uchaguzi2020
RASMI: SAMATTA AJIUNGA NA FENERBAHCE YA UTURUKI

> Mbwana Samatta amejiunga na Fenerbahce kwa mkopo wa mwaka mmoja huku Fenerbahce wakieleza kuwa baada ya muda huo wamekubaliana kumpatia Samatta mkataba wa miaka minne

Soma - https://jamii.app/SamattaUsajili
#JFMichezo
POLEPOLE: TUME YA UCHAGUZI IMEWAPENDELEA UPINZANI

> Msemaji wa CCM, Humphrey Polepole amesema, Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ingefuata Sheria bila kutumia Hekima wagombea wasingerudishwa kwenye Uchaguzi Mkuu

Soma https://jamii.app/PolepoleNEC
#Uchaguzi2020
MANYARA: TAKUKURU YAAGIZA KUONDOLEWA KWA MILANGO 83 YA KITUO CHA AFYA KWA KUKOSA UBORA

> Milango hiyo inayodaiwa kuwa ni mipya ktk kituo cha Hirbada imeonekana kupasuka huku mingine ikiwa imepinda na kuvunjika kabla ya kituo kuanza kutumika

Soma - https://jamii.app/MilangoUbora
FAHAMU SABABU ZA MAMA KUJIFUNGUA MTOTO NJITI

- Umri mdogo wa Mama unaweza kupelekea ajifungue kabla ya miezi tisa kutimia kwasababu maumbile yao yanakuwa hayapo tayari kubeba mtoto

- Magonjwa au maambukizi aliyonayo Mama yanaweza kuathiri ujauzito na kusababisha ajifungue mapema

Soma - https://jamii.app/WatotoNjiti
#JFAfya
LISSU: TUTASHINDA UCHAGUZI HUU, OLE WAO WALIOENGUA WAGOMBEA WETU

> Amesema, Serikali ya CHADEMA haitakaa na mtu ambaye hajachaguliwa na Wananchi

> Amesema, Uchaguzi utarudiwa kwa Majimbo na Kata zote ambazo wagombea wao wameenguliwa

Soma - https://jamii.app/KampeniMisungwi
#Uchaguzi2020
MBEYA: MWALIMU MKUU MBARONI KWA RUSHWA YA NGONO

> Adelhard Mjingo (44) anashikiliwa kwa kuomba rushwa ya ngono kwa Mwanafunzi (14)

> Aliahidi kumsaidia Mtihani wa Darasa la 7 huku akitishia kuwa, akikataa atahakikisha hafaulu

Soma - https://jamii.app/RushwaMwl-MBY

#KemeaRushwa
SHIBUDA: VYAMA VIJENGE HOJA, UONGO WA SIASA HUZAA DHULUMA

> Mwenyekiti huyo wa Baraza la Vyama vya Siasa amesema mfumo wa vyama vingi ni kichocheo cha maendeleo sio mafarakano

> Amewataka wagombea kuepuka kupandikiza chuki ktk taifa

Soma https://jamii.app/ShibudaVyamaHoja

#Uchaguzi2020
MAADILI YA UCHAGUZI: KUKOSOANA KWA WAGOMBEA/VYAMA KUJIKITE KATIKA SERA

> Hairuhusiwi kubeba sanamu/kinyago kinachoonesha kudhalilisha, kebehi au kufedhehesha chama kingine cha siasa, kiongozi wake au Serikali katika mkutano wa kisiasa

Soma - https://jamii.app/MaadiliUchaguzi
#Uchaguzi2020
WFP: WAKIMBIZI WENGI WA #MSUMBIJI WANAKIMBILIA #TANZANIA KUTOKANA NA MAPIGANO

> Makadirio ya Shirika la Chakula Duniani ni kuwa, idadi ya wakimbizi hao ni takriban 1000 ambapo inasemekana baadhi hutumia boti huku wengine wakiogolea Mto Ruvuma

Soma - https://jamii.app/WakimbiziMsumbiji
AMBER RUTY, MUMEWE NA JAMES DELICIOUS WAHUKUMIWA MIAKA 5 JELA

> Wamehukumiwa kifungo hicho au kulipa faini (Amber Rutty milioni. 3, Mume wa Amber milioni. 3 na James milioni. 5)

> Wameshindwa kulipa faini na hivyo kupelekwa gerezani

Soma - https://jamii.app/HukumuAmberRuty
Bodi, Menejimenti na Watendaji wa Jamii Forums tunatuma salamu za pongezi katika maadhimisho ya miaka 25 ya kulinda na kutetea haki za binadamu kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Tunawatakia kila lililo jema katika muendelezo wa kazi zote mnazozifanya.

"Haki ni maendeleo, simamia haki."

#HakiZaBinadamu #JamiiForums #LHRC
DAR: BAADHI YA VIONGOZI WA ACT-WAZALENDO WADAIWA KUCHUKULIWA NA POLISI

> Inaelezwa Arodia Peter, Dotto Rangimoto (Afisa Msaidizi Kitengo cha Habari) na Dahlia Majid, wamechukuliwa na Polisi huku Dotto akituhumiwa kwa Makosa ya Kimtandao

Soma - https://jamii.app/PolisiViongoziACT
UKRAINE: 22 WAFARIKI DUNIA BAADA YA NDEGE YA KIJESHI KUANGUKA

> Watu 27 walikuwemo katika ndege hiyo, wawili wamejeruhiwa vibaya na wengine 3 bado wanatafutwa

> Chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea

Soma - https://jamii.app/UkraineCrash