JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
IGP SIRRO: VIJANA MSIKUBALI KUTUMIKA BILA SABABU

> Amesema, zaidi ya watu 40 wanashikiliwa na Polisi Pemba kwa tuhuma za kuwashambulia wafuasi wa CCM kwa mapanga

> Amewataka vijana wasikubali watu wachache kuwaingiza kwenye fujo

Angalia - https://youtu.be/tomQpgGIIt0
#Uchaguzi2020
WANAOWATOZA FEDHA WAJAWAZITO NA WAZEE KWENYE VITUO VYA AFYA KUSHUGHULIKIWA

> Kassim Majaliwa amewataka Watendaji wa Zahanati na Hospitali kuacha kuwatoza fedha wajawazito, watoto chini ya miaka 5 na wazee na wanaofanya hivyo wachukuliwe hatua

Soma https://jamii.app/HudumaBureAfya
#KENYA KUJA NA KANUNI ZA KUWADHIBITI WANASIASA WANAODAIWA KUFANYA UCHOCHEZI

> Wizara ya Usalama wa Ndani iko mbioni kutengeneza kanuni itakayodhibiti ghasia wakati wa Uchaguzi

> Wanaoeneza chuki wadaiwa kuwa kiini cha migawanyiko ya kisiasa

Soma https://jamii.app/KanuniUchocheziKE
DKT. ABBAS: HAKUNA SIRI KATIKA FEDHA ZA MIRADI, ZINAPITISHWA NA BUNGE

> Ameeleza kuwa, fedha zote za miradi zipo kwenye bajeti na zinapitishwa Bungeni kila mwaka

> Amesema fedha za miradi yote inayotekelezwa zimetengwa kwa mujibu wa Sheria

Soma - https://jamii.app/FedhaMiradiSerikali
BOTSWANA KUANZA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI SHULENI

> Waziri wa Elimu ya Msingi, Fidelis Molao amesema Serikali ya #Botswana inakusudia kuanzisha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Shule za Msingi ndani ya siku zijazo

Soma - https://jamii.app/UseSwahiliBotswn
#JFLeo #Swahili
CUF: ADUI WA CUF NI ADUI WA CHADEMA NA ADUI WA CHADEMA NI ADUI WA CUF

> Meneja Kampeni wa CUF akiwa Kagera amesema, wapinzani wanapaswa kujitafakari kwani yawezekana kuna eneo wanapishana lakini lengo lao ni 1, kuiondoa CCM Madarakani

Soma https://jamii.app/CDMCUFKagera
#Uchaguzi2020
LOWASSA: SINA SHAKA NA MAGUFULI KUSHINDA

> Amesema, β€œSina mashaka juu ya Rais Magufuli kushinda, mashaka yangu ni atashinda kwa kura ngapi? Huko wameanza kujipambanua sana, maneno mengi, fujo kwenye TV, tumemwambia usitishike hata kidogo"

Soma - https://jamii.app/LowassaUshindiCCM
#TZ2020
UMOJA WA ULAYA WASEMA LUKASHENKO SIO RAIS HALALI WA BELARUS

> Umoja huo umesema, uapisho wake umekosa uhalali wa kidemokrasia na unapingana na idadi kubwa ya wananchi ambao wamekuwa wakiandamana tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti

Soma - https://jamii.app/EUBelarus
FAHAMU KUHUSU WATOTO NJITI (PREMATURE BABIES) - 1

> Watoto njiti ni wale ambao huzaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito

> Inakadiriwa watoto Milioni 15 huzaliwa kabla ya muda kila mwaka duniani, ikimaanisha kati ya watoto 10 mtoto 1 ni njiti

> Mtoto anapozaliwa kabla ya muda, baadhi ya viungo vyake vinakuwa havijakomaa ipasavyo

Soma - https://jamii.app/WatotoNjiti
SERIKALI YA TANZANIA IMEKANUSHA TUHUMA ZA KUWALAZIMISHA WAKIMBIZI KUONDOKA

> Serikali imekanusha tuhuma zilizotolewa na Waziri wa Masuala ya Wakimbizi Nchini #Uganda kuhusu kuwalazimisha Wakimbizi waliopo Nchini kurejea #Burundi bila ridhaa yao

Soma - https://jamii.app/WakimbiziTZ
MGOMBEA AFUKUZWA NA WANANCHI WAKATI AKIOMBA KURA

> Jasson Rweikiza ambaye ni Mgombea Ubunge Jimbo la Bukoba Vijiji (CCM), amefukuzwa na Wanachi wakati akiomba Kura

> Rweikiza alikuwa Mbunge (2015-2020) na sasa anatetea nafasi hiyo

Angalia - https://www.youtube.com/watch?v=zpw4HpT1Y_M
#Uchaguzi2020
ACT-WAZALENDO YAMJIBU MSAJILI: HATUJAUNGANA NA CHADEMA

> Kimesema kauli na imani ya Maalim Seif kuwa Lissu atakuwa Rais wa JMT haimaanishi wameungana bali wana imani ya pamoja kuwa Mgombea wa CCM hatokuwa Rais baada ya Oktoba 28

Soma - https://jamii.app/MsajiliMaelezoACT

#Uchaguzi2020
BoT YAWAFIKISHA 10 MAHAKAMANI KWA KUTENGENEZA NA KUSAMBAZA NOTI BANDIA

> Imeeleza wasiwasi wake kuhusu wahalifu kulenga minada ya mifugo na mazao

> Hii ni mara ya pili kwa BoT kuonya kuhusu mzunguko wa noti bandia katika kipindi cha mwaka 1

Soma https://jamii.app/FakeNotesBoT
MABAHARIA WANAWAKE WAHIMIZA WASICHANA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

> Ni siku ya leo katika kusherekea Siku ya Mabaharia Duniani

> Kampeni ya kuhamasisha itafanyika katika Kanda za Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa

Soma - https://jamii.app/MabahariaKike
MICHEZO: SAMATTA AWASILI UTURUKI, MAZUNGUMZO NA FENERBAHCE YANAENDELEA

> Mbwana Samatta amesema mazungumzo na Klabu hiyo yanaendelea na hawajasaini hadi sasa

> Januari mwaka huu, Mtanzania huyo alijiunga na Aston Villa akitokea Genk

Soma - https://jamii.app/SamattaUsajiliUturuki

#JFMichezo
#COVID19 KENYA: MAAFISA WA SERIKALI WAHUSISHWA KWENYE KASHFA YA UFISADI

> Serikali ilipokea msaada wa takriban Dola Bil. 2 ili kupambana na mlipuko huo

> Wachunguzi wanatarajia kupendekeza Maafisa na Wafanyabiashara takriban 15 kushtakiwa

Soma https://jamii.app/CovidCorruptionKE
AIDAN EYAKUZE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MWENZA WA ASASI ZA KIRAIA KATIKA OGP

> Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mweza wa Asasi za Kiraia katika Open Government Partnership (OGP)

> Muhula wake kwa kushirikiana na Serikali ya Italia utaanza mwaka 2021. Hii ni mara ya pili kwa Tanzania na Twaweza kutoa Mwenyekiti Mwenza

Soma - https://jamii.app/AidanCo-ChairOGP
#CORONAVIRUS-UK: VISA ZAIDI YA 6,600 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

> Visa vipya 6,634 vimerekodiwa, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuripotiwa tangu kuanza kwa mlipuko

> Mapema wiki hii Waziri Mkuu alitangaza masharti mapya ili kudhibiti maambukizi

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
KISUTU, DAR: KESI ZA TUNDU LISSU KUSIKILIZWA BAADA YA UCHAGUZI

> Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Augustina Mmbando amekubali ombi lililowasilishwa na Wakili wa utetezi na kuahirisha kesi hizo hadi Novemba 6 ambapo zitasikilizwa mfululizo

Soma https://jamii.app/LissuKesiNov6
MALI: RAIS WA MPITO KUAPISHWA LEO

> Bah Ndaw (70) ataongoza Serikali ya Mpito kwa miezi 18. Kanali Assimi Goita atakuwa Makamu wa Rais

> Ndaw alikuwa Waziri wa Ulinzi katika utawala wa Rais aliyepinduliwa na Jeshi, Ibrahim Boubacar Keita

Soma - https://jamii.app/RaisMaliKiapo