JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
IVORY COAST: RAIS WA ZAMANI ATAKA WANANCHI KUPINGA RAIS WA SASA KUWANIA MUHULA WA 3

> Konan Bedie ni miongoni mwa wanaompinga Rais Alassane Ouatarra (78)

> Tume ya Uchaguzi imewaondoa wagombea 40 akiwemo Rais wa zamani, Laurent Gbagbo

Soma https://jamii.app/ElectionsIvoryCoast
CUF: KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI

> Mwenyekiti CUF Wilayani Chakechake Pemba amesema, hawako tayari kufanya fujo wala ghasia kwa kuwaandamanisha vijana

> Ameongeza, hiyo ndio tofauti kubwa kati yao (CUF) na vyama vingine

Soma https://jamii.app/UchaguziAmani
SEPTEMBA 21: MAADHIMISHO YA SIKU YA AMANI DUNIANI

> Ni siku ya kuimarisha amani ktk nchi, kati ya mataifa na kwa wananchi

> Kaulimbiu ni "Kujenga Amani Pamoja" na Watu wametakiwa kusherehekea kwa kuwa wakarimu na kusambaza matumaini

Soma https://jamii.app/PeaceDay2020

#WorldPeaceDay
SIMIYU: CHEYO (UDP) ATOA WITO KWA WANANCHI KUMCHAGUA DKT. MAGUFULI (CCM)

> Amesema, Chama hicho kinamuunga mkono Mgombea Urais wa CCM kutokana na jitihada zake kwenye kuwasikiliza wananchi wakiwemo wanasiasa kutoka Vyama vya Upinzani

Soma - https://jamii.app/CheyoKuraMagufuli

#Uchaguzi2020
KESI YA JAMIIFORUMS: HUKUMU KUTOLEWA OKTOBA 30

> Kesi namba 458 ya mwaka 2016 imeendelea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar

> Hakimu Huruma Shaidi amepanga kutoa hukumu ya shauri hili tarehe 30 Oktoba 2020

Soma https://jamii.app/JFKesiHukumu
DKT. MAGUFULI: KUNA CHAMA KINA SERA YA KUTENGENEZA MAJIMBO, HUO NDIO MWANZO WA MFARAKANO

> Mgombea Urais wa CCM amesema, wananchi wasikubali kuingizwa kwenye uongozi wa majaribio kwasababu wanaosema hivyo wana lengo la kuvuruga nchi

Soma - https://jamii.app/MagufuliMajimbo
#Uchaguzi2020
#CORONAVIRUS-UGANDA: SHULE NA VYUO VIKUU KUFUNGULIWA OKTOBA 15

> Rais Yoweri Museveni ametangaza kuwa Shule na Taasisi za Elimu ya Juu zitafunguliwa tena kuanzia tarehe 15 Oktoba na mikakati imewekwa kuhakikisha wanafunzi wanakuwa salama

Soma - https://jamii.app/UGSchoolOpen
FAHAMU ILANI YA CUF INASEMAJE KUHUSU MSINGI WA KATIBA KATIKA UONGOZI

> Mchakato wa uandaaji wa #Katiba utafufuliwa katika kipindi cha miezi 3 baada ya Serikali kuapishwa kwa kuboresha Rasimu ya Katiba ya Tume ya Jaji Warioba

Fahamu zaidi - https://jamii.app/IlaniCUF
#Uchaguzi2020
MALEZI: TABIA ZA WAZAZI ZINAZOWEZA KUSABABISHA WATOTO KUTOFANIKIWA

> Wazazi wasiowahamasisha watoto kujitegemea. Wazazi wanapaswa kufanya hivi kwani inasaidia Mtoto kujua mabaya na mazuri anapokutana na vishawishi

> Wazazi wanaokaripia watoto wao mara kwa mara. Kumkaripia, kumtukana, kumsema kwa kejeli humfanya Mtoto kuwa muoga wa kila kitu

> Tabia ya kutaka kujua kila kinachoendelea. Kuendesha kila kitu cha Mtoto kutampelekea kuwa na wasiwasi, hatoweza kufanya uamuzi bila Mzazi

Soma - https://jamii.app/TabiaWazaziWatoto
TUNDU LISSU: NITABADILI MFUMO WA UTAWALA KUPITIA MABADILIKO YA KATIBA

> Amesema "Uchaguzi huu tunahitaji kufanya Mabadiliko na moja ni manyanyaso ya wananchi kuuziwa Vitambulisho vya wajasiriamali. Kwanini muuziwe vitambulisho?"

Soma - https://jamii.app/LissuNyakanazi
#Uchaguzi2020
CHAMA CHA ADC KINAENDELEA NA KAMPENI MKOANI TANGA

> Mgombea Urais wa Chama hicho, Queen Cuthbert Sendiga leo anaendelea na kampeni zake Wilayani Kilindi ktk Kata za Songe, Madoti, Kwamwambe, Mafisa, Kisangasa na Kwadiboma

Soma - https://jamii.app/ADCTanga

#Uchaguzi2020 #TZ2020
KENYA: WALIMU WATAKIWA KUFIKA SHULENI SEPTEMBA 28

> Tume ya Elimu kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Mitaala (KICD) imependekeza Shule kufunguliwa Oktoba

> Waziri wa Elimu amesema tarehe rasmi itatangazwa baada ya Kamati kufanya mazungumzo

Soma - https://jamii.app/WalimuShuleKE
INDIA: WATU 10 WAFARIKI BAADA YA JENGO KUPOROMOKA

> Jengo hilo liliwekwa katika orodha ya majengo hatari na taarifa ya wakazi kuondolewa ilitolewa

> Watu 20 hadi 25 wanahofiwa kukwama chini na jitihada za uokoaji zinaendelea

Soma - https://jamii.app/BuildingCollapseIndia
FAHAMU ILANI YA CHADEMA INASEMA NINI KUHUSU UHURU WA KUJIELEZA

> Itahakikisha Sheria zote zinazokandamiza uhuru wa habari zitafutwa na kila mwananchi atakuwa huru

> Itachunguza matukio ya vifo na utekaji wa waandishi wa habari

Zaidi, soma https://jamii.app/IlaniCDM
#Uchaguzi2020
ILANI YA ACT-WAZALENDO INASEMAJE KUHUSU UHURU WA KUJIELEZA?

> Ndani ya siku 100 za kwanza itafuta Sheria zote zinazobana, kuminya na kufifisha haki/uhuru wa kujieleza

> Itatengeneza majukwaa na mifumo itakayowawezesha Watu kutoa maoni

Soma - https://jamii.app/IlaniACT
#Uchaguzi2020
RUVUMA: WATU 71 WANYWA TOGWA INAYODHANIWA KUWA NA SUMU, WANUSURIKA KIFO

> Ni ktk sherehe ya kidini ijulikanayo kama Sadaka. Baadhi wamesema walianza kuharisha na kutapika baada ya kuinywa

> Mkuu wa Wilaya amepiga marufuku togwa kwenye sherehe

Soma https://jamii.app/TogwaSumuRVM
SHERIA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI

Kwa mujibu wa kifungu cha 23 kifungu kidogo cha 7; ni jukumu la Serikali kuhakikisha kuwa njia za usafirishaji zinakuwepo kwa wapiga kura wote ambao wanahitaji kufika kwenye vituo vyao vya kupigia kura

Soma => https://jamii.app/GharamaUchaguzi

#KemeaRushwa
ACT-WAZALENDO YAMUUNGA MKONO MGOMBEA URAIS WA CHADEMA

- Akifanya Kampeni Jimbo la Donge leo, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad amemuidhinisha Tundu Lissu kuwa Mgombea wao wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Soma - https://jamii.app/MaalimLissuUrais
#Uchaguzi2020
MEMBE: MIMI NDIYE MGOMBEA URAIS KUPITIA ACT-WAZALENDO

> Bernard Membe amekanusha taarifa za kuwa wamejiunga na CHADEMA katika ngazi ya Urais

> Amesema yeye ndiye aliyekabidhiwa Ilani ya Chama ili kuinadi kote nchini kwenye Uchaguzi

Soma https://jamii.app/MembeACT-CDM

#Uchaguzi2020
MAREKANI YAITAKA KENYA KUIUNGA MKONO ISRAEL HADHARANI

> Nchi hiyo imesema hakutakuwa na Makubaliano ya Biashara Huria (FTA) Kenya isipofanya hivyo

> Vilevile, imeitaka Kenya kukemea vitendo vinavyoathiri biashara kati ya Marekani na Israel

Soma https://jamii.app/USKenyaFTA