JamiiForums
52.8K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ILANI YA CHAUMMA INASEMAJE KUHUSU KATIBA MPYA?

> Itahakikisha Rasimu ya #Katiba inarejeshwa kama ilivyopendekezwa na wananchi

> Itaweka misingi ya Mgawanyo wa Mamlaka ktk Mihimili ya Dola itakayoondoa utaratibu wa Mihimili kuingiliana

Soma - https://jamii.app/IlaniCHAUMMA
#TZ2020
MGAYWA (SAU): KILA MTANZANIA ATAPEWA KIPANDE CHA ARDHI NA KIWANJA

> Mgombea huyo amesema, kodi ya kiwanja haitakuwepo kuanzia tarehe 28 atakapokuwa Rais

> Ameongeza, ardhi ni mali ya Wananchi isipokuwa iko chini ya udhamini wa Rais

Soma - https://jamii.app/SAUViwanjaBure

#Uchaguzi2020
SHINYANGA: BINTI WA DARASA LA 5 AOZESHWA KWA NG'OMBE 8 NA TSH. LAKI 6

> Watu 4 wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumuozesha Mwanafunzi kwa tamaa ya mali

> Mwanafunzi huyo amekabidhiwa ktk kituo cha kulelea watoto ili aendelee na masomo

Soma https://jamii.app/NdoaMwnf5
ILANI YA NCCR-MAGEUZI INASEMAJE KUHUSU KATIBA MPYA?

> Itakamilisha mchakato wa kupata #KatibaMpya kupitia Bunge la Katiba kwa kujumuisha makundi yote

> Ukiukaji wa #Katiba utakuwa kosa la jinai na Rais atapunguziwa madaraka yake

Soma - https://jamii.app/IlaniNCCR
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI AAGIZA ELIMU YA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI ITOLEWE

> Amesema Vitambulisho havilazimishwi kwa wafanyabiashara na vinatolewa ili wenye biashara ndogondogo waweze kufanya biashara mahali popote nchini bila kusumbuliwa

Angalia https://youtu.be/IQ1YPihUZc0
#Uchaguzi2020
KUKWAMA KWA SHERIA YA JINSIA: RAIS WA KENYA ASHAURIWA KUVUNJA BUNGE

> #Katiba ya #Kenya inataka Sheria hiyo kuwepo ili kudhibiti jinsia kutotawala ktk nyadhifa za uteuzi na kwa miaka 10 sasa Wabunge ambao wengi ni wanaume, wameshindwa kuipitisha

Soma - https://jamii.app/JinsiaBungeniKE
FAHAMU BAADHI YA MAKOSA YA UCHAGUZI

> Kifungu cha 92 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343: Ni kosa kutoa ushahidi/maelezo ya uongo

> Kifungu cha 93: Ni kosa kutoa siri inayohusu Mgombea/mchakato unaoendelea ktk Kituo cha Kupigia Kura

Soma https://jamii.app/MakosaUchaguzi
MALI: WAZIRI WA ZAMANI ATEULIWA KUWA RAIS WA MPITO

> Bah Ndaw atangazwa kama Rais wa Mpito, naye Kanali Goita aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi atakuwa Makamu wa Rais

> ECOWAS imekuwa ikiwashinikiza Wanajeshi kurudisha madaraka kwa raia

Soma - https://jamii.app/NdawRaisMali
FACEBOOK YATUHUMIWA KUINGILIA FARAGHA ZA WATUMIAJI WA INSTAGRAM KUPITIA KAMERA ZA SIMU

> Mlalamikaji Brittany Conditi amesema Facebook inatumia kamera za iPhone ili kukusanya taarifa za watumiaji ambazo hawawezi kuzikusanya kwa njia nyingine

Soma - https://jamii.app/FBSpyIstagram
DKT. MAGUFULI: MIMI BADO NI RAIS, NAAGIZA BARABARA YA ITIGI IJENGWE NA HII SIO HONGO

> Amempa maagizo Meneja wa TANROADS-Singida kutangaza tenda ya ujenzi wa barabara ya KM 10 na fedha za ujenzi atazitoa yeye mwenyewe (Magufuli)

Angalia - https://jamii.app/MagufuliItigi
#Uchaguzi2020
CHINA: MKOSOAJI MKUBWA WA RAIS AHUKUMIWA MIAKA 18 KWA UFISADI

> Ren Zhiqiang amekutwa na hatia ya ufisadi, rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma

> Inadaiwa alikiri makosa yote kwa hiari yake na hatokata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa

Soma- https://jamii.app/RenZhiqiangCH
TUNDU LISSU: UTAWALA WA MAJIMBO NI KUACHA MAMLAKA KWA WANANCHI

> Amesema mpango huo unalenga kuacha mamlaka ya kuendesha mambo yote ktk Jimbo yafanywe na viongozi waliochaguliwa kama ilivyo kwa nchi zote zinazotaka wananchi wawe na mamlaka

Soma - https://jamii.app/LissuKaragwe
ZANZIBAR: WANASIASA WALAANI TUKIO LA WANANCHI KUVAMIWA KISIWANI PEMBA

> Vyama 6 vimemuomba IGP kwenda na watu wake Pemba kutokana na baadhi ya wananchi kuvamiwa alfajiri ya leo wakati wanataka kuingia Msikitini na kukatwa na mapanga

Soma - https://jamii.app/VuruguPemba
#CORONAVIRUS: UINGEREZA YATANGAZA MASHARTI ZAIDI KUDHIBITI MAAMBUKIZI

> Kuanzia Jumatatu ijayo, watu 15 wataruhusiwa kwenye sherehe na 30 kwenye misiba

> Serikali haitaruhusu mashabiki wa michezo viwanjani kuanzia Oktoba 01

Soma - https://jamii.app/MashartiCoronaUK
SHERIA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI NAMBA 6 (2010)

> Je, wajua vitendo vilivyokatazwa na Sheria ambavyo vinapelekea mgombea au chama kupoteza sifa ya kushiriki kwenye mchakato wa uteuzi au uchaguzi?

Kuvifahamu, ingia > https://jamii.app/UchaguziGharama

#KemeaRushwa #Uchaguzi2020
ZITTO: OKTOBA 3 TUTATANGAZA NI NANI ATASIMAMA KUWA MGOMBEA WA URAIS

> Kiongozi wa ACT-Wazalendo amesema, ktk mkutano wa hadhara utakaohusisha CHADEMA, ACT na Vyama vingine vya Upinzani watatangaza ni nani atasimama kama Mgombea Urais

Soma - https://jamii.app/MgombeaUpinzani
#Uchaguzi2020
NIGER: SERIKALI YAAHIRISHA KUFUNGUA SHULE KUTOKANA NA MAFURIKO

> Idadi kubwa ya wahanga wamepatiwa hifadhi mashuleni. Mamlaka zinasema muda zaidi unahitajika kuwahamisha

> Mafuriko hayo yamesababisha vifo 70 na kupelekea mamia kukosa makazi

Soma https://jamii.app/ShuleNiger
MGOMBEA URAIS WA ADC AAHIDI KUBORESHA SEKTA ZA MADINI NA AFYA

> Kwenye madini, Queen Sendiga ameahidi kuondoa tozo zisizomsaidia mchimbaji mdogo

> Amesema, ataboresha Mfumo wa Afya kwa kuhakikisha Mtanzania anatibiwa magonjwa yote kwa bima

Soma - https://jamii.app/ADCKampeniHandeni
AFRIKA KUSINI: RAIS RAMAPHOSA AITAKA DUNIA KUISAIDIA AFRIKA

> Ametoa wito kwa mataifa kuliunga mkono Bara hilo ili lijenge upya uchumi ulioathiriwa na #COVID19

> Amesema, Afrika inahitaji msaada kwa ajili ya kusaidia uchumi (Stimulus package)

Soma https://jamii.app/AfrikaMsaadaUchumi
NYAHOZA: UONGO UNAWEZA KUSABABISHA MADHARA KWA CHAMA KINACHOONGELEWA VIBAYA

> Msajili atatakiwa kuonya na kutoa adhabu kwa Chama/Mgombea ikiwa Sheria itakiukwa, na faini ni kati ya Tsh. Mil. 10 na Mil. 50 au kukisimamisha Chama kufanya siasa

Soma https://jamii.app/MsajiliSheriaKampeni