JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MEMBE KUTAMBULISHWA KESHO KUWA MWANACHAMA WA ACT-WAZALENDO

> Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Julai 16, 2020 watamtambulisha rasmi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe kuwa mwanachama rasmi wa chama hicho

> Membe alifukuzwa CCM akidaiwa kukiuka baadhi ya taratibu za chama

Soma - https://jamii.app/MembeACT
DAR: WALINZI 8 NA WATU 12 WAFIKISHWA KISUTU KWA UHUJUMU UCHUMI

> Walinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Security Group ya Afrika (SGA) wamefikishwa Mahakama ya Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 3 likiwemo la wizi na utakatishaji fedha zaidi ya Tsh. Bilioni 2 mali ya NMB Benki

Soma - https://jamii.app/UhujumuWalinziNMB
MALEZI: WATOTO WANAOANGALIA SANA TV HUWEZA KUHARIBU MIUNDO YA UBONGO

> Wataalamu toka Chuo Kikuu cha Tohoku, Japan wanasema kuangalia Televisheni ni tofauti na kujifunza muziki au kusoma vitabu kwani 'uzoefu' ktk kuangalia Televisheni hakuongezi bali hufinyanga miundo ya Ubongo inayohusika na ufahamu

> Tafiti zinaonesha Televisheni ni mojawapo ya vitu vinavyochangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili ktk jamii

Soma - https://jamii.app/RuningaWatoto
UTEUZI: RAIS MAGUFULI ATEUA WAKUU WA MIKOA DAR, MANYARA

> Amemteua aliyekuwa Katibu Tawala wa Dar, Aboubakar Kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa huo akichukua nafasi ya Paul Makonda

> Aidha, amemteua Joseph Mkirikiti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara akichukua nafasi ya Alexander Mnyeti

Soma https://jamii.app/NewRCDar
ZAMBIA: SERIKALI YAKANUSHA MADAI KUHUSU RAIS EDGAR LUNGU KUFADHILI WAASI RWANDA

-Ni baada ya aliyekuwa Msemaji wa Kundi la waasi la FNL kusema hivyo Mahakamani

- Msemaji wa Rais, Isaac Chipampe amepinga madai hayo akisema hayana ukweli wowote

Soma https://jamii.app/RaisUfadhiliWaasi
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
JE, CCM WATASIMAMIA KAULI HII?

> Kwenye video hii Ndg. Humphrey Polepole ananukuliwa akisisitiza kuwa Wakuu wa Mikoa wasithubutu kutafuta Ubunge (akiitumia Kigamboni kama mfano)

> Anasisitiza ukiteuliwa kuwa RC uwe na nidhamu na adabu!
MAHAKAMA YA AFRIKA: TANZANIA ITOE RUHUSA MATOKEO YA KURA ZA URAIS KUPINGWA

> Mahakama imesema Ibara ya 41(7) ya Katiba inayokataza matokeo ya urais kupingwa Mahakamani inakiuka Ibara ya 1,2, 7(1)(a) ya Mkataba wa Afrika wa #HakiZaBinadamu

Soma - https://jamii.app/ViolationConstitution
SALMA KIKWETE ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MCHINGA

- Salma Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete amechukua fomu hiyo kupitia CCM

- Itakumbukwa Machi 2017, aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Tanzania

Soma https://jamii.app/SalmaKikweteUbungeMchinga
#Uchaguzi2020
MAJI YAONGEZEKA ZIWA VICTORIA, MAFURIKO YAWAKUMBA WANANCHI

> Inaelezwa Ziwa hilo ambalo ni kubwa barani Afrika lilianza kuongezeka maji tangu Oktoba 2019

> Moja ya sababu ni kuwa Ziwa hilo hukusanya maji ya mito 23 na mingine inatoka mbali

Soma - https://jamii.app/MajiZiwaVictoria
SERIKALI: TUNALINDA HAKI ZA WASANII. FAMILIA ZA MAJUTO NA KANUMBA ZIMELIPWA

> Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema β€œFamilia ya Mzee Majuto mpaka sasa tumewarejeshea Tsh. Milioni 65 na familia ya Steven Kanumba tumeirejeshea Tsh. Milioni 20 kutoka katika mikataba ya kazi waliyokuwa wameingia"

Soma - https://jamii.app/FedhaMajutoKanumba
#CORONAVIRUS: KENYA YAREKODI VISA VIPYA ZAIDI YA 400 KWA SIKU 2 MFULULIZO

- Visa 497 viliripotiwa jana, na vingine 461 vimetangazwa leo. Maambukizi nchini humo yamefikia 11,252

- Wagonjwa 3,068 wamepona na 209 wamefariki dunia

Soma - https://jamii.app/Corona11252-KE
#JFCOVID19_Updates
TAKUKURU YAKOSA USHAHIDI WA TUHUMA ZA RUSHWA DHIDI YA LUSINDE

> TAKUKURU imemsafisha aliyekuwa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde baada ya kukosa uthibitisho kuhusiana na tuhuma za kutoa rushwa kwa wajumbe 20 ili kusaidiwa kwenye mchakato wa Uchaguzi

Soma https://jamii.app/TakukuruLusinde
#KemeaRushwa
MICHUANO YA KOMBE LA DUNIANI 2022 KUFANYIKA NOVEMBA NA DESEMBA

> Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limesema michuano hiyo inayotarajiwa kuchezwa nchini #Qatar itachezwa kipindi hicho kutokana na kuwepo kwa joto kali kwenye kipindi cha kawaida yaani Juni na Julai kwenye Ukanda wa nchi za Uarabuni

Soma - https://jamii.app/WorldCup2022
#JFSports
#CORONAVIRUS-BANGLADESH: MMILIKI WA HOSPITALI ATUHUMIWA KUTOA MAJIBU FEKI

- Mohammad Shahed anashikiliwa na Polisi baada ya kutuhumiwa kutoa majibu feki kwa wagonjwa

- Pia, anatuhumiwa kuwatoza fedha wagonjwa kwa ajili ya vyeti na matibabu

Soma https://jamii.app/CoronaFakeResults
KATAVI: MUME AMCHINJA MKEWE KWA MADAI YA KUNYIMWA UNYUMBA KILA SIKU

> Dalali Malongo (20) Mkazi wa Kijiji cha Mipanga ameuawa kwa kuchinjwa na Kisabo Joseph baaada ya kukasirishwa na kitendo cha mke wake kumnyima tendo la ndoa kwa muda mrefu

> Hali hiyo ilipelekea kuhisiwa kuwa na mahusiano na Mwanaume mwingine

Soma - https://jamii.app/UnyumbaMauaji
MKENYA ATEULIWA KUWA KATIBU WA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI (IMF)

- Ceda Ogada ametangazwa kuwa Katibu mpya Shirika hilo, na ataanza kazi Septemba 01, 2020

- Taarifa ya IMF imesema raia huyo wa Kenya anachukua nafasi ya Jianhai Lin aliyestaafu

Soma - https://jamii.app/CedaOgadaIMF
IKULU, DODOMA: RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI WATEULE

> Viongozi wanaosubiri kuapishwa ni pamoja na Aboubakar Kunenge anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar

> Joseph Mkirikiti anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara na Paulo Mshimo Makanza, Katibu Tawala Dar

Fuatilia - https://jamii.app/UapishoRCDar
RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI

- Uapishaji huo unafanyika Ikulu, Chamwino-Dodoma

Fuatilia mubashara; https://youtu.be/p2XPQARf-dA
JAJI MFAWIDHI SALVATORY BONGOLE AFARIKI DUNIA

- Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, Salvatory Bongole amefariki dunia baada ya kuugua ghafla

- Taarifa za kifo chake zimetolewa na Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Hamis Juma

Soma - https://jamii.app/JajiBongoleAfariki
AKAUNTI ZA WATU MAARUFU WAKIWEMO BILL GATES NA ELON MUSK ZADUKULIWA TWITTER

- Akaunti za Gates, Musk zilituma ujumbe kuwataka watu kutuma Dola 1,000 na kusema watapata Dola 2,000

- Wengine waliokutwa na udukuzi huo ni pamoja na Barack Obama na Kanye West

Soma https://jamii.app/TwitterHacked