JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: BERNARD MEMBE APOKELEWA ACT WAZALENDO

- Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mwanachama wa CCM, amejiunga na Chama cha ACT Wazalendo na kupokelewa leo

Fuatilia > https://youtu.be/JE4BTVBa-Jg
ISRAELI WAFANYA MAANDAMANO KUMTAKA NETANYAHU AJIUZULU

> Waandamanaji hao wamesema Benjamin Netanyahu anapaswa kujiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu na kuachana kabisa na siasa kwani anakabiliwa na tuhuma nyingi za ufisadi na Serikali yake imeshindwa kukabiliana na virusi vya Corona

Soma - https://jamii.app/NetanyahuProtests
MAREKANI YATANGAZA MARUFUKU YA KUSAFIRI KWA WAFANYAKAZI WA HUAWEI

> Marekani imetangaza vikwazo katika utoaji vibali vya safari (Visa) kwa baadhi ya wafanyakazi wa Makampuni ya teknolojia kutoka China ikiwemo Huawei kutokana na baadhi yao kujihusisha katika ukiukwaji wa #HakiZaBinadamu

Soma - https://jamii.app/VisaRestrictionsHuawei
MALAWI YAFUATA NYAYO ZA TANZANIA. YAANZA MAOMBI DHIDI YA #COVID19

> Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera ametangaza maombi ya siku 3 kuanzia leo, Julai 16 na yatamalizika Julai 18 na siku ya Jumapili, Julai 19 wananchi watashiriki kutoa shukrani kwa Mungu kwa mambo aliyolifanyia Taifa hilo

Soma - https://jamii.app/MaombiCoronaMalawi
UPDATE: MTOTO WA NELSON MANDELA, ZINDZI MANDELA ALIKUWA NA #CORONAVIRUS

- Mtoto wa Zindzi, Zondwa Mandela amesema ni kweli mama yake alikutwa na #COVID19

- Amesema hawajui alipopata ugonjwa huo na familia yake inasubiri ripoti ya uchunguzi

Soma - https://jamii.app/ZindziMandelaDies
RUSHWA IMEBADILIKA, MBINU ZA KUKABILIANA NAYO NAZO NI LAZIMA ZIBADILIKE

> Uwazi na Haki ya Kupata Taarifa ni silaha kubwa za kupambana na rushwa na ufisadi. Uwazi una nafasi kubwa ya kusaidia katika vita vya kukomesha rushwa

Soma > https://jamii.app/MbadilikoRushwa

#KemeaRushwa
ABDALLAH ZOMBE ACHUKUA FOMU SONGEA MJINI

- Aliyekuwa RCO wa Dar, Abdallah Zombe amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania Ubunge kwa tiketi ya CCM

- Mwaka 2006 aliunganishwa kwenye kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini

Soma - https://jamii.app/AbdallahZombeUbunge
IRAN: KAMPENI YA MTANDAONI YAPELEKEA MAHAKAMA KUFIKIRIA KUSITISHA ADHABU YA KIFO

- Amirhossein Moradi, Mohammad Rajabi na Saeed Tamjidi walikamatwa na Polisi Novemba mwaka 2019 katika maandamano ya kupinga Serikali kupandisha bei ya Petroli

Soma - https://jamii.app/IranExecutions
MAALIM SEIF: BERNARD MEMBE ANAOGOPWA, ACT IMEOKOTA KITU CHA THAMANI

> Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema β€œMembe wanampenda wengi. Wanamfahamu uwezo wake, ujuzi wake na wanamfahamu uadilifu wake, wengi watamfuata. Membe ni maarufu na ndio maana wanamuogopa"

Soma - https://jamii.app/MaalimACTMembe
#CORONAVIRUS KENYA: VISA 241 VYAONGEZEKA, MAAMBUKIZI YAFIKIA 11,673

- Sampuli 3,895 zimefanyiwa vipimo ndani ya saa 24 zilizopita

- Jumla ya vifo 217 vimerekodiwa na waliopona wamefikia 3,638 baada ya wagonjwa 58 kuruhusiwa

Soma - https://jamii.app/Corona11673-KE
#JFCOVID19_Updates
SABABU GANI HUPELEKEA WATU WENGI KUCHELEWA KUJENGA NYUMBA ZAO?

> Wadau ndani ya JamiiForums.com wanajadili na kusema kuwa watu wengi wanaogopa kujenga wakisubiri wawe na pesa nyingi ndio waanze ujenzi

> Wengine huchelewa kwa kukwamishwa na mazingira. Gharama za ujenzi mjini au kupata kiwanja ni kubwa.Vijijini nako kujenga kuna changamoto sana hasa ushirikina

Unadhani sababu gani huchelewesha watu kujenga nyumba zao na kuzikamilisha?

Mjadala - https://jamii.app/UjenziNyumba
CHADEMA: POLISI WAMEOMBA MAJINA YA WAGOMBEA WETU

- Chama hicho kimesema viongozi wake wa ngazi za Wilaya wametumiwa barua wakitakiwa kupeleka majina ya wagombea wa Ubunge

- Wamemtaka IGP kuzitengua na kuongoza Polisi kwa mujibu wa Sheria

Soma - https://jamii.app/PolisiBaruaCHADEMA
MVUTANO WA MAHUSIANO KATI YA MKE NA WAKWE/MAWIFI, NINI KIFANYIKE?

> Ni mara nyingi wanawake wamekuwa wakishutumiwa kwa kutokuwa na mahusiano mazuri na ndugu wa upande wa mume na sababu nyingi hutolewa ikiwemo kwamba mama mkwe humwonea wivu mke wa mwanae na hana imani kama mke anaweza kumtunza mwanae

> Je, nini ambacho kinaweza kufanyika ili mke na mama mkwe/wifi waishi kwa amani na upendo?

Mjadala - https://jamii.app/MawifiWakwe
#JFMahusiano
ZIMBABWE: MADAKTARI WAUNGANA NA MANESI, WATISHIA KUFANYA MGOMO

- Madaktari hao wanalalamikia malipo ya chini na ukosefu wa vifaa kinga (PPE) dhidi ya #CoronaVirus

- Manesi takriban 15,000 nchini humo wamekuwa kwenye mgomo kwa wiki mbili

Soma - https://jamii.app/COVID19Updates
ACT WAZALENDO HATARINI KUCHUKULIWA HATUA NA MSAJILI WA VYAMA

- Ni baada ya Ofisi hiyo kutuma barua kadhaa kwa ACT

- Mojawapo ni kuhusu kuchoma bendera za chama kingine na kutumia dini kwenye siasa

Soma https://jamii.app/MsajiliACTSheria
RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA PROF. MKUMBO, OLE SENDEKA NA KATAMBI

- Dkt. Jumanne Fhika anachukua nafasi ya Ole Sendeka na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe

- Uteuzi wa Prof. Mkumbo umetenguliwa na Mhandisi Anthony Sanga na anakuwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Maji

Soma https://jamii.app/UteuziRaisMagufuli
BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU YAFUNGUA DIRISHA LA MAOMBI KWA SIKU 40

> Maombi yatumwe kwa njia ya mtandao kuanzia Julai 21, 2020 hadi Agosti 31, 2020

> Waombaji wametakiwa kusoma Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Mwaka 2020/2021 unaopatikana (www.heslb.go.tz)

Soma - https://jamii.app/MikopoElimu
BERNARD MEMBE AKUBALI KUCHUKUA FOMU YA URAIS KUPITIA ACT WAZALENDO

- Amesema ni wakati muafaka kushiriki mazungumzo na vyama vingine ili kusimamisha 'kisiki cha mpingo' kimoja

- Membe alitambulishwa rasmi kuwa Mwanachama wa ACT jana

Soma - https://jamii.app/MembeUrais2020
INDIA: VISA VYA #CORONAVIRUS VYAFIKIA MILIONI 1

- Visa 1,005,760 vimerekodiwa huku vifo ni 25,619 na waliopona 636,660

- India inakuwa nchi ya 3 kuwa na visa zaidi ya Milioni 1 nyuma ya Brazil (2,014,738) na Marekani(3,677,036)

Soma - https://jamii.app/COVID19Updates
#JFCOVID19_Updates
SUDAN YAKANUSHA KUSHIRIKI KWENYE MAPIGANO NCHINI LIBYA

> Luteni Jenerali, Yasir al Atta amekanusha madai ya Sudan kushiriki ktk mapigano ya ndani nchini Libya na haijawahi wala haitatuma mamluki kupigana nchini Libya

Soma - https://jamii.app/SudanMapiganoLibya