JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UBALOZI WA MAREKANI WASIKITISHWA UKIDAI TANZANIA INAMINYA DEMOKRASIA

> Wasikitishwa na kukamatwa kwa Viongozi wa Upinzani wakiwa katika mikutano na kufutiwa leseni gazeti la upinzani

> Wamesema hivi ni vitisho kwa Upinzani, Asasi za Kiraia na Wanahabari

Soma https://jamii.app/UbaloziDemokrasia
#JFSiasa
MWANACHAMA WA 28 WA CCM ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS ZANZIBAR

- Kada wa CCM, Idd hamad Idd amechukua fomu kuwania kuteuliwa kugombe Urais wa Zanzibar kupitia CCM Oktoba 2020

- Anakuwa mwanachama wa 28 wa chama hicho kuchukua fomu hiyo

Soma https://jamii.app/IddHamadZNZ
#Uchaguzi2020
#CORONAVIRUS: MAREKANI IMERIPOTI ZAIDI YA WAGONJWA WAPYA 34,500 NDANI YA SAA 24

- Imeripoti wagonjwa wapya 34,516 na vifo 751 kwa mujibu wa Chuo cha John Hopkins

- Idadi ya visa imefikia 2,381,538, vifo 121,979 na waliopona 987,669

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
#JFCOVID19_Updates
MWANACHAMA WA 29 WA CCM ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS ZANZIBAR

- Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaame Simai Mcha ambaye ni Mwandishi wa Habari amechukua fomu kuwania kuteuliwa kugombe Urais wa #Zanzibar kupitia CCM, Oktoba 2020

Soma https://jamii.app/ShaameMchaZNZ
#Uchaguzi2020
MWANZA: WATU 4 WAFARIKI, 27 WAJERUHIWA KWA KUPIGWA NA RADI ZIWA VICTORIA

> Waliofariki ni Nahodha na msaidizi wake, pamoja na abiria wawili Deogratius Mulungu na Ndege Abdu

> Majeruhi 27 wamelazwa katika Zahanati ya Bukiko na Kituo cha Afya Bwisya

Soma https://jamii.app/RadiMwanza4
#JFLeo
MANYARA: MWENYEKITI NA KATIBU WA CCM MBARONI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

> TAKUKURU inawashikilia viongozi wa CCM Tawi la Maisaka Kati, kwa kuomba na kupokea Tsh 200,000 kutoka kwa Mwinjilisti

> Waliomba ili wamuachie kiwanja walichodai ni cha CCM

Soma https://jamii.app/RushwaManyaraCCM
VYAMA VYA SIASA 12 VYAMTAKA MSAJILI KUMCHUKULIA HATUA MAALIM SEIF

- Vimedai kauli za Maalim Seif kama β€œLazima tujipange kwa lolote” β€œkama noma na iwe noma” ni za kichochoezi

- Vyama hivyo ni Demokrasia Makini, DP, SAU, TLP, UPDP, CCK, NLD, NCCR, ADA TADEA, AFP, ADC na UDP

Soma https://jamii.app/MaalimSeifHatua
TABORA: MTUHUMIWA SUGU WA MAUAJI AKAMATWA

> Polisi wamemkamata Juma Nassibu maarufu Juma Macho aliyekuwa akisakwa kwa muda mrefu

> Pia, wamefanikiwa kumkamata kinara wa wizi wa pikipiki mwenye mtandao Tabora, Mwanza, Shinyanga na Mara

Soma https://jamii.app/MuuajiSugu
#CORONAVIRUS: IDADI YA VISA KENYA YAFIKIA 5,384

- Wagonjwa 178 wameongezeka baada ya sampuli 3,918 kupimwa ndani ya saa 24 zilizopita

- Wagonjwa 34 wamepona na waliopona wamefikia 1,857. Waliofariki ni 132 baada ya 2 kuongezeka

Soma https://jamii.app/COVID19KE-5384
#JFCOVID19_Updates
WATU 9 WAFARIKI NA 51 KUOKOLEWA BAADA YA BOTI KUPINDUKA ZIWA TANGANYIKA

- MV Nzeimana inayofanya safari zake kati ya Sibwesa na Ikola imezama leo eneo la Rasini

- Inasemekana ilikuwa na watu 60 na ilizama baada ya kupinduka kutokana na dhoruba kali

Soma https://jamii.app/MVNzeimanaYazama
ARUSHA: AFISA ARDHI AFUKUZWA KAZI KWA KUSABABISHA HASARA YA TSH. BILIONI 5

> Nikodemus Hilu ameisababishia Serikali hasara kwa kurejesha kwa Mwananchi hati ya ardhi ya ekari zaidi ya 3,000 zilizofutwa na Rais Magufuli na Mahakama kuamuru Serikali ilipe fidia

Soma https://jamii.app/AfisaArdhiArusha
NJOMBE: MBARONI KWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 15

> Peter Paulo Chaula(30) wa Makambako anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumlawiti kijana mwenye miaka 15

> Baada ya mahojiano ilionekana kuna mazoea na aliyelawiti amedai wao ni wapenzi

Soma https://jamii.app/MbaroniLawiti
#JFLeo
IRAN: WATU 3 WAKAMATWA KWA KUWAUZA WATOTO WACHANGA INSTAGRAM

> Watu hao huwatafuta wajawazito masikini na kuwalipia gharama za kujifungua na kuchukua watoto baada ya kujifungua

> Polisi wamesema watoto walinunuliwa kwa takriban Tsh. 1,157,000

Soma https://jamii.app/IranBiasharaWatoto
#JFLeo
SIKU YA MABAHARIA (SEAFARERS) DUNIANI

> Juni 25 ni siku ya Mabaharia duniani, kutokana na #COVID19 Mabaharia wamepata changamoto ya kutoruhusiwa kutoka katika meli zao

> Zaidi ya 80% ya biashara duniani hutumia bahari, Mabaharia hufanikisha hilo

Soma https://jamii.app/SeafarersDay
#JFLeo
MASTER J ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE ROMBO

> Muandaaji muziki Joachim Marunda Kimaryo maarufu kama β€˜Master J’ ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Rombo, Kilimanjaro kwa tiketi ya CCM

> Amesema yupo CCM tangu zamani

Soma https://jamii.app/MasterJRombo
#JFSiasa
LIVERPOOL YATAWAZWA KUWA MABINGWA WA ENGLAND. SHUKRANI KWA CHELSEA

- Klabu ya Liverpool imetawazwa kuwa Bingwa wa Ligi Kuu Soka nchini England 2019/20 baada ya Chelsea kuifunga Manchester City goli 2-1

- Kwa matokeo hayo Liverpool yenye alama 86 baada ya michezo 31 haiwezi kufikiwa kwa alama na Manchester City yenye alama 63 huku michezo 7 ikiwa imebaki

- Liverpool ilikuwa na kiu ya kuchukua Kombe hilo kwa takriban miaka 30
NGEMELA LUBINGA: MEMBE ANAWEZA KUSHTAKIWA KWA KUMSHAMBULIA AMIRI JESHI

> Kanali mstaafu Ngemela Lubinga amemkumbusha Bernard Membe kuheshimu kiapo

> Amesema Askari akistaafu atadumu kuheshimu kiapo na kuwatii Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hasa Amiri Jeshi Mkuu

Soma https://jamii.app/LubingaMembe
#JFSiasa
TAARIFA ZILIZOPIGWA MARUFUKU KUTOLEWA NA KUSAMBAZWA NA VYOMBO VYA HABARI(KIFUNGU CHA 7 SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI (2016)

1. Taarifa zitakazodhoofisha usalama wa nchi au upelelezi

2. Zinazokwamisha taratibu za sheria au kuhatarisha usalama wa maisha

Soma > https://jamii.app/SheriaHudumaHabari

#UhuruWaKujieleza
BURUNDI: PIERRE NKURUNZIZA KUZIKWA LEO, JUNI 26

> Aliyekuwa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza atazikwa kwenye makaburi ya mji wa Gitega

> Nkurunziza alifariki Juni 8, kutokana na mshtuko wa moyo kama ilivyotangazwa na Serikali ya nchi hiyo

Soma https://jamii.app/PiereBurundi
#JFLeo
TANGA: MWANACHUO ATUHUMIWA KUMUUA MWENZAKE

> Waziri Ramadhani anadaiwa kumuua Hussein Daud kwa kumchoma kisu baada ya kumkuta ktk chumba cha rafiki yake wa kike

> Polisi wamesema tukio hilo si fumanizi. Wanamshikilia binti, mtuhumiwa amekimbia

Soma https://jamii.app/MapenziMauaji