JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
VIONGOZI WA ARUSHA WALIOSAMEHEWA NA RAIS MAGUFULI WAHAMISHWA VITUO

> Aliyekuwa Mkuu wa Usalama Mkoa Arusha anahamishiwa Mkoa mwingine

> Mkuu wa TAKUKURU Mkoa, Frida Wikes, amehamishiwa Makao Makuu

> Pia, Kamanda wa Polisi Mkoa, Jonathan Shanna amehamishiwa Chuo cha Polisi (CCP) Kilimanjaro

Soma https://jamii.app/VigogoWahamishwa
#JFSiasa
LOWASSA NA MKEWE WAMDHAMINI RAIS MAGUFULI

- Edward Lowassa na mkewe, Regina Lowassa wamemdhamini Rais Magufuli ili atetee Urais Oktoba 2020

- Rais Magufuli ndiye pekee aliyechukua fomu ya kuwania Urais Tanzania kupitia CCM

Soma https://jamii.app/LowassaAmdhaminiMagufuli
#Uchaguzi2020
MAWE MAKUBWA YA TANZANITE YANUNULIWA NA SERIKALI. YATAWEKWA MAKUMBUSHO

> Rais Magufuli amempigia simu na kumpongeza mchimbaji Saniniu Laizer na aliamuru mawe hayo yanunuliwe na Serikali ili mchimbaji asidhulumiwe

Soma https://jamii.app/MadiniBilioneaTZ
#JFLeo
MWANAMKE WA TATU AJITOKEZA KUWANIA URAIS ZANZIBAR

- Kada wa CCM, Fatma Kombo Masoud amekuwa mwanamke wa tatu kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kugombea urais wa #Zanzibar

- Anakuwa mwanachama wa 26 kuomba fomu hiyo kupitia chama hicho

Soma https://jamii.app/FatmaKomboZNZ
#Uchaguzi2020
MGOMBEA WA KWANZA WA URAIS ZANZIBAR KUPITIA NCCR-MAGEUZI ACHUKUA FOMU

- Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Visiwani, Ambari Haji Khamis amekuwa wa kwanza kuchukua fomu kuomba ridhaa ya chama kumteua kuwa Mgombea Urais #Zanzibar

Soma https://jamii.app/UchaguziNCCRZnz
#Uchaguzi2020
KAMATI YA NIDHAMU TFF YAWAFUNGIA MKUDE NA MORRISON

> Mchezaji wa Simba SC, Jonas Mkude na wa Yanga SC, Benard Morrison watakiwa kulipa Tsh. 500,000 na kutocheza mechi mbili

> Ni baada ya kuwapiga viwiko wachezaji wenzao katika mechi

Soma https://jamii.app/MkudeMorrisonTFF
#JFMichezo
BUNDA: BABA AMTONGOZA MWANAYE KWA TSH. 5,000, ALIPOKATAA AKAMBAKA

> Mtoto huyo alisema hiyo ni mara ya pili baba yake kumfanyia ukatili huo

> Shangazi yake alimlazimisha kujisafisha sehemu za siri ili asionekane kama amebakwa

Soma https://jamii.app/MtotoBabaUbakaji
#JFLeo
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
THRDC YALAANI KUKAMATWA KWA WAKUFUNZI WAKE NA KUSITISHWA KWA MAFUNZO

> Walikamatwa na Polisi wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wanachama wapya 30

> Polisi walidai mafunzo hayo hayakufuata utaratibu na baadaye kuwaachia Wakufunzi hao

Soma https://jamii.app/THRDCYalaaniUonevu
#JFLeo
LINDI: ZITTO KABWE NA VIONGOZI WENZAKE WAACHIWA KWA DHAMANA

- Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na wenzake 7 wameachiwa kwa dhamana ya wadhamini 2 kila mmoja na kutakiwa kuripoti Polisi Lindi Julai 01, 2020

- Awali, walikuwa wanashtakiwa kwa kufanya maandamano bila kibali cha Polisi lakini baadaye shtaka likageuzwa na kuwa kutishia uvunjifu wa amani

Soma https://jamii.app/ZittoBwegeLindi
#Siasa
#CORONAVIRUS-KENYA: MAAMBUKIZI YAFIKA 5,206 NA VIFO 130

> Watu 254 wamekutwa na maambukizi ya #COVID19 katika sampuli 4,859 zilizopimwa saa 24 zilizopita

> Pia, watu 1,823 wameripotiwa kupona huku vifo vikifikia 130

Soma https://jamii.app/KECOVID19Cases
#JFCOVID19_Updates
FAIDA ZA MAFUTA YA MKARATUSI

> Mafuta haya hukamuliwa kutoka kwenye majani na huweza kutumika kama tiba

> Mafuta ya Mkaratusi hutuliza maradhi yanayohusika na kifua na mafua. Hufukuza wadudu, hutibu vidonda na pia hukipa kinywa harufu nzuri

Soma zaidi https://jamii.app/MkaratusiFaida
#JFAfya
KUTOIJUA SHERIA HAKUKUFANYI USIWE MKOSAJI

> Sheria zinatambua kuwa tunazifahamu. Kusema ulikuwa hujui sheria Mahakamani kama utetezi, haikusaidii kitu

> Hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuzifahamu sheria za nchi au mahali alipo

Soma zaidi https://jamii.app/KutoijuaSheria
#JFSheria
NAMNA NZURI YA KUFANYA β€˜GROWTH HACKING’ ILI KUKUA KWA HARAKA

> Tangaza biashara ionekane kuna uhaba. Mfano, Ofa ya muda mfupi au bidhaa zinazokaribia kuisha

> Cheza na saikolojia. Mfano; unauza Laptop, usiandike Nunua Laptop kwa 400,000 nikupunguzie 15% ya begi na hard disk, bali andika Lipia Laptop Tsh 590,000 upate begi na Hard Disk bure

Soma https://jamii.app/GrowthHacking
#JFBiashara
NJOMBE: KIJANA WA MIAKA 19 AJINYONGA KWA KUTUMIA SHUKA

> Chesco Mtega(19) mkazi Kijiji cha Ludewa amejinyonga huku Msongo wa mawazo ukidaiwa kuwa sababu

> Hata hivyo uchunguzi unaendelea ili kubaini kulikuwa na mgogoro gani kwenye familia

Soma https://jamii.app/NjombeShuka
#JFLeo
KATAVI: MAITI 2 ZA WATOTO WACHANGA ZAPOTEA NDANI YA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI

> Mkuu wa Mkoa aagiza wasimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti kusimamishwa kazi

> Ahusisha tukio na imani za kishirikina, awataka wanasiasa na wadau wa madini kutofanya hivyo

Soma https://jamii.app/MaitiWatotoKatavi
#JFLeo
TANGA INAKADIRIWA KUWA NA WAATHIRIKA 5,190 WA HEROINE

> Waziri wa Afya amezindua Kliniki ya Methodone Mkoani Tanga ili kutoa huduma kwa waathirika

> Aitaka jamii kuwafichua wauzaji na wasambazaji wa #DawaZaKulevya

Soma https://jamii.app/Tanga5190
#JFLeo
KESI DHIDI YA JF: JAMHURI YAOMBA HATI YA KUKAMATWA SHAHIDI, MAHAKAMA YARIDHIA

> Jamhuri imeiomba Mahakama ya Kisutu iruhusu kukamatwa kwa Shahidi ktk shauri namba 458 la mwaka 2016

> Ni Tully Esther Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Umma (CRDB)

Soma https://jamii.app/TullyArrest
DODOMA: AFISA MIPANGO MIJI ASIMAMISHWA KAZI KWA KUSHINDWA KUTENDA HAKI

- DC wa Dodoma, Patrobasi Katambi amemsimamisha kazi Hadson Magomba

- Ni kutokana na kumnyanyasa na kushindwa kumpa eneo lake mjane Mdala Anna na kulibadilishia matumizi

Soma https://jamii.app/MipangoMijiDom
#JFLeo
ZANZIBAR: PEREIRA AME SILIMA AWA WA 27 KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS

> Kada wa CCM, Pereira Ame Silima aliyekuwa Mbunge wa Chumbuni 2010-2015, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais Zanzibar

Soma https://jamii.app/PereiraUraisZnz
#JFSiasa
JE, WAVIJUA VIPENGELE VYA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI (2016)?

> 1. Vyombo vya Habari vya Uchapishaji (Magazeti) vinalazimika kupata leseni kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo (Kifungu 8)

> Ukinyimwa leseni, mamlaka ya rufaa yapo kwa Waziri

Soma > https://jamii.app/SheriaHudumaHabari

#UhuruWaKujieleza