JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TABORA: MBARONI KWA KUHUJUMU MRADI WA MAJI ZIWA VICTORIA

> Creti Mabula (20) na wenzake wanne wamekutwa na vifaa vya thamani ya Tsh. milioni 57.6

> Vifaa hivyo ni vya kampuni inayotekeleza mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Tabora

Soma https://jamii.app/TaboraMradiWizi
ZANZIBAR: MJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA ZFA ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS

- Hashim Salum Hashim amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kuwa mgombea urais kupitia CCM

- Amekuwa mwanachama wa 24 wa CCM kuchukua fomu hiyo ya kuwania nafasi hiyo

Soma https://jamii.app/HashimSalumZNZ
#Uchaguzi2020
KAGERA: MTENDAJI WA KATA KIZIMBANI KWA KUMPAPASA MATITI MTOTO

- Mtendaji Kata ya Kyakailabwa, Patrick Rwegasira (44) amefikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya kumtorosha mtoto (14) na kumfanyia shambulio la aibu la kumpapasa matiti

Soma https://jamii.app/MtendajiKizimbaniKGR
UNESCO: WATOTO MILIONI 258 DUNIANI HAWAKWENDA SHULE MWAKA 2018

- Asilimia 90 ya vijana walioathiriwa zaidi ni kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia

- Mamilioni ya Vijana hubaguliwa katika mifumo ya elimu kutokana na asili zao au ulemavu walionao

Soma https://jamii.app/RipotiElimuUNESCO
SERIKALI YASITISHA LESENI YA GAZETI LA TANZANIA DAIMA NDANI NA NJE YA NCHI

- Gazeti hilo halitaruhusiwa kuchapishwa wala kusambazwa nchini au nje ya nchi kuanzia kesho

- Ni kutokana na kukithiri na kujirudia kwa makosa yanayokiuka sheria ya nchi na maadili ya uandishi

Soma https://jamii.app/TanzaniaDaimaLeseni
#JFLeo
IDADI YA WALIOATHIRIKA NA #COVID19 KENYA YAFIKIA 4,952

- Wagonjwa 155 wameongezeka. Wote ni Wakenya; Wanaume 120 na Wanawake 35

- Wagonjwa 3 wamefariki na vifo vimefikia 128. Pia, Wagonjwa 102 wamepona na jumla watu 1,782 wamepona

Soma https://jamii.app/COVID19KE-4952
#JFCOVID19_Updates
SIKU YA WAJANE DUNIANI: #COVID19 YAONGEZA CHANGAMOTO KWA WAJANE

> Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema #COVID19 inaua zaidi wanaume

> Wajane wengi wanaingia katika hali mbaya kutokana na mifumo ya jamii inayombagua mwanamke katika kurithi mali

Soma https://jamii.app/SikuYaWajane
KILWA: DC AAMURU VIONGOZI 8 WA ACT-WAZALENDO WAKAMATWE. BWEGE AUGUA MAHABUSU

> Selemani Bungara (Bwege) amezidiwa ghafla akiwa mahabusu na kukimbizwa Hospitali ya Kilwa Masoko

> Viongozi hao akiwemo Zitto Kabwe wamekamatwa asubuhi na Polisi wanataka kila Kiongozi awe na mdhamini wake

Soma https://jamii.app/LindiViongoziACT
#JFSiasa
ENGLAND: KLABU YA BURNLEY YALAANI UJUMBE ULIOONESHWA UWANJANI

> Ujumbe wa kibaguzi ulipitishwa katika Uwanja wa Etihad wakati wa mechi ya Burnley na Manchester City

> Uchunguzi unaendelea kuwabaini waliohusika, wakibainika watazuiwa kuingia viwanjani

Soma https://jamii.app/UbaguziPremierLeague
WANAFUNZI WASISITIZWE, WAPATAPO DALILI HIZI WATOE TAARIFA MARA MOJA

> Homa, kikohozi na mafua, kubanwa mbavu na kupumua kwa shida, kuumwa kichwa, vidonda kooni, mwili kuchoka

> Wawajuze walimu, wazazi au kupiga namba 199

Soma https://jamii.app/CoronaMashuleni
MBEYA: WANNE AKIWEMO POLISI WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI

> Erasto Mwalwego (29), dereva wa bodaboda mkazi wa Nzovwe, aliuawa na watu wanne kwa kupigwa na kitu butu

> Tukio lilitokea katika nyumba ya kulala wageni, Erasto alifariki hospitalini

Soma https://jamii.app/MauajiMbeyaPolisi
PEMBA: KARAFUU YA MAGENDO YAKAMATWA. WALIOTOA TAARIFA KUPATA GAWIO

> Magunia 30 ya Karafuu yaliyokuwa yasafarishwe nje ya kisiwa hicho kimagendo yamekamatwa

- Serikali imeagiza karafuu iliyokamatwa iuzwe na waliotoa taarifa kuhusu magendo hayo wapate mgao kama motisha

Soma https://jamii.app/KarafuuPemba
#JFLeo
CHINA: TUTAENDELEA NA MSIMAMO MKALI DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

> Rais Xi Jinping leo ametoa wito kuendeleza juhudi za kupambana na #DawaZaKulevya

> Takwimu za mwaka jana zinaonesha 0.18% ya wachina (takriban watu milioni 2.5) wanatumia dawa za kulevya

Soma https://jamii.app/XiOnDrugs
PROFESA BASSETTI: #CORONAVIRUS INAWEZA KUISHA YENYEWE BILA CHANJO

> Mtaalamu wa Magonjwa ambukizi amesema #COVID19 imetoka kuwa Chui mkali hadi kuwa Paka mwitu

> Asema tahadhari zikiendelea kuchukuliwa, #COVID19 itapotea yenyewe

Soma https://jamii.app/CoronaExpertTalks
#JFCOVID19_Updates
TWITTER YAFICHA β€˜POSTS’ ZA RAIS TRUMP ZINAZOTISHIA WAANDAMANAJI

> Jumbe hizo za Rais Trump zinatishia kutumia nguvu kumaliza maandamano

> Pia, Facebook waliiondoa tangazo la Rais Trump lililokuwa na alama ya Utawala wa β€˜Nazi’ iliyotumika na wajerumani

Soma https://jamii.app/TwitterTrump
#JFLeo
MWANAMKE WA PILI AJITOKEZA KUWANIA URAIS ZANZIBAR

- Kada wa CCM, Hasna Attai Masoud amekuwa mwanamke wa pili kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kugombea Urais wa #Zanzibar

- Anakuwa mwanachama wa 25 kuchukua fomu hiyo kupitia chama hicho

Soma https://jamii.app/HasnaAttaiZNZ
#Uchaguzi2020
ZITTO NA WENZAKE WAHAMISHIWA LINDI. BWEGE ATOLEWA HOSPITALI

- ACT Wazalendo imeeleza kuwa Zitto na viongozi wenzake 6 walisafirishwa jana usiku kwa gari la wazi kutoka Kilwa hadi Kituo cha Polisi Lindi

- Aidha, Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara (Bwege) ambaye hali yake imetengemaa amefikishwa Lindi na kujumuishwa na wenzake

Soma https://jamii.app/ZittoBwegeLindi
RUKWA: AIBA MTOTO NA KUDANGANYA AMETEKETEA KWA MOTO

> Mwanamke huyo amesema, sababu ya kumuiba mtoto wa wiki moja wa nduguye ni kuwa ametafuta mtoto kwa muda mrefu bila mafanikio

> Taratibu za kisheria zinafanyika ili afikishwe Mahakamani

Soma https://jamii.app/MtotoWiki1
#JFLeo
AWA BILIONEA BAADA YA KUPATA TANZANITE YA THAMANI YA TSH. BILIONI 7.8

> Saninniu Laizer amepata mawe ya Tanzanite, moja likiwa na Kg 9.2 na lingine kg 5.8

> Wizara ya Madini imesema mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana tangu machimbo yaanze

Soma https://jamii.app/MadiniBilioneaTZ
#JFLeo