JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZANZIBAR KUFUNGUA SHULE NA SHUGHULI ZA KIJAMII KUANZIA JUNI 29

> Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein ametangaza kufungua skuli zote pamoja na shughuli za kijamii kuanzia Juni 29 baada ya kupungua kwa maradhi ya #COVID19

> Pia, amevunja Baraza la Wawakilishi la 9 huko Chukwani

Soma - https://jamii.app/ShuleZbarJuni29
Jamii Forums tunapenda kutambua uwepo, umuhimu, Jitihada na changamoto ambazo hupitiwa na wale wote ambao wanaheshimu na kuthamini nafasi zao kama baba kwa watoto wao wa kuwazaa na kuwalea

Tunatambua kama walezi si kazi rahisi, hivyo tungependa kutumia nafasi hii kuwakumbusha na kuwasihi kutokata tamaa kwasababu Watoto na familia hufarijika pale wanapofanya Jitihada za makusudi kuwalea, kuwatunza na kuwa karibu nao Kimahitaji ya kisaikolojia, kiuchumi na hata Faraja

Kheri ya siku ya akina baba duniani
UNA MTAZAMO GANI KUHUSU BUNGE LA 11? UNAKUMBUKA TUKIO GANI LILILOTOKEA

> Baadhi ya wadau wamesema kwa miaka 5 ya Bunge la 11 lilikuwa na upitishaji wa sheria zinazokinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

> Mkurugenzi THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema halikufanya jukumu lake la uwakilishi bali ilikuwa sehemu ya kutetea Serikali

Kwa mjadala zaidi - https://jamii.app/MaoniBunge11
DARAJA LA WAMI KUFUNGWA KWA MUDA KWA SIKU 3 KUANZIA JUNI 25

- Litafungwa kwa saa 2, kuanzia 8 usiku hadi saa 10 alfajiri kwa siku 3 kuanzia Juni 25-27

- Ni kutokana na ukaguzi na matengenezo ya daraja hilo kwenye barabara ya Chalinze-Segera

Soma https://jamii.app/KufungwaDarajaWami
CUF: WABUNGE, MADIWANI WALIOPOKELEWA NA ACT WALISHAJITENGA NA CHAMA

- Mkurugenzi wa Habari, Eng. Ngulangwa amesema Wabunge na madiwani hao walishajitenga

- Amesema CUF iliamua kutowafukuza ili kudhibiti matumizi mabaya ya kodi za wananchi

Soma - https://jamii.app/WabungeMadiwaniCUF
MEMBE: KAMATI KUU IKITAMKA LEO KUWA ILIKOSEA KUNIFUKUZA NACHUKUA FOMU JUMATATU

> Adai tamko likitolewa kwa wakati, kesho Jumatatu atachukua fomu ya β€˜kujipima’ na Rais

> Ameonya kuwa bila yeye Uchaguzi hautonoga kama ule wa Zanzibar

> Aomba utulivu kwani Oktoba ni mbali na lolote linaweza kutokea

Angalia https://youtu.be/YDReKJ5mBD0
RAIS MAGUFULI ATEUA WAKUU WA WILAYA MOROGORO NA MONDULI

- Rais Magufuli amemteua Bakari Msulwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro

- Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Edward Jotham Balele ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha

Soma https://jamii.app/RaisAfanyaUteuzi
MAREKANI: RAIS TRUMP AANZA VIBAYA KAMPENI, ASHINDWA KUJAZA UWANJA WA WATU 19,000

- Ni kampeni yake ya kwanza tangu kuanza kwa mlipuko wa #CoronaVirus

- Amesema vyombo vya habari na waandamanaji wamesababisha wanaomuunga mkono wasihudhurie

Soma https://jamii.app/TrumpTulsaRally
WAZIRI MKUU: WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KIPINDI CHA UCHAGUZI WAKAMATWE

> Maagizo hayo yametolewa ili kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu unakuwa huru na wa haki, hivyo kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi wanaowahitaji na si kwa msukumo wa rushwa

Soma - https://jamii.app/RushwaUchaguzi
#CORONAVIRUS-BRAZIL: WATU 7,285 WAMEFARIKI NDANI YA WIKI MOJA

- Imeripoti vifo vipya 641 kwa siku ya jana na kufanya jumla ya vifo kufikia 50,617

- Pia, imerekodi Wagonjwa wapya 17,459 na kufanya jumla ya visa kufikia 1,085,038

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
#JFCOVID19_Updates
ALIYEKUWA WAZIRI WA HABARI, RASHID JUMA ACHUKUA FOMU YA URAIS

- Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni Zanzibar, Rashid Ali Juma amechukua fomu kuwania urais Zanzibar kupitia CCM

- Amekuwa Mgombea wa 16 kujitokeza kuchukua fomu hiyo

Soma https://jamii.app/RashidJumaZNZ
#JFSiasa
KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA ZANZIBAR ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS

- Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Khamis Mussa Omar amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar

- Amechukua fomu hiyo kupitia CCM na amekuwa mgombea wa 17 kuchukua fomu hiyo

Soma https://jamii.app/KhamisOmarZNZ
#JFSiasa
IKULU, DAR: RAIS MAGUFULI AMUAPISHA MKUU WA MKOA ARUSHA

- Rais Magufuli amemuapisha Mkuu wa Mkoa mteule wa Arusha, Idd Hassan Kimanta

- Mkuu huyo aliteuliwa juzi kuchukua nafasi ya Mrisho Gambo ambaye uteuzi wake ulitenguliwa

Fuatilia - https://jamii.app/Uapisho-RCArusha
#JFSiasa
WAZIRI WA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS

- Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Mjawiri amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar

- Amechukua fomu hiyo kupitia CCM na amekuwa mgombea wa 18 kuchukua fomu hiyo

Soma https://jamii.app/MjengoMjawiri-ZNZ
#JFSiasa #Uchaguzi2020
ZANZIBAR: NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, HAMAD MASAUNI ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS

- Hamad Masauni amechukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM

- Anakuwa mwanachama wa 19 wa chama hicho kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho

Soma https://jamii.app/MasauniZanzibar2020
#JFSiasa
ZANZIBAR: WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS

- Mohammed Aboud Mohammed amechukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM

- Amekuwa mwanachama wa 20 wa chama hicho kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho

Soma https://jamii.app/MohammedUraisZNZ
#JFSiasa
RAIS MAGUFULI ATAJA SABABU YA KUTENGUA UONGOZI WA ARUSHA

> Rais Magufuli amesema ametengua uteuzi wa RC Mrisho Gambo, DC Gabriel Daqarro na Mkurugenzi wa Arusha, Dkt. Maulid Madeni kwa kuwa zaidi ya miaka miwili viongozi hao wamekuwa wakigombana huku kila mmoja akitaka kuwa bosi wa mwingine

Angalia; https://youtu.be/-7XtOPFg25c
#JFLeo
ASKARI POLISI AFUKUZWA KAZI KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA BANGI

> Koplo Anthony Francis wa Kituo cha Polisi Kisarawe amekamatwa akiwa na Kg 76 za Bangi kwenye gari yake, Mkoani Morogoro

> Pia, Polisi inawashikilia watu 22 kwa kuhusika na biashara hiyo

Soma https://jamii.app/BangiPolisi