JamiiForums
βœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZIMBABWE: MATAJIRI WATAKAOSHINDWA KUELEZEA UTAJIRI WAO, MALI ZAO KUTAIFISHWA

> Mwenyekiti wa Tume ya kupambana na Ufisadi, Jaji Loyce Matanda-Moyo ndiye ameanzisha operasheni hiyo

> Zimbabwe sio nchi ya kwanza kuchukua hatua hiyo duniani

Soma https://jamii.app/ZimbabweUtajiri
#JFLeo
ZANZIBAR: BAKARI RASHID BAKARI ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

- Kada wa CCM, Bakari Rashid Bakari amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM

- Anakuwa Mgombea wa 21 kuchukua fomu hiyo kupitia CCM

Soma https://jamii.app/BakariRashidZNZ
#JFSiasa
ZANZIBAR: HUSSEIN IBRAHIM MAKUNGU ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

- Kada wa CCM, Hussein Ibrahim Makungu amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM

- Anakuwa Mgombea wa 22 kuchukua fomu hiyo kupitia CCM

Soma https://jamii.app/HusseinIbrahimZNZ
#JFSiasa
ZANZIBAR: MKUU WA MKOA WA KUSINI UNGUJA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

- Ayoub Mohamed Mahmud amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM

- Amekuwa mgombea wa 23 kujitokeza kuchukua fomu hiyo kupitia CCM

Soma https://jamii.app/AyoubMahmudZNZ
#JFSiasa
MATAIFA 188 YATHIBITISHA KUWA NA #COVID19

> Hadi sasa mlipuko wa #COVID19 ulioanza Desemba, 2019, umesababisha Vifo 474,823, maambukizi 9,772,296 na waliopona 4,605,114 wameripotiwa

> Marekani inaongoza kwa maambukizi ikifuatiwa na Brazil

Soma https://jamii.app/Corona188Nchi
#JFCOVID19_Updates
DR CONGO: WATU 19 WAUAWA. 9 KATI YAO WALITEKWA IJUMAA

> Watu tisa kati ya hao walitekwa Ijumaa na wapiganaji wa ADF na miili yao ikakutwa Kaskazini mwa Kivu wakiwa wamefariki

> ADF pia waliwaua kwa mapanga na risasi raia 10 wa kijiji cha Bukaka

Soma https://jamii.app/19CongoADF
#JFLeo
MANYARA: MBARONI KWA KUWEKA MADIRISHA YALIYO CHINI YA KIWANGO KATIKA IKULU NDOGO

> Mzabuni Patrick J. Kauky aliweka madirisha tofauti na yaliyotakiwa kuwekwa

> Pia, TAKUKURU imebaini Kauky alipata Kandarasi hiyo kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma

Soma https://jamii.app/MzabuniTAKUKURU
#JFLeo
KENYA: MAAMBUKIZI YA #COVID19 YAFIKIA 4,797, VIFO VYAFIKA 125

> Watu 59 zaidi wamethibitika kuwa na #CoronaVirus, huku watu 2 wakiripotiwa kufariki na kufanya vifo kufikia 125

> Watu 73 wamepona na kufanya idadi ya waliopona kufikia 1,682

Soma https://jamii.app/59CoronaKE
#JFCOVID19_Updates
MALAWI KUFANYA UCHAGUZI JUNI 23, BAADA YA MAHAKAMA KUBATILISHA MATOKEO YALIYOPITA

> Rais Peter Mutharika alitangazwa kuwa mshindi Mei 2019 lakini upinzani walipinga matokeo

> Lazarus Chakwera atakabiliana na Mutharika katika Uchaguzi huo

Soma https://jamii.app/MalawiUchaguzi
#JFSiasa
WAZIRI JAFO AWATAKA VIONGOZI KUTOFANYA MAMBO YATAKAYOMTWEZA RAIS MAGUFULI

- Amewasihi Viongozi wanaopewa dhamana katika maeneo mbalimbali kumsaidia Rais

- Ameongeza kuwa Rais ni Mtu na Urais ni Taasisi na kuwa Rais ana mambo mengi ya kufanya

Angalia Video; https://youtu.be/9QnWDxhL3-I
TATIZO LA HARUFU MBAYA KINYWANI NA NAMNA YA KULIEPUKA

> β€˜Halitosis’ inaweza kusababishwa na magonjwa ya meno, magonjwa ya fizi au maambukizi kwenye koo la hewa au kwenye mapafu

> Kutotumia Sigara na kupiga mswaki vizuri kunaweza kusaidia kupunguza tatizo hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/KunukaKinywa
#JFAfya
CHADEMA: TUTAISHINDA CCM JINSI ILIVYO. NG'OMBE HUYU MARA HII HAGEUZIWI KIBLA, ANACHINJWA ALIVYO

- Wamesema Serikali inayoishi kwa uongo haiwezi kushinda kura na katika Uchaguzi huu hawajitoi

- Wamesema wanajua hakuna Tume Huru ila wanaenda kushinda Kituoni

Angalia Video; https://youtu.be/Npxg1I3z2Vk
#Siasa #JFSiasa
UNAIDS: #COVID19 YAATHIRI UPATIKANAJI NA GHARAMA ZA ARVs

> Utafiti umebaini kubaki ndani na ufungwaji wa mipaka kuepuka #COVID19 kumeleta changamoto katika uzalishaji na usambazaji wa ARVs

> Huenda ikasababisha vifo 500,000 Kusini mwa Jangwa la Sahara

Soma https://jamii.app/ARVsCOVID19
#JFLeo
VANESSA MDEE: WASANII WENZANGU WAMENISHUKURU KWA KUFUNGUKA KUHUSU TASNIA YA MUZIKI

- Vanessa alitangaza kujitoa katika tasnia ya muziki wiki iliyopita kupitia β€˜podcast’ yake akidai ilimpelekea kupata msongo wa mawazo

- Ameeleza kuwa maisha ya wasanii hayana uhalisia kwani wanalazimika kuendana na ukubwa wa brand zao hata wanapokosa uwezo huo

Soma https://jamii.app/VanessaMdeeMuziki
#COVID19 YASABABISHA SAUDI ARABIA KUZUIA RAIA WA KIGENI KWENDA KUFANYA HIJJA

> Raia kutoka nchi nyingine ambao tayari ni wakazi wa Saudi Arabia wataruhusiwa kufanya Hijja

> Hatua hiyo itawawezesha kutokaribiana wakati wa ibada hiyo

Soma https://jamii.app/Hijja2020SaudiArabia
#JFLeo
CHINA YAINGIA KATIKA USHINDANI WA β€˜NAVIGATION SATELLITE SYSTEM’ KWA KURUSHA SATELAITI YA MWISHO

> Leo Juni 23, China imezindua satelaiti ya kukamilisha mfumo wa β€˜Geolocation’

> Mfumo huo utaleta ushindani kwa GPS wa Marekani, GLONASS wa Urusi na Galileo wa Umoja wa Ulaya

> Hatua hii inaifanya China kuacha kuitegemea Marekani na Ulaya

Soma https://jamii.app/ChinaBeiDou
#JFLeo
MAREKANI YAIOMBA CHINA KUWAACHIA RAIA 2 WA CANADA

> China inadaiwa kuwashikilia raia hao kama kisasi dhidi ya Canada inayomshikilia Mkurugenzi wa Huawei

> China inawatuhumu raia hao kujihusisha na ujasusi na tayari kesi yao imeanza kusikilizwa

Soma https://jamii.app/ChinaCanadaRaia
#JFLeo
MBARONI KWA KUTAKATISHA TAKRIBAN TSH. BILIONI 2

> Salum Rajabu(51), amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kujipatia kiudanganyifu fedha takriban Tsh. Bilioni 2

> Amedaiwa kutenda hayo kati ya Aprili 1 na 20 katika maeneo tofauti ikiwemo Lubumbashi, Congo

Soma https://jamii.app/Kizimbani898k
#JFLeo
LINDI: ZITTO KABWE NA SULEMANI BUNGARA WAKAMATWA NA POLISI

- Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Sulemani Bungara (Bwege) na viongozi wengine wamekamatwa

- Ni baada ya Polisi kuwasili kwenye mkutano wa ndani wa ACT Wilayani Kilwa ambapo shughuli za kuwapokea Madiwani 8 wa CUF zilikuwa zikiendelea

Angalia Video; https://youtu.be/zzh_jXkxnKY
#JFSiasa
UGANDA: WAGONJWA 23 WA #COVID19 WAONGEZEKA. WATANZANIA 2 WARUDISHWA

- Wagonjwa wapya ni Waganda na visa vimefikia 797. Waliopona ni 699 na hakuna kifo

- Madereva 13; Kenya 8, Tanzania 2, Burundi 1, Eritrea 1 na Rwanda 1 wamekutwa na virusi na kurudishwa

Soma https://jamii.app/COVID19UG-797
#JFCOVID19_Updates