JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MASHABIKI WAZUIWA KUHUDHURIA MECHI ZA NYUMBANI ZA KLABU YA JKT TANZANIA

> Wizara ya Michezo imeizuia timu ya JKT Tanzania kucheza mbele ya mashabiki kwa mechi zake zote zilizosalia kwenye uwanja wake wa Jamhuri,Dodoma

> Ni baada ya jana katika mechi dhidi ya Yanga SC mashabiki kutozingatia mwongozo wa afya wa kukaa umbali wa mita 1 ili kujikinga na #COVID19

Soma - https://jamii.app/MashabikiJKT
UKATILI KWA WATOTO: WATOTO ZAIDI YA 200 WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO MWANZA

> Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt. Severine Lalika amesema "Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi Mkoani Mwanza, mwaka huu kuanzia Januari hadi Machi matukio 236 yaliripotiwa ambapo kati yao Wavulana ni 17 na Wasichana ni 219"

Soma - https://jamii.app/UkatiliWatoto
ZANZIBAR: MOHAMED HIJA MOHAMED ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CCM

- Anakuwa mgombea wa 8 kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Urais

- Amewahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Mwambata Ubalozi nchini India

Soma https://jamii.app/MohamedHijaZnz
BURUNDI: RAIS EVARISTE NDAYISHIMIYE AAPISHWA, AAHIDI KUHESHIMU KATIBA

- Rais Ndayishimiye (52) alishinda Uchaguzi Mkuu wa mwezi Mei na alitarajiwa kuapishwa ifikapo Agosti lakini utaratibu ulibadilika baada kifo cha Rais Pierre Nkurunziza

Soma - https://jamii.app/UapishoRaisBurundi
BALOZI MSTAAFU SULEIMANI NASSOR ACHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR

- Balozi Meja Jenerali Mstaafu Issa Suleimani Nassor anakuwa mgombea wa 9 kuchukua fomu ya kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani humo

Soma - https://jamii.app/BaloziNassorZanzibar

#Uchaguzi2020
UGANDA: VISA VYA #CORONAVIRUS VYAFIKIA 741

- Serikali imethibitisha ongezeko la visa vipya 9. Wagonjwa 442 wamepona hadi sasa

- Madereva 31; Kenya-24, Tanzania-6 na Burundi-1 wamerudishwa nchini mwao baada ya kukutwa na #COVID19

Soma https://jamii.app/Corona741-UG
#JFCOVID19_Updates
BULEMBO: UNACHUKUAJE FOMU YA URAIS WAKATI MAGUFULI HAJAMALIZA VIPINDI 2?

> Aliyekuwa Mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema “Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana-CCM, Rais anatakiwa awe katika vipindi 2. Sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?"

> Amesema hataki kugombea Ubunge licha ya kwamba anajua atashinda na haiwezekani nyumba nzima wawe Wabunge

Soma - https://jamii.app/BulemboUrais
DODOMA: RAIS MAGUFULI APIGA MARUFUKU WAPIGA DEBE KWENYE STENDI KUU YA MABASI

> Ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuhakikisha wajasiriamali wadogo, waendesha bodaboda na daladala kutosumbuliwa kwenye stendi hiyo

> Asema wapiga debe wakati mwingine wanageuka kuwa wezi

Soma https://jamii.app/WapigadebeStendi
#CORONAVIRUS: KENYA YATANGAZA VISA VIPYA 213 NA VIFO 10

- Kenya imerekodi jumla ya visa 4,257 na vifo 117 ya #COVID19 hadi sasa

- Idadi ya wagonjwa waliopona imeongezeka na kufikia 1,459 baada ya wagonjwa 107 kupona

Soma - https://jamii.app/Corona4257-KE
#JFCOVID19_Updates
UMOJA WA MATAIFA: ZAIDI YA ASILIMIA 1 YA WATU DUNIANI NI WAKIMBIKIZI

> Takriban watu milioni 80 duniani walilazimika kuyahama makazi yao mwaka 2019 ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kurekodiwa

> 68% ya jumla ya wakimbizi duniani ni kutoka nchi 5 za Syria, Venezuela, Afganistan, Sudan Kusini na Myanmar

Soma - https://jamii.app/OngezekoWakimbizi
MALEZI: UNASHAURIWA USIMWAMBIE MWANAO KAULI ZA AINA HII

> 1. Kwanini usiwe kama dada au kaka yako?: Kauli hii humfanya mtoto ajione dhaifu kwa sababu unamlinganisha na wengine

> 2. Wasichana au Wavulana hawafanyi hivyo: Kumwambia mtoto neno hili ni kumuonesha kuwa kuna jinsia fulani bora au yenye nguvu zaidi

> 3. Hakuna mtu anamtaka mtoto kama wewe: Kuna wazazi huwajengea watoto roho ya kukataliwa tangu wakiwa wadogo sana

Zaidi, soma - https://jamii.app/KauliWatoto
DAR: HUDUMA KATIKA HOSPITALI YA AMANA ZAREJEA KAMA AWALI

> Kutokana na kupungua kwa wagonjwa wa #COVID19, Serikali imerejesha rasmi huduma zote za Matibabu zinazotolewa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana

> Watu wanaokwenda ktk Vituo vya kutoa huduma za Afya nchini wametakiwa kuvaa Barakoa, kunawa mikono na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu

Soma - https://jamii.app/RejeoHudumaAmana
JAPAN: WANANCHI WASHAURIWA KUSAFIRI, KUHUDHURIA MAONESHO ILI KUKUZA UCHUMI

- Zuio la safari za ndani lafutwa, mikusanyiko ya watu 1000 yaruhusiwa. Raia watakiwa kusafiri, kuhudhiria matamasha ili kuimarisha uchumi kufuatia janga la #COVID19

Soma https://jamii.app/UchumiJapan
FACEBOOK YAONDOA MATANGAZO YA KAMPENI YA RAIS TRUMP

- Matangazo hayo yalitumia alama ya pembe 3 nyekundu inayofanana na ile iliyotumika na utawala wa 'Nazi' wa Ujerumani

- Facebook imedai matangazo hayo yanaenda kinyume na Sera yake ya chuki

Soma https://jamii.app/FacebookTrumpKampeni
WAZIRI WA MAJI, PROF. MBARAWA ACHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR

- Prof. Makame Mbarawa amewasili Ofisi za CCM kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais

- Anakuwa Mgombea wa 10 kuchukua fomu ya kuwania Urais visiwani humo kupitia CCM

Soma https://jamii.app/MbarawaUraisZNZ
#JFLeo
KENYA YASHINDA SITI YA MWISHO KWENYE BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA (UNSC)

- Kenya imepata ushindi baada ya kupata kura 129 na kuishinda Djibouti

- Itaungana na mataifa mengine katika Baraza hilo kwa miaka 2 kuanzia Januari 01, 2021

Soma - https://jamii.app/KenyaUNSCWin
MWANAMKE WA KWANZA ACHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR

- Mwantum Mussa Sultan anakuwa Mwanamke wa kwanza kuchukua fomu ya Urais kwa tiketi ya CCM

- Ni Mwanachama wa 11 kujitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais Zanzibar

Soma - https://jamii.app/MwantumFomuUraisZnz
JAJI MKUU: RUSHWA HUSHAMIRI PALE WATU WANAPOCHELEWESHEWA HAKI YAO

> Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma ameitaka Mahakama kuacha kuchelewesha haki kwani ndiyo chanzo kikubwa cha rushwa ktk mhimili huo

> Asema rushwa hushamiri zaidi ktk taasisi zinazochelewesha haki kwani watu wanaohitaji kupata haki zao kwa wakati hulazimika kuitafuta haki hiyo kwa njia ya mkato

Soma - https://jamii.app/RushwaMahakamani
JINSI YA KUJILINDA NA #COVID19 KWA WAFANYAKAZI WASIOHUDUMIA WATEJA ANA KWA ANA

> Vaa Barakoa, nawa mikono kwa maji tiririka na sabuni

> Zingatia Social Distancing, epuka kujishika uso na mikusanyiko isiyo ya lazima

Soma > https://jamii.app/COVID19VsWafanyabiashara

#IshiNaCOVID19
UJERUMANI: WAFANYAKAZI 730 WA MACHINJIONI WAPATA #COVID19. KIWANDA CHA NYAMA CHAFUNGWA

> Maambukizi hayo yametokea katika machinjio ya jimbo la North Rhine-Westphalia (NRW)

> Mamlaka zimeamuru kufungwa kwa Kiwanda cha kuchakata nyama cha Kundi la Toennies

> Aidha, watu wapatao 7,000 wamewekwa karantini na Jimbo limeanzisha uchunguzi kujua chanzo cha maambukizi hayo

Soma - https://jamii.app/CoronaMachinjioni
#JFCOVID19_Updates