JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZANZIBAR: HUSSEIN MWINYI ACHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS

> Waziri wa Ulinzi wa JMT, Dkt. Hussein Mwinyi amechukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

> Anakuwa mtu wa 5 kuchukua fomu kwa lengo la kuomba ridhaa ya CCM kuwa mgombea

Soma https://jamii.app/MwinyiFomuZNZ

#Uchaguzi2020
ZANZIBAR: OMAR SHEHA MUSSA (CCM) ACHUKUA FOMU YA URAIS

- Omar Sheha Mussa amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM

- Wengine waliochukua fomu ni Mbwana Bakari Juma, Ali Abeid Karume, Mbwana Yahya Mwinyi na Dkt. Hussein Mwinyi

Soma - https://jamii.app/OmarShehaFomuUrais
MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA YATARAJIWA KUMALIZIWA NDANI YA SIKU 12

> Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), linatarajiwa kumaliza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi Agosti mpango utakaoamuliwa leo kwenye kikao cha Kamati Tendaji

> Hatua za robo fainali, nusu fainali na fainali zitachezwa jijini Lisbon kuanzia Agosti 12-23

Soma - https://jamii.app/UEFALeague
UGANDA: KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA KIDIJITALI

- Kutokana na #COVID19, Tume ya Uchaguzi imewataka wagombea kuendesha kampeni kwa kutumia vyombo vya habari

- Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika kati ya Januari 10 na Februari 8, 2021

Soma - https://jamii.app/KampeniUchaguziUG
CHADEMA: WANACHAMA 11 WAJITOKEZA KUWANIA NAFASI YA URAIS

> Baadhi ya Wagombea hao ni pamoja na Isaya Mwita, Tundu Lissu, Mch. Peter Msigwa, Wakili Nikodemus Gaspar, Naro Opio

> Wengine ni Lazaro Nyalandu, Dkt. Majinge Maryrose, Manyama Leornard na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe

Soma https://jamii.app/UraisTZCDM
CHINA: WALIOPEWA CHANJO YA #CORONA WATHIBITIKA KUPATA KINGAMWILI

> Matokeo yameonesha kuwa baada ya kupewa chanjo hiyo, hakuna mtu aliyekuwa na dalili mbaya na wote wamepata kingamwili dhidi ya virusi vya #COVID19

> Majaribio hayo yalifanyika kwa siku 66 chini ya uongozi wa Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa cha Henan

Soma - https://jamii.app/VaccineCorona
#JFCOVID19_Updates
KENYA: VISA VYA #CORONAVIRUS VYAFIKIA 4,044

- Visa vipya 184 vimethibitishwa baada ya sampuli 2,518 kupimwa. Idadi hiyo ni kubwa zaidi kurekodiwa kwa siku 1

- Wagonjwa waliopona hadi sasa ni 1,353 na vifo vilivyorekodiwa ni 107

Soma - https://jamii.app/Corona4044KE
#JFCOVID19_Updates
HONDURAS: RAIS JUAN HERNÁNDEZ, MKEWE WAAMBUKIZWA #CORONAVIRUS

- Rais Juan Orlando HernΓ‘ndez, Mkewe Ana GarcΓ­a CarΓ­as na wafanyakazi 2 wamepata #COVID19

- Nchi ya Honduras iliyopo Amerika Kusini imerekodi visa 9,656 na vifo 330

Soma - https://jamii.app/CoronaRaisHonduras
#JFCOVID19_Updates
#CORONAVIRUS: MWONGOZO KWA WAFANYABIASHARA NA WATOA HUDUMA KATIKA SEKTA YA UTALII

- 1. Uvaaji wa Barakoa uzingatiwe

- 2. Wahudumu, wafanyabiashara waepuke ukaribu usio lazima

- 3. Wasafirishaji wazingatie Social Distancing

- 4. Sheria kali za unawaji wa mikono ziwekwe kwenye maeneo yote yanayohusu sekta ya utalii

- 5. Waongozaji wa watalii wanapaswa kuwa na namba za mamlaka zinazohusika na suala zima la COVID19 endapo dharura itatokea ya mtalii kuonesha dalili

- 6. Waongozaji wa watalii wawasihi watalii kutojihusisha kingono na wazawa na wawaonye pia wazawa ambao hutumia ngono kama fursa ya kupata manufaa kifedha

- 7. Mamlaka ziwashauri watalii kutotumia usafiri wa umma ili kuepusha kueneza maambukizi

Soma > https://jamii.app/UtaliiVsCOVID19

#IshiNaCOVID19
RC SHIGELLA APIGA MARUFUKU WATANZANIA KUPIMWA #CORONA KENYA

> Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amepiga marufuku madereva wa Tanzania kupimwa #COVID19 Kenya baada ya kuwa wamepimwa hapa nchini

> Asema kurudiwa kupimwa kunaweza kuwasababishia matatizo ya ubongo kwa kuchokonolewa kila baada ya siku 14

Soma - https://jamii.app/UpimajiCoronaKE
BUNDA: BABA AWABAKA MABINTI ZAKE NA KUMPA MMOJA UJAUZITO

> Mama wa watoto hao, Gaudensia Michael amesema siku ya kwanza aliyomfuma mume wake kitandani na mwanaye, aliamua kusamehe kwa kuamini asingerudia

> Amewabaka watoto 2 kwa nyakati tofauti huku mmoja wa miaka 13 akipata ujauzito

Soma - https://jamii.app/BabaUbakajiWatoto
WANAFUNZI ZAIDI YA 70,000 WACHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA 5

> Wanafunzi 73,101 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha 5 mwaka 2020 na kutakiwa kuripoti Julai 18 ili kuanza masomo Julai 20

> Wanafunzi 1,572 wamechaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalumu na 9,264 wamechaguliwa kujiunga na vyuo ktk ngazi ya Stashahada

Soma - https://jamii.app/NafasiKidato5
BURUNDI: RAIS MTEULE KUAPISHWA KESHO. MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA KUHUDHURIA

> Evariste Ndayishimiye anatarajiwa kuapishwa kesho, tarehe 18 Juni 2020, badala ya Agosti kama ilivyopangwa hapo awali

> Makamu wa Rais nchini, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kuhudhuria sherehe hizo

Soma - https://jamii.app/NdayishimiyeKuapishwa
#CORONAVIRUS UPDATE: RAIS WA HONDURAS ALAZWA HOSPITALI

- Rais Juan Orlando HernΓ‘ndez ambaye pia anaumwa #COVID19 amelazwa akitibiwa Homa ya Mapafu (Pneumonia)

- Rais huyo yupo Hospitali ya Jeshi na anapatiwa dawa kwa kutumia dripu

Soma https://jamii.app/CoronaRaisHonduras
#JFCOVID19_Updates
CHINA KUSAMEHE MADENI KWA BAADHI YA NCHI ZA AFRIKA

- Rais wa China Xi Jinping ameahidi kufuta madeni yasiyo na riba kwa baadhi ya mataifa

- Pia, amesema atashirikiana na wakopeshaji wa kimataifa kusaidia nchi zilizoathirika zaidi na #Corona

Soma https://jamii.app/ChinaMadeniAfrika
ZANZIBAR: SHAMSI VUAI NAHODHA ACHUKUA FOMU YA URAIS

- Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha amechukua fomu ya kuwania Urais Zanzibar kupitia CCM

- Nahodha alikuwa Waziri Kiongozi kuanzia mwaka 2000 – 2010

Soma - https://jamii.app/ShamsiUraisZnz

#Uchaguzi2020
WADHAMINI WAIOMBA MAHAKAMA ITOE HATI YA KUMKAMATA TUNDU LISSU

> Mahakama ya Kisutu, imetoa siku 7 kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani na maombi ya wadhamini hao

> Wadhamini wamefungua maombi wakiiomba Mahakama itoe hati ya kumkamata kwani wameshindwa kumpata na kumfikisha Mahakamani

Soma https://jamii.app/KukamatwaLissu
TWITTER YATAMBULISHA HUDUMA YA UJUMBE WA SAUTI (AUDIO TWEETS)

- Watumiaji wa Mtandao huo wataweza kutuma ujumbe wa sauti wenye sekunde 140

- Hivi sasa, huduma ya Audio Tweets inapatikana kwa baadhi ya watumiaji wenye mfumo wa iOS

Soma - https://jamii.app/AudioTweets
MICHEZO: CHELSEA YAMSAJILI TIMO WERNER KUTOKA RB LEIPZIG

- Timo Werner (24) anajiunga Chelsea kwa ada ya Paundi Milioni 53 (Tsh. 153,621,501,700)

- Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Ujerumani amesaini kandarasi ya miaka 5 na anatarajia kulipwa Paundi 175,000 kwa wiki

#JFSports
ZANZIBAR: MOHAMED JAFFAR JUMANNE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS

- Mohammed Jaffar Jumanne amekuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania Urais visiwani humo kwa tiketi ya CCM

- Anakuwa mgombea wa 7 kuchukua fomu hiyo kupitia CCM

Soma https://jamii.app/CCMUraisZnz
#Uchaguzi2020 #JFLeo