JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 2020

> Maadhimisho haya yatukumbushe maendeleo ya Taifa letu hayawezi kupiga hatua bila kutilia maanani mahitaji ya watoto

> Kuzingatia mahitaji ya Watoto ni nyenzo ya maendeleo

Zaidi, Soma > https://jamii.app/SikuYaMtoto

#SikuYaMtoto
#COVID19: RAIS MAGUFULI AZUNGUMZIA WABUNGE WALIOONDOKA BUNGENI

- Rais Magufuli wakati anavunja Bunge leo amewapongeza Wananchi kwa kupambana na #CoronaVirus

- Pia, amewapongeza Wabunge kwa kuendelea na Bunge na kusema walioondoka walionesha uoga na kutojiamini

Angalia; https://youtu.be/i8fusZlszcs
CHINA: PROFESA ASHAURI SERIKALI KURUHUSU WANAWAKE KUWA NA MUME ZAIDI YA MMOJA

- Prof. Yew Kwang Ng ameshauri hivyo ili kukabiliana na ukosefu wa uwiano wa idadi ya Wanawake na Wanaume

- Amesema ushindani wa kutafuta Wanawake umekuwa mkali

Soma - https://jamii.app/WanawakeNdoaChina
EWURA YAAGIZWA KUWASAKA WANAOUZA MAFUTA TOFAUTI NA BEI ELEKEZI

- Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa siku 7 kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa Kuagiza Mafuta kuwasaka wafanyabiashara wanaoficha mafuta au kuuza juu ya bei elekezi

Soma - https://jamii.app/BeiMafuta
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020: RAIS AWATAHADHARISHA WAGOMBEA

- Rais Magufuli akivunja Bunge amewataka Wagombea kujiepusha na Shetani wa Matusi

- Amewataka wakashindane kwa hoja na kushindanisha ilani zao huku wakijua Serikali iko macho haijalala

Angalia: https://youtu.be/kW4m-cfyU4g
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020: CUF YASEMA HAITASHIRIKIANA NA CHADEMA, ACT

- Chama hicho kimesema kimejifunza kwa kilichotokea katika Uchaguzi Mkuu wa 2015

- Hata hivyo, CUF imesema ipo tayari kushirikiana na vyama vyingine vyenye nia ya dhati

Soma https://jamii.app/CUFUshirikianoUchaguzi
KOREA KASKAZINI YALIPUA OFISI YAKE YA PAMOJA NA KOREA KUSINI

- Ni baada ya kutishia kuchukua hatua za kijeshi mpakani mwa nchi hizo

- Korea Kusini imeonya itajibu shambulio hilo ikiwa Korea Kaskazini itaendelea kusababisha mvutano zaidi kati yao

Soma https://jamii.app/MvutanoKorea
MWANZA: BABA AMUUA MWANAYE KWA KUPOTEZA TSH. 500

- Anthony Lyala anatuhumiwa kumpiga mwanaye wa miaka 8 hadi kufa kwa madai ya kupoteza Shilingi 500

- Mwenyekiti wa Kijiji amesema mtuhumiwa amekuwa akijihusisha na matukio mengi ya ukatili

Soma - https://jamii.app/BabaAmuuaMtoto
ALIYEKUWA RAIS WA MGODI WA BULYANHULU NA WENZAKE, WAHUKUMIWA KULIPA BILIONI 1.5

- Deodatus Mwanyika na wenzake 2 wamekutwa na hatia ya kukwepa kodi

- Mbali na faini hiyo, Mahakama imewataka kulipa Milioni 1.5 au kutumikia kifungo cha miezi 4

Soma https://jamii.app/HukumuDeoMwanyika
NACTE YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI WA WANAFUNZI

> Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limefungua dirisha la udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi zote na litafungwa Septemba 15, 2020

> Septemba 22 hadi 29 majina ya waliochaguliwa yatawasilishwa NACTE kwa ajili ya uhakiki

Soma - https://jamii.app/UdahiliNACTE
KENYA: VISA VIPYA 133 VYA #COVID19 VYATHIBITISHWA, MAAMBUKIZI YAFIKIA 3,860

- Vimethibitishwa baada ya sampuli 3,860 kufanyiwa vipimo

- Jumla ya wagonjwa waliopona ni 1,326 na vifo vimeongezeka hadi 105 baada ya kifo 1 kurekodiwa

Soma - https://jamii.app/Corona3860-KE
#JFCOVID19_Updates
MAALIM SEIF: HOTUBA YA RAIS MAGUFULI IMESAHAU MAMBO YA MSINGI KAMA DEMOKRASIA

> Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif amesema Rais Magufuli ameongea vitu vingi wakati akifunga Bunge ila amesahau masuala ya msingi kama #Demokrasia, #HakiZaBinadamu, Tume Huru ya Uchaguzi na Uchumi imara kwa kila Mtanzania

Angalia - https://youtu.be/FPsbvCcNS_4
#CORONAVIRUS BRAZIL: VISA ZAIDI YA 34,000 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

- Visa vipya 34,918 vimeripotiwa na jumla ya maambukizi nchini humo ni 923,834

- Vifo vya #CoronaVirus vimeongezeka hadi 45, 456 na wagonjwa 464,774 wamepona

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
#JFCOVID19_Updates
RAIS MAGUFULI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS

- Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Magufuli amechukua fomu ya kugombea Urais ktk Uchaguzi Mkuu ujao kwa muhula wa pili

- Amekabidhiwa fomu katika Makao Makuu ya CCM-Dodoma na Katibu Mkuu, Dkt. Bashiru Ally

Angalia - https://youtu.be/4f3GB_Jc968
#JFLeo
WIZARA YA ELIMU YATANGAZA RATIBA YA MITIHANI KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

- Darasa la 7 wataanza mitihani ya taifa Oktoba 7-8, Kidato cha 2 Novemba 9-20, Kidato cha 4 wataanza Novemba 23

- Darasa la 4 watafanya mitihani Novemba 25 -26

Soma - https://jamii.app/RatibaMitihaniTaifa
#CORONAVIRUS BEIJING: VISA VIPYA 31 VYAREKODIWA. SHULE NA VYUO VYAFUNGWA. MICHEZO YAZUIWA

- Baadhi ya safari za ndege na treni zimepigwa marufuku hadi Julai 9

- Wananchi waliopo maeneo ya hatari wamezuiwa kusafiri nje ya Mji

Soma https://jamii.app/CoronaOutbreakBeijing
#JFCOVID19_Updates
ZANZIBAR: MBWANA YAHYA MWINYI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CCM

- Kada huyo anakuwa mwanachama wa 3 kujitokeza na kuchukua fomu ya kugombea Urais

- Wanachama wengine ambao wamechukua fomu ni Mbwana Bakari Juma na Ali Abeid Karume

Soma - https://jamii.app/FomuUraisZnz
#CORONAVIRUS: JE, NI SAHIHI KUVAA BARAKOA WAKATI WA KUFANYA MAZOEZI?

> Haitakiwi kuvaa barakoa kwa sababu zinapunguza uwezo wa kupumua vizuri

> Jilinde na #COVID19 kwa kuhakikisha kuna umbali wa angalau mita 1 kati yako na wengine

Soma https://jamii.app/BarakoaMazoezini
#IshiNaCOVID19
- Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako amesema Wanafunzi hakutakuwa na likizo hadi Desemba

- Pia amesema Shule zitalazimika kuongeza saa mbili za masomo

- Taratibu zote hizo hazitawahusisha wanafunzi wa awali (Chekechea) hadi darasa la 2

Angalia - https://youtu.be/Li6DzCX5yEo
RAIS TRUMP ASAINI AMRI KUHUSU UBAGUZI WA POLISI KWA RAIA

> Amri hiyo imezingatia kuhakiki sifa za Maofisa wa Polisi, kuongeza upashanaji wa habari ili kufuatilia Maofisa wanaoshukiwa kwa matumizi ya nguvu na kuzindua mipango ya kukabiliana na watu wenye shida ya afya ya akili, waliotumia dawa za kulevya na waliopoteza makazi

Soma - https://jamii.app/TrumpPoliceViolenc